Ingekuwaje 'irst Lady'awe MWALIMU??

Mzee wa Gumzo

Senior Member
Apr 21, 2008
197
5
"CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimewataka wake wa marais waache kufanya biashara wakiwa Ikulu kwa kisingizio cha kuanzisha taasisi za kuwasaidia wanawake.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni, Kampeni na Uchaguzi, Faustine Sungura, alisema taasisi hizo zinawanufaisha zaidi wanawake wa marais badala ya walengwa.
Alisema hiyo ni mbinu ya kuitumia Ikulu kufanya biashara, kwani kama kweli taasisi hizo zingeanzishwa kwa lengo la kuwasaidia wanawake, kusingekuwa na taasisi mpya kila anapoingia mke wa rais mpya.
Alisema Mfuko wa Fursa Sawa kwa wote (EOTF), ulio chini ya Mama Anna Mkapa, mke wa rais wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa hivi sasa umegeuka kuwa mali ya mtu binafsi, jambo ambalo kimsingi halikupaswa kuwa hivyo.
Alisema hata mke wa Rais Jakaya Kikwete naye kaanzisha mfuko wake ujulikanao kama WAMA, nao atalazimika kuondoka nao pindi Rais Kikwete atakapomaliza muda wake wa kuongoza.
“Sisi haturidhiki na matumizi ya mifuko au taasisi inayoanzishwa na marais wetu kwani inaonekana ni ujanja wa kufanya biashara kwa kutumia mwamvuli wa Ikulu,” alisema Sungura."


(Source:Tanzania Daima, Jumatatu 21/07/2008)

Hoja ya NCCR Mageuzi ni sahihi kwa mtizamo wangu.

Haya yaliwahi kusemwa huko nyuma na watu lakini ikaonekana watu wana 'wivu wa kimaendeleo'.
Tumesikia ya mama Mkapa na taasisi yake ya mikopo.Mambo yanaanza kufumuka taratibu.

Mwalimu Nyerere aliwahi kuasa kuwa "Ikulu ni mahali patakatifu".Kila anayepachafua ataumbuka.Hatujui ya WAMA baada ya miaka....

Kwani kuna tatizo gani 'first lady' wa nchi akaendelea na kazi yake ya awali.Kama alikuwa mwajiriwa wa NSSF, NMB n.k.Au alikuwa Mwalimu shule ya msingi mahali fulani kwanini asiendelee na kazi hiyo??? KWANI INGEKUWAJE MAMA KIKWETE ANGEBAKIA KAWE PRIMARY SCHOOL akishika chaki????

Kuwa mke wa rais ni kuonesha mfano na kuwa kioo cha jamii pale ulipo.Unapoacha ualimu mathalan na kuanzisha taasisi ndo kusema ualimu siyo kazi 'decent'?Kama ni suala la taasisi za kusaidia siyo lazima iwe chini ya first lady na kama ni suala la ushawishi nadhani tunahitaji kuwashawishi watu zaidi kwenye kufanya kazi na kujitegemea na siyo kuwatafutia misaada.

Hizi ni dili za kutengeneza maisha bora kwa wachache kwa kisingizio cha taifa.
Tutasikia na watoto na wajuuu wa marais nao wanapewa nafasi ikulu kuanzisha taasisi wakitumia mihuri ya ikulu na akauti binafsi.Sitashangaa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom