Ingekuwa wewe ungefanyaje?

Suzzie

Member
Feb 25, 2009
98
12
Hebu soma hii,


Jamaa mmoja alikuwa akitokea shamba pamoja na mkewe. Wakiwa njiani waliona uyoga, wakaung'oa na kwenda nao nyumbani kwa lengo la kwenda kupika na kuula. Lakini kabla ya kufika nyumbani, wakahofu kwenda kula ule uyoga wakihisi unaweza kuwa si uyoga wa kula.

Basi wakaamua wapike uyoga kidogo,na kiasi waubakishe, halafu ule waliopika wampe mbwa wao, asipokufa mbwa basi ule waliobakisha nao wale.

Mbwa akala uyoga ule. Wakakaa siku ya kwanza,ya pili, mbwa hajafa wakaamua wapike ule uyoga uliobakia nao wakala.

Walipomaliza kula tu, mara mtoto wao wa kiume akaingia ndani akitokea shule, na kuwaeleza wazazi kuwa amemuona mbwa wao amekufa.

Wazazi wakapigwa na butwaa wakijua basi nao mwisho wa maisha yao umefika, na muda wowote watakufa tu kwa kuwa nao wamekula uyoga kama mbwa alivyokula.

Basi yule baba akaamua kumwambia mkewe anaomba atubu mbele yake kwa kuwa kifo kinamjia wakati wowote. Jamaa akaanza kumwambia mkewe amsamehe kwani ni maovu mengi alifanya. Kwanza msichana wa kazi waliomfukuza akiwa na ujauzito, ule ni ujauzito wake. Mdogo wake na mkewe wa kike anayeishi naye pale ni mpenzi wake wa siku nyingi. Pia ana watoto wengine watatu nje ya ndoa, na kila mtoto ana mama yake.

Mama akasema nashukuru kwa hayo yote, Basi naomba nani nitubu Kwako. Huyu mtoto wa kiume mdogo si wakon nilizaa na Shamba boy wetu na huu ujauzito nilionao sasa ni wa mpangaji wetu humu ndani.

Jamaa kusikia hayo akapandwa na jazba ukawa ugomvi mkubwa mule ndani.

Wakati wakigombana, mara mtoto wao wa kwanza wa kike akaingia ndani na kukuta wakigombana. Akawauliza ,Baba na mama mnagombania nini humu ndani,badala ya kwenda kuona mbwa wetu amekufa kwa kugongwa na gari kule nnje?

Wazazi waliposikia kuwa mbwa amekufa kwa kugongwa na gari walibaki wanatazamana na kupigwa na bumbu wazi.

Fikiria ni wewe ITAKUWAJE?
 
Hapo topic ya mbwa na uyoga inaisha, na Topic mpyaa inaanza.
Nalianzisha anieleze kuhusu hiyo mimba na mtoto wa kiume.
Ya kwangu ntamwambia shetani tu alinipitia.
 
halafu siku hizi mtu akicheat mbona anachukuliwa ize kwa mimi naona kama unyama fulani unampenda nje unafata nini kama mwanzo alikuwa mzuri na sasa amebadilika lazima utambue kama wewe ndio chanzo cha yeye kubadilika msapoti kwa kila kitu mwanaume asipotoka nje ni vigumu mwanamke kutoka.so ukianza anamaliza
 
Ha ha ha, huyo shetani anapitia wanaume tu, wanawake hawapitii Mkuu? If that w'd really b ur excuse
 
he he he, duuh!!! if only uyoga ndio ingekua chakula chetu cha kila siku mbona tungesikia mambo.

Labda sasa tukatafute uyoga ulio safi baada ya kula tuwaongopee wenzetu kwamba unasumu tuanze kutubu ili tupate ukweli thanks for the tip.

Kwani dada Suzzie we mwenzetu huna siri yeyote uanyo mficha nayo kaka.
 
Huyo mpangaji malaya mdandia wake za watu ama zake ama zangu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom