Ingekuwa Kenya leo TV zote mjadala mkuu ungekuwa hukumu ya Jaji dhidi ya Tundu Lissu

Kamgomoli

JF-Expert Member
May 3, 2018
1,865
3,801
Sijui ni hofu,woga,ukada au nini? Vyombo vya habari vya TZ havitulishi habari vile inavyotakiwa nadhani ndio maana watanzania tunaishi kwa habari za umbea na ushabiki usiokuwa na maana, kwa sababu tunapewa habari za juu juu mno na vyombo vyetu vya habari. Hakuna uchambuzi makini wa mambo hasa yanayotokea ndani ya nchi yetu.

Juzi tu hapa tumesikia viongozi wa juu wakitoa matamko mazito ya kutoa vipigo vizito kwa wananchi( Mbeya). Vyombo vya habari kimyaaa. Kwao hiyo sio story.

Kama ingekuwa Kenya leo wanasheria nguli wangeongoza mijadala mizito kujadili kilichoamuliwa jana na mahakama dhidi ya kesi ya Tundu Lissu kupinga maamuzi ya Spika kumvua ubunge.

Habari za Konki Likwidi ndo zinapewa mjadala mzito mpaka bungeni cha ajabu hili eti linaonekana ni la kipuuzi tu. Hii ni hatari kwa afya ya akili ya wananchi wetu. Huenda ndio maisha tulioyachagua.
 
Sijui ni hofu,woga,ukada au nini? Vyombo vya habari vya TZ havitulishi habari vile inavyotakiwa nazani ndio maana watanzania tunaishi kwa habari za umbea na ushabiki usiokua na maana, kwa sababu tunapewa habari za juu juu mno na vyombo vyetu vya habari. Hakuna uchambuzi makini wa mambo hasa yanayotokea ndani ya nchi yetu. Juzi tu hapa tumeskia viongozi wa juu wakitoa matamko mazito ya kutoa vipigo vizito kwa wananchi( Mbeya). Vyombo vya habari kimyaaa. Kwao hiyo sio story. Km ingekua Kenya leo wanasheria nguli wangeongoza mijadala mizito kujadili kilichoamuliwa jana na mahakama dhidi ya kesi ya Tundu lisu kupinga maamuzi ya Spika kumvua ubunge. Habari za Konki likwidi ndo zinapewa mjadala mzito mpaka bungeni ja ajabu hili eti linaonekana ni la kipuuzi tu. Hii ni hatari kwa afya ya akili ya wananchi wetu. Huenda ndo maisha tulioyachagua.

#baharia ana trend
 
Nyie si mnao wanasheria wasomi kwa nini wasiongoze hiyo mijadala? Au wamepigwa ganzi wapo icu kwa majigambo yao?
 
Sijui ni hofu,woga,ukada au nini? Vyombo vya habari vya TZ havitulishi habari vile inavyotakiwa nadhani ndio maana watanzania tunaishi kwa habari za umbea na ushabiki usiokuwa na maana, kwa sababu tunapewa habari za juu juu mno na vyombo vyetu vya habari. Hakuna uchambuzi makini wa mambo hasa yanayotokea ndani ya nchi yetu.

Juzi tu hapa tumesikia viongozi wa juu wakitoa matamko mazito ya kutoa vipigo vizito kwa wananchi( Mbeya). Vyombo vya habari kimyaaa. Kwao hiyo sio story.

Kama ingekuwa Kenya leo wanasheria nguli wangeongoza mijadala mizito kujadili kilichoamuliwa jana na mahakama dhidi ya kesi ya Tundu Lissu kupinga maamuzi ya Spika kumvua ubunge.

Habari za Konki Likwidi ndo zinapewa mjadala mzito mpaka bungeni cha ajabu hili eti linaonekana ni la kipuuzi tu. Hii ni hatari kwa afya ya akili ya wananchi wetu. Huenda ndio maisha tulioyachagua.
Hi Tz yetu inaitwa the 'sleeping giant'..... haina sekita yoyote inayo fanya ipasavyo........
 
Hapo tatizo ni vyombo vya habari... Kwani wamekatazwa!?
 
Kitu cha kwanza ni udhibiti wa vyombo vya habari na wana habari wenyewe.

Kwani hukujua tu!?
 
Mkuu na wewe ungeenda hata tbc ukawa mfano.. hlf kaa ukijua mambo yanayokujaza wewe wengine hayapo akilini pao watu wanamajukumu mbalimbali bado waongeze na ya lisu!
 
Kisa Lissu?watu wana wagonjwa huko na gharama za matibabu ziko juu sasa tuache kujadili haya we unataka tumjadili Lissu tu na kesi zake kwa faida ya nani?
 
Kwahiyo Kenya jambo hupewa nafasi kubwa moja tuu kwani mengine si ya msingi? Basi vyombo vyote ni viko na lengo maalumu.
 
Nyie si mnao wanasheria wasomi kwa nini wasiongoze hiyo mijadala? Au wamepigwa ganzi wapo icu kwa majigambo yao?
Soma kwanza ndio uchangie,umeambiwa vyombo vya habari wewe kwa ulimbukeni unaibuka na wanasheria,sijui nao ni vyombo vya habari
 
Press yote inaunga mkono juhudi,muda huu tunajadili xenophobic attacks huko SA na nini Tanzania tulisaidia kwenye ukombozi wao!!!!
 
Back
Top Bottom