Ingekuwa wewe Ungefanyaje?

Masaki

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,463
752
KAMA NI WEWE IMEKUTOKEA UTAFANYAJE?

Jamaa mmoja alikuwa akitokea shamba pamoja na
mkewe. Wakiwa njiani waliona uyoga, wakaung'oa na
kwenda nao nyumbani kwa lengo la kwenda kupika na
kuula. Lakini kabla ya kufika nyumbani, wakahofu
kwenda kula ule uyoga wakihisi unaweza kuwa si uyoga
wa kula.





Basi wakaamua wapike uyoga kidogo,na kiasi
waubakishe, halafu ule waliopika wampe mbwa wao,
asipokufa mbwa basi ule waliobakisha nao wale.

Mbwa akala uyoga ule. Wakakaa siku ya kwanza,ya
pili, mbwa hajafa wakaamua wapike ule uyoga
uliobakia nao wakala.

Walipomaliza kula tu, mara mtoto wao wa kiume
akaingia ndani akitokea shule, na kuwaeleza wazazi
kuwa amemuona mbwa wao amekufa.

Wazazi wakapigwa na butwaa wakijua basi nao mwisho
wa maisha yao umefika, na muda wowote watakufa tu
kwa kuwa nao wamekula uyoga kama mbwa alivyokula.

Basi yule baba akaamua kumwambia mkewe anaomba
atubu mbele yake kwa kuwa kifo kinamjia wakati
wowote. Jamaa akaanza kumwambia mkewe amsamehe kwani
ni maovu mengi alifanya. Kwanza msichana wa kazi
waliomfukuza akiwa na ujauzito, ule ni ujauzito
wake. Mdogo wake na mkewe wa kike anayeishi naye
pale ni mpenzi wake wa siku nyingi. Pia ana watoto
wengine watatu nje ya ndoa, na kila mtoto ana mama
[FONT=Times New
 Roman] yake.[/FONT]

Mama akasema nashukuru kwa hayo yote, Basi naomba
nani nitubu Kwako. Huyu mtoto wa kiume mdogo si
wakon nilizaa na Shamba boy wetu na huu ujauzito
nilionao sasa ni wa mpangaji wetu humu ndani.

Jamaa kusikia hayo akapandwa na jazba ukawa ugomvi
mkubwa mule ndani.

Wakati wakigombana, mara mtoto wao wa kwanza wa
kike akaingia ndani na kukuta wakigombana.
Akawauliza ,Baba na mama mnagombania nini humu
ndani,badala ya kwenda kuona mbwa wetu amekufa kwa
kugongwa na gari kule nnje?

Wazazi waliposikia kuwa mbwa amekufa kwa kugongwa
na gari walibaki wanatazamana na kupigwa na bumbu
wazi.
 
Mmmmmmmmh no comment dia,KILA ASEMAE HANA DHAMBI ANAJIDANGANYA MWENYEWE
 
ningemuomba tu mwenzangu msamaha.
pia ningemsamehe mwenzangu hata kama angekuwa ni mbishi kuniomba msamaha.
ukitaka raha wasemehe wale wanaokukosea.
 
Aisee hii ni kali. sijawahi kuona. Thank you so much. Nafikiri cha maana hapo ni kusameheana tu, manake kila mmoja amemkosea mwenzake.
 
Hiyo ni Kasheshe kwakweli. Nadhani hawa Wazazi walikuwa na Matatizo makubwa sana kwenye ndoa yao. Mungu awasamehe bure kabisa nasi tusiooa atusaidie tupate Wachumba wema.

Kama yupo MSICHANA anayedhani ananafuu kidogo basi anijulishe nianze pilka za awali. Usihofu mie siangaliii dini ila ni umri tu usizidi 26.Kazi hiyo jamani wenye sifa wanweza kuomba. Teh teh eeee hhhhhh.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom