Uchaguzi 2020 Ingekuwa katika Nchi za wenzetu, Nyalandu na wenzake wangejitoa na kumuachia Lissu

abel p

Member
May 8, 2020
24
75
Membe mwenzake ameshaonyesha dalili za kumuunga mkono Lissu ila yeye kakomaa.

Hii sio soka ambayo umapaswa kukomaa hata kama bao moja unalotafuta katika mechi ya fainali kwenye dakika za majeruhi , haliwezi badili matokeo pale mpinzani wako anapokuwa na anaongoza kwa magoli mengi.
Kwa hili inabidi nyalandu ajitathimini mapema kisha ajiondoe mwenyewe amuachie lisu, hatutaki sababu maana hamkawii kusema mbowe na genge lake wamenifanyia zengwe
 
Shambaboy jogoli

Senior Member
Apr 7, 2020
114
225
Mpaka muda huu, nashindwa kuwaelewa Nyalandu na wenzake kwani nyakati zinambeba Lissu kwa asilimia 100.

Kwa hali ilivyo, ingekuwa ni katika nchi za wenzetu,mfano US, mtu kama Nyalandu naamini angetangaza kujitoa na kumuunga mkono Lissu bila kusubiri kupigwa kura na wajumbe.

Anyway, wacha tusubiri lakini huku ni kushindwa tu kusoma alama za nyakati kwa kisingizio cha demokrasia, demokrasia ambayo haimpi nafasi yeye na wenzake.

Hata hivyo,hii itakuwa ni fursa ya Lissu kuonyesha kukubalika kwake ndani ya chama kulinganisha na wagombea wenzake.

Wacha tusubiri labda kuna wanaopanga kujitoa siku ya kupiga kura kupitisha mgombea na kumuunga mkono Lissu maana siasa ndio zilivyo.
Nakwambia Lisu kwa Magu anakanyagwa asbh kweupeee! Afadhari kidogo Member, yaani Lisu hapati hata asilimia 2 ya kura, take it from me!
 
Baba Swalehe

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
16,405
2,000
nyalandu He is a spy

nalijua hilo muda mrefu

mwenzangu yeyote aliyesoma chuo cha.... nchini Us Anajua nachoongea
 
Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
2,319
2,000
Ajabu yenyewe mleta mada siku chache zijazo tutakuona unaponda upande wa pili wamechapisha form moja ya uraisi, wakati kwako unalilia kitu unachopinga upande wa pili kifanyike.

Kuna wakati unajiuliza hivi wafuasi wa CDM wanajua wanapigania nini zaidi ya kuitoa CCM.

Ndio kama siasa za M.E; Saddam hafai, Gaddafi hafai; sasa hivi asilimia kubwa ya wananchi wanajuta kutofikiria nini kifanyike baada ya hao watu kutolewa.

Ukishaanza kusema fulani asiwe na mshindani ina maana wewe mwenyewe uamini democratic values, siku mkishinda uchaguzi god knows yepi mengine mtazuia kama fikra zenyewe ndio hizo.
 
ChizzoDrama

JF-Expert Member
Sep 29, 2019
1,089
2,000
Membe mwenzake ameshaonyesha dalili za kumuunga mkono Lissu ila yeye kakomaa.

Hii sio soka ambayo umapaswa kukomaa hata kama bao moja unalotafuta katika mechi ya fainali kwenye dakika za majeruhi , haliwezi badili matokeo pale mpinzani wako anapokuwa na anaongoza kwa magoli mengi.
Hatutaki dalili tunataka kuona vitendo
 
ChizzoDrama

JF-Expert Member
Sep 29, 2019
1,089
2,000
Mbona mnalazimisha nyalandu ajitoe? Kwa nini msiseme Lisu ndo ajitoe? Kama mnahubiri demokrasia acheni waende mpaka mwisho, atakaeshinda ndio wajumbe watakuwa wamechagua.

Hii ya kusema mara nyalandu ana pesa mara Lisu ni maarufu ni kutaguta kumnyima nyalandu haki yake huko chadema.
Yanapowakuta manaaza kuweweseka, acheni kila mtu apime upepo wake mwenyewe.
Wanahubiri DEMOGHASIA
 
Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
35,542
2,000
Mpaka muda huu, nashindwa kuwaelewa Nyalandu na wenzake kwani nyakati zinambeba Lissu kwa asilimia 100.

Kwa hali ilivyo, ingekuwa ni katika nchi za wenzetu,mfano US, mtu kama Nyalandu naamini angetangaza kujitoa na kumuunga mkono Lissu bila kusubiri kupigwa kura na wajumbe.

Anyway, wacha tusubiri lakini huku ni kushindwa tu kusoma alama za nyakati kwa kisingizio cha demokrasia, demokrasia ambayo haimpi nafasi yeye na wenzake.

Hata hivyo,hii itakuwa ni fursa ya Lissu kuonyesha kukubalika kwake ndani ya chama kulinganisha na wagombea wenzake.

Wacha tusubiri labda kuna wanaopanga kujitoa siku ya kupiga kura kupitisha mgombea na kumuunga mkono Lissu maana siasa ndio zilivyo.
Mda wa kujitoa bado,lazima ujue timing,,lisu akifungwa je,inakuaje?
 
Siwamilele

Senior Member
Oct 22, 2019
117
250
Hapa sikubaliani na wewe mkuu!
Ikiwa mnalalamikia m/kiti wa ccm kujiandalia fomu 1 tu kwa kuogopa kushindanishwa na wenzake ndani ya chama na hivyo kukanyaga demokrasia ndani ya chama chake + udikteta. Vipi na ninyi mnatamani kufanya yale yale?
Mnaogopa nini?
Mnahubiri demokrasia gani?

Kama unasema ni nyakati za Lissu, why uogope?
Binafsi najua pia kwamba Lissu ni mtu sahihi kabisa kumkabili JPM na anakubalika na watu wengi si tu Chadema, bali hata huko ccm pia.
Nstumaini atashinda, ila napendekeza ashinde kwa kupigiwa kura. Amini tu kwamba Nyaradu hatotoboa mbele ya Lissu, usitishwe na ushindi wake wa awali mkuu.
 
Omulasil

JF-Expert Member
May 5, 2015
3,062
2,000
Mkuu hii ya kufukuzwa ubunge inamuondolea sifa ya kugombea?, Kuna sheria inasema hivyo!?
Hiyo haimuondolei. Ila kuna hii kesi ya Mtuhumiwa wa Uhaini, bado haijathibitika wala hajashunda au kushindwa.
Akishindwa inabidi afungwe itakywaje? Au akishinda ana kuwa huru(jambo jema)

Itakuwa mgombea ni mtuhumiwa wa uhaini. Hapa amepoteza sifa( Mtego huu uliwekwa)
 
Fahari

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
834
500
Mpaka muda huu, nashindwa kuwaelewa Nyalandu na wenzake kwani nyakati zinambeba Lissu kwa asilimia 100.

Kwa hali ilivyo, ingekuwa ni katika nchi za wenzetu,mfano US, mtu kama Nyalandu naamini angetangaza kujitoa na kumuunga mkono Lissu bila kusubiri kupigwa kura na wajumbe.

Anyway, wacha tusubiri lakini huku ni kushindwa tu kusoma alama za nyakati kwa kisingizio cha demokrasia, demokrasia ambayo haimpi nafasi yeye na wenzake.

Hata hivyo,hii itakuwa ni fursa ya Lissu kuonyesha kukubalika kwake ndani ya chama kulinganisha na wagombea wenzake.

Wacha tusubiri labda kuna wanaopanga kujitoa siku ya kupiga kura kupitisha mgombea na kumuunga mkono Lissu maana siasa ndio zilivyo.
What if anapitishwa harafu anawekewa mapingamizi na NEC wanamuondoa kwenye kinyang'anyiro? Maana mda huo hakutakuwa na fursa ya kum replace.Huoni itakuwa ni hasara kubwa mno? Kama akikatwa plan B ikoje?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom