Ingekuwa ni leo, ungesomea hicho unachokifanya sasa?

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
14,491
26,978
Hii ni kwa wale waliosomea taaluma fulani na hivyo kuendesha maisha kupitia taaluma hizo.

Ikumbukwe ni enzi za shule, kiumri na ukomavu ni mdogo usiotosha kujua hasa nini kesho yako inahitaji.

Unaweza kujikuta umechagua njia yoyote ili mradi tu kulingana na ufaulu wa masomo yako, au basi kwa ushauri wa watu fulani kama walezi/wazazi au marafiki.

Ukishakuwa mkubwa unajikuta uko hapo, inaweza kuwa ulifanya chaguo sahihi na unafurahia au ndo basi tena huna namna inakubidi uji-adjust tu ili maisha yaende.

Binafsi nilisomea kozi fulani ya AFYA, ilikuwa ni sifa na heshima tu ila kumbe sina WITO huo kabisa na FURAHA yangu ni kupiga PESA sio kuokoa MAISHA ya WATU.

Leo ingekuwa ndio juzi, nisingechagua kusomea hiki ninachokifanya leo... nafanya kama wajibu lakini sijioni kabisa kuishi maisha yangu halisi.

Je, ni mimi pekee niliyeingia cha kike?
 
Ningalikuwa Mimi ningalisomea uchumi na biashara tu yani tokea mdogo unacheza na uchumi tu halafu haya mambo mengine yanakuwa ile n.k yani nakadharika! Bata kabisa..

Tangia mdogo unacheza na uchumi, kivipi?
 
Nilikariri Akimedesi principo nikiwa form 1, nikifikiri nitakuja kuwa nahodha wa meli. Gravity, acceleration, velocity...
5-6 nikasoma ma Bernoulli principle nikiamini nitakuwa engineer wa ndege,

Siku hizi nafikiri bora ningesomea history ya kina Nzwangedaba na Berlin conference, huenda ningekuwa dalali mzuri mbogamboga sokoni! Mjumbe au diwani kata fulani napokea tu bahasha za vikao vya chaguzi na miradi ya maendeleo.

What a waste?? Mitaala inatupeleka shule ili tusisumbue mitaani na balehe!

Everyday is Saturday.............................. :cool:
 
Tangia mdogo unacheza na uchumi, kivipi?
Tunafundishwa elimu ya kuja kutafuta pesa ila hatufundishwi tabia za pesa. Matajiri wakubwa huwalisisha watoto wao elimu ya kusimamia Mali na kuziendeleza nipewe Mimi sasa..🤣 mtaona kila rangi.. mkuu niheri ufundishwe uchumi na mfanya biashara kuliko walimu tu ambao hawafanyi hicho kitu.. ukitaka kujifunza kitu chochote nenda kwa mwenye experience ye ndo anaona hali ikoje.. ukitaka majibu ya maswali yako mfate kamsome au msikilize Robert kiyosaki hutatoka bure.
 
Nilikariri Akimedesi principo nikiwa form 1, nikifikiri nitakuja kuwa nahodha wa meli. Gravity, acceleration, velocity...
5-6 nikasoma ma Bernoulli principle nikiamini nitakuwa engineer wa ndege,

Siku hizi nafikiri bora ningesomea history ya kina Nzwangedaba na Berlin conference, huenda ningekuwa dalali mzuri mbogamboga sokoni! Mjumbe au diwani kata fulani napokea tu bahasha za vikao vya chaguzi na miradi ya maendeleo.

What a waste?? Mitaala inatupeleka shule ili tusisumbue mitaani na balehe!

Everyday is Saturday.............................. :cool:
Mkuu, you've nailed it!!
 
Mimi na watoto wangu watatu wote ni wanafunzi japo wao shule wanafungua jumatatu.

Hongera sana mkuu kama ulichagua sahihi, maana kuna wengine hujiendeleza zaidi na zaidi ili kupunguza majukumu... pengine ili kuwa msimamizi tu.

Hofu yangu ni ikiwa utawachagulia watoto, kwa kudhani sahihi kwako ni kwao pia!
 
Wakati nachagua Cha kusoma...sikua najua vitu vingi...Nlichagua degree ilw kwasababu Kaka yangu nae alisoma hiyo..akawa na KAZi nzuri..

elimu yangu ya Mambo nlosomea na upana wa degree za kuchagua ulikua finyu...

Sijutiiii nlichosomea...Hayo yashapitaga.
 
Hii ni kwa wale waliosomea taaluma fulani na hivyo kuendesha maisha kupitia taaluma hizo.

Ikumbukwe ni enzi za shule, kiumri na ukomavu ni mdogo usiotosha kujua hasa nini kesho yako inahitaji.

Unaweza kujikuta umechagua njia yoyote ilimradi tu kulingana na ufaulu wa masomo yako, au basi kwa ushauri wa watu fulani kama walezi/wazazi au marafiki.

Ukishakuwa mkubwa unajikuta uko hapo, inaweza kuwa ulifanya chaguo sahihi na unafurahia au ndo basi tena huna namna inakubidi uji-adjust tu ili maisha yaende.

Binafsi nilisomea kozi fulani ya AFYA, ilikuwa ni sifa na heshima tu ila kumbe sina WITO huo kabisa na FURAHA yangu ni kupiga PESA sio kuokoa MAISHA ya WATU.

Leo ingekuwa ndo juzi, nisingechagua kusomea hiki ninachokifanya leo... nafanya kama wajibu lakini sijioni kabisa kuishi maisha yangu halisi.

Je, ni mimi pekee niliyeingia cha kike?
Ningejua mambo ya kusoma ni hivi ningekuwa mfugaji tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom