Uchaguzi 2020 Ingekuwa katika Nchi za wenzetu, Nyalandu na wenzake wangejitoa na kumuachia Lissu

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
38,714
2,000
Mpaka muda huu, nashindwa kuwaelewa Nyalandu na wenzake kwani nyakati zinambeba Lissu kwa asilimia 100.

Kwa hali ilivyo, ingekuwa ni katika nchi za wenzetu,mfano US, mtu kama Nyalandu naamini angetangaza kujitoa na kumuunga mkono Lissu bila kusubiri kupigwa kura na wajumbe.

Anyway, wacha tusubiri lakini huku ni kushindwa tu kusoma alama za nyakati kwa kisingizio cha demokrasia, demokrasia ambayo haimpi nafasi yeye na wenzake.

Hata hivyo,hii itakuwa ni fursa ya Lissu kuonyesha kukubalika kwake ndani ya chama kulinganisha na wagombea wenzake.

Wacha tusubiri labda kuna wanaopanga kujitoa siku ya kupiga kura kupitisha mgombea na kumuunga mkono Lissu maana siasa ndio zilivyo.
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
38,714
2,000
Nyarando yule ni kimeo,
Membe mwenzake ameshaonyesha dalili za kumuunga mkono Lissu ila yeye kakomaa.

Hii sio soka ambayo umapaswa kukomaa hata kama bao moja unalotafuta katika mechi ya fainali kwenye dakika za majeruhi , haliwezi badili matokeo pale mpinzani wako anapokuwa na anaongoza kwa magoli mengi.
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
23,859
2,000
Nchi zingine hununua wagombea pinzani wajitoe mfano Ni hapo Kenya unaletewa mabox ya pesa na mgombea uraisi au mgombea ubunge anasema hi nafasi naitaka chukua haya mabilioni jitoe niachie

Nyalandu Ni mkristo mshika dini hanunuliki .Hizo nchi unazosema za nje ndicho hufanya Watu hawajitoi bila kulamba pesa ya uhakika

Hata ku form alliance Kama ile ya UKAWA pesa ya Lowasa ilibidi imwagwe Hadi kwa akina Lisu Baada ya kuipata wakampisha na kuimba Lowasa mabadiliko , mabadiliko Lowasa!!! Nyalandu hahongeki ana pesa za kufa mtu hizo porojo zako za nchi zingine
 

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
8,537
2,000
Mkuu kura ndiyo zitaonesha yupi anapendwa na kukubalika na wapiga kura wengi. Kura ndani ya chama chenye demokrasia zita akisi uhalisia wa yaliyo moyoni mwa wapiga kura 6.7M.
Hiki kipimo chako cha hisia siyo sahihi, muhimu kusiwe na udanganyifu au rushwa katika upigaji kura ndani ya chama chao.
 

Nazgur

JF-Expert Member
Apr 19, 2020
913
1,000
Mbona mnalazimisha nyalandu ajitoe? Kwa nini msiseme Lisu ndo ajitoe? Kama mnahubiri demokrasia acheni waende mpaka mwisho, atakaeshinda ndio wajumbe watakuwa wamechagua.

Hii ya kusema mara nyalandu ana pesa mara Lisu ni maarufu ni kutaguta kumnyima nyalandu haki yake huko chadema.
Yanapowakuta manaaza kuweweseka, acheni kila mtu apime upepo wake mwenyewe.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom