....ingebakia adhabu ya kifo tu ingekuwa afadhali, kuliko na hii nyingine,.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

....ingebakia adhabu ya kifo tu ingekuwa afadhali, kuliko na hii nyingine,..

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ziroseventytwo, Dec 26, 2011.

 1. Ziroseventytwo

  Ziroseventytwo JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 3,544
  Likes Received: 1,537
  Trophy Points: 280
  Kila kosa au amri lina/ina adhabu yake,kwa mujibu wa sheria. Wakati Mungu akiumba dunia hakukuwa na sheria au amri kwa mujibu wa maandiko(bibilia). Amri ya kwanza kabisa duniani ni USILE TUNDA LA MTI WA KATIKATI, na ukila adhabu yake ilikuwa ni kifo..nanukuu hakika siku mkila tunda la mti ule wa ktkt hakika mtakufa!. Ndivyo alivyowaambia Adam na Hawa. Hawa alikuwa wa kwanza kula tunda, then akampa na Adam, mungu alipowatokea pale bustani, badala ya kuwapa ile adhabu ya kifo papo hapo, akawafukuza bustanini,..adhabu ya kifo ikabaki palepale, akaongeza na nyingi ambaya ni ngumu zaidi "UTAKULA KWA JASHO" ardhi imelaaniwa kwa ajili yetu! Kiukweli adhabu hii ni ngumu sana..bora tungebakiziwa adhabu hii ya kifo kuliko kula kwa jasho, ila pamaja na hayo God is good.
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Pamoja na hayo bado mnaendelea tu. . . .
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  nadhani angeacha ya kufa basi lazima ingekuwa balaa zaidi ndo maana kapunguza machungu kwa kukupatia hiyo ya jasho lako..
   
 4. Ziroseventytwo

  Ziroseventytwo JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 3,544
  Likes Received: 1,537
  Trophy Points: 280
  we dada we! Usikute unavuna usipolima, na kukusanya usipotawanya.! Mama, umewahi kulima kwa jembe la mkono wewe? Umewahi kulala umesimama wewe?
   
 5. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #5
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,633
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  ....napenda sana simulizi hizi hasa hili la adhabu ya kifo. Kwa uelewa wangu mdogo nikitumia mfano wa mbuga za wanyama....hebu jiulize tukiwaondoa simba wote,chui,fisi,na wanyama wote wanaokula nyama haitapita miaka 10 kabla ya maafa kutokea...yaani malisho ya swala,nyumbu n.k yataisha. Kwangu binadamu kufa sio adhabu ni kanuni ya maumbile,..maumbile yanaji-balance
   
Loading...