Ingekuwa ni wewe ungeoa?

Lekundayo2

Member
Nov 23, 2017
33
37
Mimi ni baba wa watoto wanne mama tofauti tofauti na niliowapata nilipokuwa kwenye harakati za kutafuta mchumba ili awe mke wangu kwenye historia yangu niliwahi kuwa na mwanamke niliempenda sana na kumpa kila kitu ambacho nilikuwa na uwezo nacho,watu wote waliotujua walijua nampenda mwanamke huyu, kama ilivyo mapenzi unaempenda akupend..huyu mtu alinitenda kwa kila namna na tuliachana kishingo upande na nikaanza mahusiano mapya.

Nilimpata mdada wa kabilaletu,huyu dada alinizidi umri kidogo lakini alikuwa mwanamke mwenye kumaanisha na sijui niseme ni ubaya auzuri ni kwamba wazazi wangu walimpenda sana tena mnoo, lakini ukweli uliokuwa moyoni mimi nilianzisha mahusiano nae sii kwa kuwa nilimpenda bali ni ili kumsaau yule alienitenda.

Binafsi nilijitaidi kuonyesha nipo nae lkn mawazo na fikra zangu zoote zilikuwa kwa yule mwanamke wa zamani, niliendelea nae lakini sikuwahi kumjali japo yeye alinijali sana ,matukio ya mimi kuwa na mahusiano na wanawake wengine hayakuisha japo sii ya kunifumania ready handed lakini yalikuwa mengi sana, tulisuluhisha na kuisha lakini shetani huwa sikuzote ukimlea lazima akuaibishe kwani siku ya siku pale nilipokuwa naishi waliona nimezidi kuleta mabint mara kwa mara pale.

Ndipo siku nimeingiza tuu mwanamke majirani wakamwambia nae akaja kunifumania live..nduo ilikuwa mara ya kwanza ya fumanizi na mwisho wa mahusiano yetu . Nilijitaidi kumuomba lakini kwa zaidu ya miaka miwili haikuwezekana adi alipokuja kumpata mchumba wake na nasikia wameshatoleana mahari..changamoto ziliendeleq za mahusiano lakini kuna siku nilichati na mdada niliejuana nae kipindi cha nyuma na hatukuwahi kuingia kwenye mahusiano na tuliamua kuanzisha mahusiano baada ya kuona umri unasogea.... dada huyu alikuwa na maisha yake ya wastani aliajiriwa nami wakati huo sikuwa na ajira, nilikuwa nabangaza.

Kwa kuwa nilipokuwa naishi kodi ilikaribia kuisha na sikuwa na uakika wa kazi basi tulizungumza na huyu mwanamke nikaamia kwake ..yeye aliishi mkoa mwingine na tukaanza maisha .mwanamke huyu alikuwa na watoto wawili wa kiume pamoja na kuwa nao sikujali kwani kwenye kama nilivyoeleza hapo nyuma niliwahi kuwa na mahusiano na mabint kadhaa na kupata watoto wanne hivyo niliona sii tatizo kuendelea kuwa nae na tumeendelea kuishi kama wapenzi hadi leo nikiwachukulia hawa watoto wake kama wangu, ingawa hadi leo ni mwaka na sijapata kazi nakula kwa nguvu za huyu mwanamke.

Kilichonifanya niwaletee hii thread ni kwamba Wazazi kule hawajui kama nina mwanamke na baba yangu alikataa kata kata mimi nisiije kuoa mwanamke wa kabila lingine, huyu sikuwahi kumpeleka kwa baba yangu kwa kuwa najua kabisa hawezi kumkubali... umri wangu umesogea nina 35 sasahivi....Nimejikuta njia panda kwa mengi, kwanza nitampelekaje kwetu huyu mwanamke wakati kabisa haitajiki sii tuu kwa sababu ni kabila tofauti pia kabila hilo ni kabila ambalo uko kwetu linapigwa marufuku kuliko kabila nyingine ndivyo nilivyokutauko kwenye kaya yetu.

Wana JamiiForums naomba mnifungue akili imefunga..sijui la kufanya, mzazi hapo alipo anasisitiza mimi kwenda uko makwetu kutafuta mchumba na nioe. Mzee huwa anasema yupo tayari kunisaidia kupata mwanamke...baba yangu ni wale wazee wakoloni mnoo wakishilia jambo hawabadiliki lkn pia ndugu zangu waliooa wanawake wa makabila mengine wamekuwa hawafanyi vizuri sana wamekuwa na kasoro za mara kwa mara ndio maana yeye amekazia sitakiwi kuoa nje ya kabila langu.

Mwanamke wangu huyu nilienae Sii kwamba ni mzuri sana kwa sura kama mwale wa awali na wala sii mwema sana kuliko wengine niliowahi kuwa nao ila ni vile sasa tumeshapitia mengie na kujuana vema, ndie mwanamke wa kwanza kuishi nae mwaka mzima hivyo na nikiangalia umri nao unaenda na ana ujauzito, kweli nitoke tena niende kumtafuta mwanamke mwingine kijijini nimuache kwa kuwa ni wa kabila langu tuu kama wazazi wanavyotaka ama nifanye nini..namuonea huruma sana huyu dada amejitoa mno kwangu amevumilia kasoro zangu nyingi pia amejitaidi kunibadilisha kitabia sana...mimi hapa nimebaki njia panda naomba mnishauri kwani mzazi wangu ni yule asielewa jambo lolote.
 
1,Tafuta kazi kwanza mkuu !

2, fuata moyo wako ! Unawaolea wazazi ? Ndg ? Ukoo ? Umesema mnaelewana vyema , mmepitia mengi , !!!

Nimesoma kwa shida Sana, jitahidi uwe na hati nzuri, zingatia kaida za uandishi, weka vituo na aya panapostahili !
 
35yrs bdo hujajua namna ya kuamua moyoni mwako..? Tulio wengi humu tutakushauri lkn kumbuka kuwa wewe ndo mwenye maamuz ya mwisho juu ya huyo mwanamke..!! Remember always do what your heart need.
 
Unanizidi mbali mkuu mimi ni 27 hata mimi nimepitia situations na mabinti kuna huyo alinitenda niliumia sana ndio alikua kila kitu nili risk kila kitu kwake ila havikutosha

sikua na hela za kumpa vitu hasa alivyokua anataka so alitokea boss wake huyo kamkula af nikafuma ma conv yote so nikatemana nae niko broke ile mbaya sikua na kazi nlikua nakaa gheto kwangu ila most vitu vingine alisaidia pia

So kipindi niko broke baada ya kuachana nae nilipata hasira sana kukosa vitu ambavyo alipewa na boss wake hadi akaliwa so maumivu yangu nili invest kutafuta kitu cha kufanya kazi na mtaji maana nina career flani sikua nalala kwa mawazo nikisoma huku na kule

Kukicha mimi nina ma idea tu kutafuta ishu maofisi tofauti tofauti nilizunguka sana nikaacha namba zangu sehemu kibao tu

Siku moja nlipata simu kampuni moja m kuna project nikapata ya muda nikapiga ilikua ya hela kidogo katika ile project nikakutana na mtu ni mkubwa kampuni nyingine alipenda ujuzi wangu wakaniita kule nikapigwa project nyingine kubwa hii ilikua na pesa ndefu

Nikapiga nikapata mtaji nikafumgua ofisi zangu nikahamia nyumba nzuri kdg na kausafiri nikapata

Asee asikwambie mtu ukitoka kua maskini kuna feeling unapata mapenzi unaona sio kitu yule manzi alinisumbua sana baada ya kuona nna drive ila nlimtosa sa hv mimi ndo nachagua nioe yupi na lini nyumbani wananisikiliza na wanawake wananisikiriza

So mkuu tafuta pesa ukizipata hata ukiwa ja miaka 50 utagombaniwa na watoto wenye 20
 
Mimi ni baba wa watoto wanne mama tofauti tofauti na niliowapata nilipokuwa kwenye harakati za kutafuta mchumba ili awe mke wangu kwenye historia yangu niliwahi kuwa na mwanamke niliempenda sana na kumpa kila kitu ambacho nilikuwa na uwezo nacho,watu wote waliotujua walijua nampenda mwanamke huyu, kama ilivyo mapenzi unaempenda akupend..huyu mtu alinitenda kwa kila namna na tuliachana kishingo upande na nikaanza mahusiano mapya.

Nilimpata mdada wa kabilaletu,huyu dada alinizidi umri kidogo lakini alikuwa mwanamke mwenye kumaanisha na sijui niseme ni ubaya auzuri ni kwamba wazazi wangu walimpenda sana tena mnoo, lakini ukweli uliokuwa moyoni mimi nilianzisha mahusiano nae sii kwa kuwa nilimpenda bali ni ili kumsaau yule alienitenda.

Binafsi nilijitaidi kuonyesha nipo nae lkn mawazo na fikra zangu zoote zilikuwa kwa yule mwanamke wa zamani, niliendelea nae lakini sikuwahi kumjali japo yeye alinijali sana ,matukio ya mimi kuwa na mahusiano na wanawake wengine hayakuisha japo sii ya kunifumania ready handed lakini yalikuwa mengi sana, tulisuluhisha na kuisha lakini shetani huwa sikuzote ukimlea lazima akuaibishe kwani siku ya siku pale nilipokuwa naishi waliona nimezidi kuleta mabint mara kwa mara pale.

Ndipo siku nimeingiza tuu mwanamke majirani wakamwambia nae akaja kunifumania live..nduo ilikuwa mara ya kwanza ya fumanizi na mwisho wa mahusiano yetu . Nilijitaidi kumuomba lakini kwa zaidu ya miaka miwili haikuwezekana adi alipokuja kumpata mchumba wake na nasikia wameshatoleana mahari..changamoto ziliendeleq za mahusiano lakini kuna siku nilichati na mdada niliejuana nae kipindi cha nyuma na hatukuwahi kuingia kwenye mahusiano na tuliamua kuanzisha mahusiano baada ya kuona umri unasogea.... dada huyu alikuwa na maisha yake ya wastani aliajiriwa nami wakati huo sikuwa na ajira, nilikuwa nabangaza.

Kwa kuwa nilipokuwa naishi kodi ilikaribia kuisha na sikuwa na uakika wa kazi basi tulizungumza na huyu mwanamke nikaamia kwake ..yeye aliishi mkoa mwingine na tukaanza maisha .mwanamke huyu alikuwa na watoto wawili wa kiume pamoja na kuwa nao sikujali kwani kwenye kama nilivyoeleza hapo nyuma niliwahi kuwa na mahusiano na mabint kadhaa na kupata watoto wanne hivyo niliona sii tatizo kuendelea kuwa nae na tumeendelea kuishi kama wapenzi hadi leo nikiwachukulia hawa watoto wake kama wangu, ingawa hadi leo ni mwaka na sijapata kazi nakula kwa nguvu za huyu mwanamke.

Kilichonifanya niwaletee hii thread ni kwamba Wazazi kule hawajui kama nina mwanamke na baba yangu alikataa kata kata mimi nisiije kuoa mwanamke wa kabila lingine, huyu sikuwahi kumpeleka kwa baba yangu kwa kuwa najua kabisa hawezi kumkubali... umri wangu umesogea nina 35 sasahivi....Nimejikuta njia panda kwa mengi, kwanza nitampelekaje kwetu huyu mwanamke wakati kabisa haitajiki sii tuu kwa sababu ni kabila tofauti pia kabila hilo ni kabila ambalo uko kwetu linapigwa marufuku kuliko kabila nyingine ndivyo nilivyokutauko kwenye kaya yetu.

Wana JamiiForums naomba mnifungue akili imefunga..sijui la kufanya, mzazi hapo alipo anasisitiza mimi kwenda uko makwetu kutafuta mchumba na nioe. Mzee huwa anasema yupo tayari kunisaidia kupata mwanamke...baba yangu ni wale wazee wakoloni mnoo wakishilia jambo hawabadiliki lkn pia ndugu zangu waliooa wanawake wa makabila mengine wamekuwa hawafanyi vizuri sana wamekuwa na kasoro za mara kwa mara ndio maana yeye amekazia sitakiwi kuoa nje ya kabila langu.

Mwanamke wangu huyu nilienae Sii kwamba ni mzuri sana kwa sura kama mwale wa awali na wala sii mwema sana kuliko wengine niliowahi kuwa nao ila ni vile sasa tumeshapitia mengie na kujuana vema, ndie mwanamke wa kwanza kuishi nae mwaka mzima hivyo na nikiangalia umri nao unaenda na ana ujauzito, kweli nitoke tena niende kumtafuta mwanamke mwingine kijijini nimuache kwa kuwa ni wa kabila langu tuu kama wazazi wanavyotaka ama nifanye nini..namuonea huruma sana huyu dada amejitoa mno kwangu amevumilia kasoro zangu nyingi pia amejitaidi kunibadilisha kitabia sana...mimi hapa nimebaki njia panda naomba mnishauri kwani mzazi wangu ni yule asielewa jambo lolote.
KUISHI NYUMBANI KWA MWANAMKE NI BOMU UNALOLISUKA, IPO SIKU LITAKULIPUKIA...

KWANZA ONDOKA HAPO TAFUTA KWAKO HATA KAMA CHINI YA MTI NI KWAKO, YEYE NDIO AKUFUATE...

ANYWAY, SWALI LANGU JE YEYE KWAO WANAKUKUBALI?

KAMA WANAKUKUBALI NENDA KAOE HUYO MWANAMKE...

ACHANA NA HABARI ZA WAZAZI NYUMBANI...WAPE TAARIFA SIO UOMBE RUHUSA...

MWANAMKE NDIO AOZESHWA, RIDHAA YA WAZAZI WA BINT NDIO YATAKIWA, SIO WAZAZI WA KIUMENI, LABDA USHAURI TU AMBAO VILEVILE HAUTOFANYIWA KAZI IKIBIDI....

ILA TOKA KWANZA HAPO KABLA HUJAFUKUZWA KWA UDHALILI, IPO SIKU ATAKUBADILIKIA HUTOAMINI, USINUNUE KITU UKAKICHANGANYA NA VYAKE, SIKU UTAVIACHA VYOTE...

TAFUTA KWAKO MWANAUME MWENZANGU, HUENDA HIYO TABIA ILIYOBADILIKA NI KUTOKA MWANAUME RIJALI MPAKA KUWA ZEZETA...
 
Una watoto wanne, una miaka 35, una mwanamke mwenye watoto wawili, ana mimba yako!
Bado unataka umuache utafute mke na kazi hauna?
Unafeli mr.
Huyo ndiyo mkeo ishi nae tafuta msingi fanya biashara au Kama ana uwezo akuwezeshe ufanye biashara kama amejitoa hivyo kwako anakupenda na anakuheshimu utaishi maisha yenye furaha yasiyoumiza Sana kichwa
 
Umesema una umri wa miaka 35

Hivi ni malezi ndio mabovu hau mlo duni? Hawa watoto wetu wa kiume tunakosea wapi kuwalea
 
Kama una mtoto WA kiume mlee vizur
Hata nguo ajue hata kujifulia plus kujipikia

Maaana dhaaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom