Ingekuwa enzi za Augustino Lyatonga Mrema,mauji ya kibiti yasingedhibitiwa?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,887
143,983
Ukikumbuka utendaji wa Augustino Lyatonga Mrema enzi zile akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, ndio utajua umuhimu wa waziri mwenye dhamana katika balaa hili la mauji linaloendelea huko mkoani Pwani na pia utajua ni kwanini Mwigulu Nchemba anapaswa kuachia ngazi.

Hivi sasa,licha ya yanayoendelea, Waziri na Naibu wake wote wako Bungeni unless wawe wameenda leo.

Nina hakika ingekuwa ni enzi za Mrema, leo hii yeye mwenyewe angekuwa ameshahamishia kambi huko kibiti pamoja na vigogo wa Jeshi la Polisi.

Mrema alikuwa na juhudi binafsi,alikuwa mbunifu na zaidi alkuwa anajituma katika kusimamia maagizo yake.

Mh.Mwigulu please do the needful.
 
mpiga kampeni unampa wizara nyeti wapi na wapi,lyatonga alikuwa mtu wa usalama ivyo alikuwa anajua wapi aanzie, sio hawa wengine bla blaaa kibao na woga wa uthubutu kwa kuogopa kutumbuliwa. Hii ni aibuuu
 
Alidhibiti ujambazi kwa kiasi kikubwa kwa kuanzisha sungusungu, alifanikisha ujenzi wa vituo vidogo vya polisi maeneo mbalimbali nchini, hakuwa waziri wa kusubiri amri kutoka juu - alikuwa anafanya initiative mwenyewe katika mambo mengi, alijaribu kwa kiasi kikubwa kuwabana mapapa wa madawa ya kulevya lakini kuna viongozi wa ngazi za juu walimuangusha...
Sorry,sikukulewa nilidhani ulikuwa unamtetea Mwigulu.

Sasa tuko pamoja.
 
Hivi watu waliwahi kujiuliza zile bunduki zilizokuwa zikiporwa katika vituo vya police zilienda?! Hawa watu wamefanya maandalizi ya muda mrefu na jeshi letu la ama police au Jw wafanye utafiti wa kina na si wa kick labda wanaweza kufanikiwa. Nguvu saana haitasaidia
 
Ni wazi ukiibuka ugaidi tutaangamia sana.
 
Mwigulu ni mbwatukaji wa majukwaani tu na mjuvi wa fitina za kuwachafua wapinzani lkn uongozi hawezi. Sasa kawa kimya kama kondoo wa kitoweo cha Eid
 
Ukikumbuka utendaji wa Augustino Lyatonga Mrema enzi zile akiwa waziri wa mambo ya ndani ndio utajua umuhimu wa waziri mwenye dhamana katika balaa hili la mauji linaloendelea huko mkoani Pwani na pia utajua ni kwanini Mwigulu Nchemba anapaswa kuachia ngazi.

Hivi sasa,licha ya yanayoendelea, Waziri na Naibu wake wote wako Bungeni unless wawe wameenda leo.

Nina hakika ingekuwa ni enzi za Mrema, leo hii yeye mwenyewe angekuwa ameshahamishia kambi huko kibiti pamoja na vigogo wa Jeshi la Polisi.

Mrema alikuwa na juhudi binafsi,alikuwa mbunifu na zaidi alkuwa anajituma katika kusimamia maagizo yake.

Mh.Mwigulj do the needful.
Nakala ya uzi huu imfikie technically popote alipo .
 
Ni wazi ukiibuka ugaidi tutaangamia sana.
Fuatilia nyuzi za Mwigulu humu Jf , utaelewa kwanini alifikiriwa kupewa wizara hii , nenda mbali kidogo fuatilia maisha yake na mwenendo wake kwenye awamu ya 4 , utaelewa kwamba kilichompa madaraka ni uhusiano wake mbaya na chadema .

Nisome zaidi ya hii mistari niliyoandika hapa .
 
Nyakti zimebadilika sana, maisha yamekuwa magumu mno, uonevu umekithiri, watu hawaogopi kabisa hata Lyatonga kwa leo angepata changamoto to, vilevile idara aliyopo anaweza kushauriana jambo na polisi.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom