Infinix phones: Mnasemaje kuhusu hizi simu wataalam?

kombaME

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
2,115
2,809
Wakuu kwema,

Mimi sio mtaalamu kabisa wa hizi simu, ila kuanzia mwezi uliopita nilianza kutumia infinix hot 6 pro baada ya kushawishiwa na mshikaji, asee very wonderful, nimeifurahia sana hii simu, camera safi, haikwami kwami, chaji ndo mwisho wa matatizo kifupi iko poa sana..

Sasa nipo interested kutaka kujua kutoka kwa mnaozijua na kufuatilia simu, hii kampuni ya infinix mnaizungumziaje
 
Kama ipo sawa tumia tu mkuu ukiwasikiliza watu kila walisemalo hutofanikiwa ktk maisha yako. Kuna watu hujiingiza gharama kubwaaa kununua kitu kujionyesha au kwa kufuata mkumbo halafu matumizi yake muhimu kwa chombo chenyewe ni pengine 15% tu. Mfano mtu ananunua tv ya kisasa yenye wasifu mwingiii halafu anaishia kuangalia bongo muvi tu wakati kilichosababisha auziwe ghali ni huo wasifu ambao hautumii.
 
ni kweli , ila penye ukweli lazima watu waujue, izi chinese smartphones ni ovyo kabisa, wanatumia vifaa duni katika uundaji, ndio maana simu inakua ya bei rahisi na ya ovyo (worthless)

tekino(au izi infiniks) yenye 13mp inazidiwa na 5mp ya samsung

3gb ram ya infinix unazidiwa na 1gb ram ya samsung katika performance
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom