Ingekuwa vyema Usalama wa Taifa wenye umri wa 20-35,wakachomekwa kama wanafunzi wa primary na sec kuzuia viboko na uchomaji wa shule...

FrankLutazamba

JF-Expert Member
Aug 9, 2018
449
408
Kwakuwa Usalama wa Taifa ni kama kinyonga wanafiti popote,basi wangevaa uniform za shule ya msingi na sekondari na kuingia madarasani kama wanafunzi ilimradi tu wawe wanajulikana na walimu ili wasichapwe kuzuia matukio ya walimu wanaochapa ovyo kwa kuripoti mapema kwa maafisa elimu na kukaa mabwenini kama wanafunzi.

Mimi mwenyewe nilifeli hesabu Leo nikiambiwa rudi form three kusoma hesabu narudi japo Nina miaka 36,raha tu.mchango wenu jamani.
 
Usalama wa nchi hii ni jukumu la kila mtanzania, mzalendo anayeilipenda taifa lake kwa dhati.

Tupo watanzania takribani milioni 50 sasa, jenga picha kila mmoja akitimiza wajibu wake ipasavyo nchii hii itakuwa mbali kiasi gani?

Unakuta kijana anatamani kufanya kazi TISS lakini wanafunzi wa secondary wanashika miba mtaa anapoishi anashindwa kwenda kutoa taarifa ofisi ya serikali ya mtaa, kwa mjumbe au hata kituo cha police kilicho karibu yake.

Wahusika watajuje kama una mapenzi mema na taifa lako bila kuona matendo ya kizalendo?
 
Masuala mengi ya kiusalama yanaweza kutatuliwa na teknolojia ya mawasiliano bila hata ya uwepo wa watu wa usalama kila sehemu. Matumizi ya teknolojia yanaweza kuwa ni jicho la uhakika zaidi uwepo wa watu.

Kuna kila haja ya vifaa rafiki vya jicho mbadala kama vile kamera za CCTV vipate kuondolewa kabisa ushuru, ikiwa kama njia kuvifanya kuwa na bei rahisi kabisa viingiapi sokoni. Ama ikiwezekana itafutwe njia nzuri ya uwekezaji ili uwezekano upatikane wa kuzalishwa vifaa hivi kwa wingi hapa nchini.

Aidha vifaa vya aina hii vihamasishwe vile vitumiavyo umeme wa mionzi ya jua, matumizi yake yapewe kipaumbele na kufungwa ktk maeneo yote korofi ya kiusalama. Na ikiwezekana matumizi yake, utunzaji wa taarifa zilizopo ndani yake zikapate kusimamiwa na Jeshi la Polisi kupitia kamati za ulinzi na usalama ktk ngazi za mitaa, vitongoji na vijiji.
 
hicho kitu unachosema wewe kipo tayari

primary nilifundishwa na mwalimu ambae alikuwa ni TISS

secondary nilisoma na mwanafunzi TISS huyu alileta nuksi alifanya tufutiwe matokeo baada ya kusoviwa mtihani

nikarudia tena O level nikafundishwa na mwalimu TISS huyu alikuwa ni kiraka alikuja kama mwalinu wa arts lkn akatupigia mpaka plaki za phy na chemistry

A level nikasoma na kaka yangu ambae yeye alijiunga form five mara ya kwanza kipindi mm nipo rasaba lkn huwa hapandi darasa zaidi ya kuhama shule mbalimbali bad enough huu ni mwaka wa 5 anasoma vyuo mbalimbali kama first year's
Mkuu uliwajuaje kwamba wao ni TISS? Halafu wao sio malaika waweze kufundisha masomo ya Arts na Science kwa wakati mmoja kiufupi umewapamba sana ila jamaa ni kawaida sana hasa kwenye nyanja ya Elimu.
 
Ni kweli wawepo mashuleni pia,

Wangekuwepo hata kule sekondari ya Bihawana wangelijua mapema kabla yule kama jana hajakamatwa kule Kenya kwenye Shambulio la chuo cha Gharisa!

Hata kwenye nyumba za Ibada wawepo kwa dini zote ili kuweza kung’amua hila zote kama zitakuwepo kabla ya madhara kutokea kwenye jamii.

Hii itasaidia kupata taarifa za tetesi mfano za ugaidi n.k

Hii hadi vijijini huko mkoani wawepo.

Maana n nani angeweza kufikiria ya Bihawana?!
 
Wenyeviti wa mitaa kwa kushirikiana na wajumbe wa nyumba 10 wakiona wageni wanaowatilia shaka wanatakiwa watoe taarifa kwa DSO na isijulikane kuwa mwenyekiti ndiye aliyetoa taarifa kwaajili ya usalama wale na familia.

Sijui hii kama inafanyika ..

Tunapaswa kuwa proactive na siyo reactive.

Mwenyekiti wa Kijiji au hata wajumbe wa nyumba 10 wakiona wageni wasiowaelewa watoe taarifa kwa DSO moja kwa moja na walindwe.

Hii inahitaji usiri mkubwa sana!

Tetesi zozote za harufu ya Ugaidi au wahamiaji haramu ziweze kuwa detected mapema kabla ya madhara kutokea.

Kinga ni bora kuliko tiba.

Tuitunze amani ya Taifa letu ili hata vizazi vijavyo viifurahie.
 
Huo moyo wa kutoa taarifa utatoka wapi wakati wanajiona wao hawana kitu. Hawana mishahara... Tatizo linakuja hapo.. Ila kiukweli ngazi ya chini kabisa ya kijiji.. Ina umuhimu mkubwa sana kuzuia matukio na viashiria vya uharifu
 
Kwakuwa Usalama wa Taifa ni kama kinyonga wanafiti popote,basi wangevaa uniform za shule ya msingi na sekondari na kuingia madarasani kama wanafunzi ilimradi tu wawe wanajulikana na walimu ili wasichapwe kuzuia matukio ya walimu wanaochapa ovyo kwa kuripoti mapema kwa maafisa elimu na kukaa mabwenini kama wanafunzi.

Mimi mwenyewe nilifeli hesabu Leo nikiambiwa rudi form three kusoma hesabu narudi japo Nina miaka 36,raha tu.mchango wenu jamani.
hizo kazi hata police wanafanya. usalama wana kazi nyingi sana serious. si hiz za kitoto kama hizo
 
Back
Top Bottom