Ingalikuwa rahisi Watu wote wangepimwa siku moja na wale positive wakaji lockdown, gonjwa lingalikwisha siku 14 tu

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,952
4,326
Ingalikuwa rahisi, gonjwa hili la corona tungaliweza kulitokomeza (cut the transmission chain) kwa kupima watu wote nchini na duniani kwa siku moja kwa mtindo wa nyumba hadi nyumba. Na nyumba zitakazopatikana zina mtu positive zikawekwa lockdown au self isolation papo hapo kwa siku 14, tungalifanikiwa sana kulitokomeza gonjwa hili ndani ya siku 14 tu kwa kukata mnyororo wake wa usambazaji.

Jambo kama hilo si rahisi na haliwezekani. Kwa mfano gharama tu ya kipimo kimoja ni Tsh 120,000/. Watanzania tuko millioni 60. Hivyo gharama ya kipimo ni:
Shs 60,000,000 × 120,000 = Tsh 7,200,000,000,000/ = Trillion 7.2 Shs.

Hapo hujaweka gharama za logistics zingine za kufanya zoezi hilo nchi nzima ndani ya siku moja na mambo mengine mengi. Hizi ukizijumlisha ni zaidi ya bajeti yetu ya mwaka mmoja. Hata hizo nchi zilizoendelea haziwezi kumudu kitu kama hicho.

Hivyo mbinu hiyo haiwezekani. Mbinu nyingine effective ni ku lockdown watu wote kwa siku 14 kwa mara moja duniani kote. Yaani watu wote duniani kwa muda mmoja wakaji lockdown kwa siku 14. Watu wote hakuna cha exemption: uwe mtumishi wa afya, askari wa jeshi lo lote na kadhalika wote lockdown.

Kifedha mbinu hii inaweza kuwa rahisi ukilinganisha na mbinu ya kwanza lakini matokeo yake ni janga (disaster) kubwa zaidi kuliko hiyo ya corona. Watu wengi watakufa kwa magonjwa mengine na njaa, mifugo yote itakufa kwani wachungaji wake watakuwa lockdown, mazao yote ya kilimo yatakufa kwani wakulima wake watakuwa lockdown na kadhalika. Itakuwa balaa lisilokipimo.

Hivyo mbinu hizo zote ambazo ndizo madhubuti kuvunja mnyororo wa usambazaji wa mdudu huyu haziwezekani. Ndiyo maana kinachofanyika ni part messures tu ambazo zinawezekana kwenye nchi husika bila kusababisha madhara zaidi kwa binadamu na viumbe vingine. Tufuate wanachotushauri wataalamu wa nchi yetu na tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu!
 
Umejaribu ku-imagine ugumu wa hilo zoezi?
Ndiyo nimejaribu na ni wengi tu wamejaribu ku imagine uwezekano wa hizo ideal intervention methods.

Haziwezekani lakini ndizo zinazotuongoza kupata hizo half measures tunazotumia kutegemea na kile nchi inachoweza kumudu hususani 2 metres social distancing, everybody to wear masks, washing hands as frequently as possible, avoiding touching your face, ban crowding etc.
 
Things are very far from the ideal reality. Wengine kama Kenya wanafanya lockdown usiku tu, tena usiku wa manane hadi saa 11 asubuhi tena kwenye miji mikuu tu.

Hiki ndicho wameona wanakiweza. WHO iliwapa big up kubwa kwa kitendo hicho cha kishujaa na IMF ikawapa mamilioni ya dola za kimerikani.

Nchi zilizojaribu kufanya zaidi ya hapo hiki ndicho walichoambulia:

Countries around the world are reopening — here's our constantly updated list of how they're doing it and who remains under lockdown

Nchini kwetu chama machachari cha upinzani kiliweza ku lockdown wabunge wake 15 kwa siku 14. Kilichoambulia sote tunakifahamu kwa lockdown hizo zisizo na maana ye yote kukatisha mnyororo wa maambukizi nchini.
 
Back
Top Bottom