Ingekuwaa wewee ungefanya je? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ingekuwaa wewee ungefanya je?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by B'REAL, Nov 22, 2010.

 1. B'REAL

  B'REAL JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 3,104
  Likes Received: 171
  Trophy Points: 160


  Jamaa mmoja alikuwa akitokea shamba pamoja na mkewe. Wakiwa njiani
  waliona uyoga, wakaung'oa na kwenda nao nyumbani kwa lengo la kwenda
  kupika na kuula. Lakini kabla ya kufika nyumbani, wakahofu kwenda kula ule
  uyoga wakihisi unaweza kuwa si uyoga wa kula.


  [FONT= ]Basi wakaamua wapike uyoga kidogo,na kiasi waubakishe, halafu ule waliopika wampe mbwa wao, asipokufa mbwa basi ule waliobakisha nao wale.
  Mbwa akala uyoga ule. Wakakaa siku ya kwanza,ya pili, mbwa hajafa
  wakaamua wapike ule uyoga uliobakia nao wakala.
  Walipomaliza kula tu, mara mtoto wao wa kiume akaingia ndani akitokea shule, na kuwaeleza wazazi kuwa amemuona mbwa wao amekufa. [/FONT]  [FONT= ]Wazazi wakapigwa na butwaa wakijua basi nao mwisho wa maisha yao umefika, na muda wowote watakufa tu kwa kuwa nao wamekula uyoga kama mbwa alivyokula.
  Basi yule baba akaamua kumwambia mkewe anaomba atubu mbele yake kwa
  kuwa kifo kinamjia wakati wowote.
  Jamaa akaanza kumwambia mkewe amsamehe kwani ni maovu mengi alifanya. [/FONT]


  Kwanza msichana wa kazi waliyemfukuza akiwa na ujauzito, ule ni ujauzito wake. Mdogo wake na mkewe wa kike anayeishi naye pale ni mpenzi wake wa siku nyingi. Pia ana watoto wengine watatu nje ya ndoa, na kila mtoto ana mama yake.
  Mama akasema nashukuru kwa hayo yote, Basi naomba nami nitubu Kwako.Huyu mtoto wa kiume mdogo si wako nilizaa na Shamba boy wetu na huu ujauzito nilionao sasa ni wa mpangaji wetu humu ndani.
  Jamaa kusikia hayo akapandwa na jazba ukawa ugomvi mkubwa mule ndani.
  Wakati wakigombana, mara mtoto wao wa kwanza wa kike akaingia ndani na kukuta wakigombana.
  [FONT= ]Akawauliza ,Baba na mama mnagombania nini humu
  ndani,badala ya kwenda kuona mbwa wetu amekufa kwa kugongwa na gari kule nje?
  [/FONT]
  [FONT= ]Wazazi waliposikia kuwa mbwa amekufa kwa kugongwa na gari walibaki wanatazamana na kupigwa na bumbu wazi.
  FIKIRIA !
  KAMA NIWEWE UNGE FANYAJE?[/FONT]  Source: Mtandao
   
 2. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  kwenda kuzika mbwa na kuendelea kula uyoga maana hauna madhara yeyote
   
Loading...