Ingekuwa ni leo, ungesomea hicho unachokifanya sasa?

Tunafundishwa elimu ya kuja kutafuta pesa ila hatufundishwi tabia za pesa. Matajiri wakubwa huwalisisha watoto wao elimu ya kusimamia Mali na kuziendeleza nipewe Mimi sasa.. mtaona kila rangi.. mkuu niheri ufundishwe uchumi na mfanya biashara kuliko walimu tu ambao hawafanyi hicho kitu.. ukitaka kujifunza kitu chochote nenda kwa mwenye experience ye ndo anaona hali ikoje.. ukitaka majibu ya maswali yako mfate kamsome au msikilize Robert kiyosaki hutatoka bure.

Nimesoma vitabu kadhaa vya huyo bwege, nafikiri pia vimechangia kufidisha interest kwenye njia yangu... unasoma halafu unajiona fwala kabisa sijui unaishije tu!
 
Wakati nachagua Cha kusoma...sikua najua vitu vingi...Nlichagua degree ilw kwasababu Kaka yangu nae alisoma hiyo..akawa na KAZi nzuri..

elimu yangu ya Mambo nlosomea na upana wa degree za kuchagua ulikua finyu...

Sijutiiii nlichosomea...Hayo yashapitaga.

Hujutii, 'hayo yalishapitaga'... hiyo kauli ina majuto ndani yake sema hakuna namna!

Je, uliuona kweli uzuri wa kazi ya kaka’ko?

Maana ni kawaida kuuona msitu kwa mbali, ila ukiufikia wala huuoni waona miti tu... wakati huo mamia wanakutamania.
 
Kwa kwel niliyoyapitia Mimi basi tu,nmeshasoma kozi tatu tofauti,hii imechangiwa na kumaliza elimu ya secondary bila kujua unataka kuwa nani na ipi ni kozi ambayo ni rahis kuingia kwenye system ya serikal na yenye mshahara mzuri,jiwe nalo limechangia kunivuruga,kwa wanangu,ntawaandaa mapema kabisa toka wakiwa primary, wajiandae kusomea ktu kzur chenye chance na mshahara mzuri
 
Nimekwambia sijutii naamanisha SIJUTII...
Sasa Nawaza unalazimisha Nini KWAMBA NAJUTIA..

njia nlopita ndio njia nlochagua ..haikua mbaya na pengine ningechagua njia nyingine nisingeipata hii degree..

SIJUTIJ degree yangu Ya UDSM...Kweli kabisa
 
Kama unajutia na bado unaamini katika mshahara, hivyo unafikiria kusoma tena kozi ya 4!

Nawaonea huruma hao watoto wako.
 
Nilikariri Akimedesi principo nikiwa form 1, nikifikiri nitakuja kuwa nahodha wa meli. Gravity, acceleration, velocity...
5-6 nikasoma ma Bernoulli principle nikiamini nitakuwa engineer wa ndege,

Siku hizi nafikiri bora ningesomea history ya kina Nzwangedaba na Berlin conference, huenda ningekuwa dalali mzuri mbogamboga sokoni! Mjumbe au diwani kata fulani napokea tu bahasha za vikao vya chaguzi na miradi ya maendeleo.

What a waste?? Mitaala inatupeleka shule ili tusisumbue mitaani na balehe!

Everyday is Saturday.............................. :cool:
Mitaala ya kitanzania ya kijinga sana. Sijui wakuu hawaoni hili..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekwambia sijutii naamanisha SIJUTII...
Sasa Nawaza unalazimisha Nini KWAMBA NAJUTIA..

njia nlopita ndio njia nlochagua ..haikua mbaya na pengine ningechagua njia nyingine nisingeipata hii degree..

SIJUTIJ degree yangu Ya UDSM...Kweli kabisa

Umeona ukazie UDSM kabisa, hongera mkuu kweli hujutii... furahia chaguo lako sahihi.
 
Kama unajutia na bado unaamini katika mshahara, hivyo unafikiria kusoma tena kozi ya 4!

Nawaonea huruma hao watoto wako.
Naweza kusoma tena,lakin sahv nawaza kujipanua katika harakat za ktaa,maana naona ndugu zangu wameajiriwa lakin wanalia tu,Mimi kila siku nna pesa na akiba kubwa,lakin walioajiriwa hata akiba hawawez weka
 
Nakushauri jikite zaidi kwenye hizo mishe za kitaa, ujinga wa kuajiriwa ni pamoja na matarajio ya ndugu... wanajua mshahara ni uhakika na ukiingia tu shida zao kama zote!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom