Ingekuwa ma-rais wanaazimwa kwa muda, mi ningempendekeza kagame aje tz | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ingekuwa ma-rais wanaazimwa kwa muda, mi ningempendekeza kagame aje tz

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by CPA, Apr 22, 2011.

 1. CPA

  CPA JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 737
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Pamoja ya kuwa kagame anashutumiwa kuwa ni miongon mwa mwanzilishi wa machafuko na umwagaji wa damu '94, lakin huyu jamaa ni kiboko. Kutoka nchi iliyoharibiwa na vita mpaka kuwa nchi inayokuwa kwa kasi sio kazi ndogo. Sasa hivi anajenga reli ya kufika tz, ana masterplan ya 50yrs to come ya nchi yake. Wanafunzi wote wa primary wanacomputer, kigali ni mji unaopendeza, wafanyakaz wa serikali wanamikataba wa miaka 3, 3, ukiburunda after 3yrs kwenu analetwa mwingine. Magar ya kifahar wanamiliki watu binafsi tu. Kipindi cha uchaguz alikuwa anatumia gar lake aina la benz, dereva mwenyewe na mke wake, na magar mengine 2 binafsi kwa ajiri ya walinzi wake. Amekomesha ukabila, wanajeshi wanapiga dolia, wakimkamata mwizi,kibaka,jambaz hawampigi wanawapigia cmu polisi wanakuja kumchukua. Lakin cha ajabu mialiko ya kuja tz anaikwepa anatuma wawakilishi wake tu, cjui ki2 gan kimejificha. Huo ni mtazamo wangu tu, nawakilisha
   
 2. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2011
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  labda na sie tukipigana ndo tutaheshimiana. si unaona kenya sasa hivi wanaheshimiana sana.
   
 3. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #3
  Apr 22, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Kaka hao ndo viongozi,wenye miono ya mbali,hapa kwetu tuna watawala na sio viongozi,
   
 4. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,173
  Likes Received: 1,174
  Trophy Points: 280
  Kagame ni mtu makin mno anayetambua analolifanya na kwa wakati muafaka.
   
 5. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu naona unajichanganya hapo kwenye red, benz sio gari la kifahari? na hapo kwenye blue jaribu kuandika vizuri hii thread yako, Paul Kagame the new Hitler
   
 6. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,173
  Likes Received: 1,174
  Trophy Points: 280
  mku nackia eti baba yake na Raila odinga aliwahi kuwaomba wakenya wamruhusu akae ikuru japo kwa siku 1, cjui alikuwa na maana gani? Na africa hiyo ndo type ya viongozi 2lonao specificaly TZ
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hana muda wa porojo na mipasho isiyo na kikomo. Kikao cha nusu saa mnafanya kwa siku mbili. Time wasters.
   
 8. CPA

  CPA JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 737
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  ndio maana nikasema wanamiliki watu, binafsi, hilo benz ni la kwake mwenyewe na sio serikali. Ujumbe umefika, hata kama ni hitler lakini maendeleo yanaonekana. Wananchi wake wanamkubari
   
 9. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  CPA hapo kwenye blue kuwa makini na kiswahili chako samahani lakini, Kagame muuaji mkubwa wapinzani wake wengi wamekimbia nchi
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  Apr 22, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  ndo maana hawezi kukaa meza moja na ****** maana anaona anampotezea muda tu ..we kwenye mkutana rais anashika simu anajibu meseji ..sasa huyo rais au diwani
   
 11. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hahaaaaa umenifurahisha sana chatu dume....huyu atakuwa ni muraaa au anatokea kyabakariiii
   
 12. k

  kalechee Member

  #12
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni dikteta anaependa nchi yake na watu wake sana
   
 13. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,394
  Trophy Points: 280
  Juzi kapewa nishani ya utawala bora, kwa sasa KASI YA UKUAJI UCHUMI DUNIANI YA RWANDA NI SAWA NA YA SINGAPORE!
   
 14. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #14
  Apr 22, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Tanzania tungeazimwa Col.Gaddafi japo kwa mwaka mambo yangeenda vizuri
   
 15. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #15
  Apr 22, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Si unajuwa mwafrica yaani alikuwa anamaanisha kuwa akipewa dakika moja tu atakuwa amebeba kila kitu kitakachowezekana kubebwa,lakini nasikia hawaku mpa
  kama hujashiba ktk sufuria unazani utashiba ktk kijiko bana?

  Watawala wa Tz na Africa tuna waza kujilimbikizia mali zaidi
  ebu mwangalie yule raisi wa misri inasemekana ndie rais tajiri africa akifuatiwa na Riziwan Bongo hehehehehehe
   
 16. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #16
  Apr 22, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ni bora uwe muuaji lakini nchi inasonga mbele kimaendeleo,uchumi na mambo mengine,ebu angalia china,hakuna kutumia face book,google,watu tillion kadhaa lakini nchi hiyo inapaa kiuchumi
  Huwezi kuendesha nchi bila kuwa na kaelement ka udictactor mambo yatakushinda tuu,ni lazima uwe mbishi sio kila kitu sawa
  hata Idd amini dada umafia wake ulisababisha nchi kuwa na uchumi mzuri hata waingereza walikwenda kumpigia magoti na kumwomba msaada,lakini hatuyaoni hayo kwa kuwa alitaka kutupiga
   
 17. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #17
  Apr 22, 2011
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  CPA kweli umekua mateka wa propaganda za kagame akisaidiwa na marekani na nchi za magharibi! Pole sana mdogo wangu! Kwa taarifa yako hakuna kiongozi balaa kwa mustakabali wa taifa lake kama kagame! Kwanza uliyoongea mengi sio kweli!,

  Nikianza na kubwa la kukomesha ukabila hajafanya la maana! Anakandamiza sana wahutu na anajaribu kuweka chuki zaidi kwa kuhubili na kuonesha mafuvu kwamba wahutu ni wauaji wakati yeye ndio muuaji mkubwa! Kwenye safu ya uongozi wa juu na jeshini hakuna wahutu na mhutu yeyote mwenye pesa atazushiwa lolote ili afilisiwe na kufungwa ikibidi! Kagame ni mkabila kwa vitendo ndio maana hawezi kukomesha ukabila kwa maneno!

  Mpango wa miaka hamsini umeusoma?, ni mzuri? Au kwako kuwepo mpango tu hata kama ni mpango kandamizi ni jambo la kusifiwa?

  Kuhusu reli nakuomba CPA acha uzushi!, kwa haijaanza kujengwa pili sio yeye bali ni jumuia ya africa mashariki!, ni mpango wa nchi zote husika. Hata umeme utazalishwa rusumo kwa mpango huo huo!

  Kwenye kikao kilichopita hakuja kwa sababu mwenyekiti alikua mhutu, rais wa burundi!

  Pili, maendeleo yanayosemwa sio sawa na hali halisi wala hayajazidi yaliyokuwepo wakati wa Habyarimana! Kagame amewekwa na marekani kama mlango wa kuingilia kongo. Si unajua kipindi cha habyarimana rwanda na mobutu congo, marekani ilikua haifaidiki sana congo? Jamaa ni bonge la kibaraka!

  Mji wa kigali ni mji mdogo sana, unaweza kutembea kwa miguu ukafika kila kona ndani ya siku moja! Haufikii hata robo ya Dar!, ni kama singida au kahama vile kwa ukubwa!
   
 18. U

  Uswe JF-Expert Member

  #18
  Apr 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  yaani asubuhi leo my wife na mie tulikua tunaongea kuhusu huyu bwana na yule wa burundi, huwezi amini jinsi wanavyofanya vitu vikubwa kwa nchi zao, si tuko busy tunavua magamba
   
 19. c

  chetuntu R I P

  #19
  Apr 22, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jambo msilolijua, kwanza population ya rwanda ni ndogo, mbili kagame ananufaika na congo -kinshasha . Rejea mgogoro wa Goma. Wanyamulenge wanasaidiwa na rwanda. Na ni wanyarwanda walioingia congo kwa mpango maalum. Anajichotea madini congo, kabila ni mjombake (mama wa kabila mnyarwanda) popote walipo duniani hawatupani.
   
 20. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #20
  Apr 22, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu umenichekesha sana Reference zako za maendeleo, facebook na Google sio maendeleo Google ni search engine wachina wanazo kibao, na facebook ni mtandao wa kijamii kama vile JF wachina wanayo mingi tu, kingine hiyo data ya watu tillioni kadhaa sijui umeitoa wapi dunia mpaka sasa ina watu 7 billion, China ina watu 1,341 billion, turudi Rwanda wapo wachache ina watu 11 million tu
   
Loading...