Indonesia: Mamia wahamishwa kutokana na hatari ya mlipuko wa volkano

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Mamlaka nchini Indonesia zimewahamisha mamia ya watu waliokuwa wakiishi karibu na mlima wenye hatari ya kulipuka kwa volcano baada ya dalili za mlipuko kuongezeka mapema wiki hii.

Zaidi ya watu 600, wengi wakiwa wazee, wanawake wajawazito na watoto, pamoja na wale wenye ulemavu wamelazimika kuwekwa katika makazi ya muda, kwa mujibu wa shirika la kukabiliana na majanga nchini humo, huku tahadhari zote muhimu za kujikinga na ugonjwa wa corona zikichukuliwa.

Shughuli za kuhamishwa zilienda sambamba na upimaji wa haraka wa maambukizi ya virusi vya corona, uvaaji wa barakoa pamoja kukaa umbali salama.

Shirika la Kijeolojia la Indonesia limeonya kuhusu hatari ya mlipuko wa volcano katika Mlima Merapi hapo siku ya Alhamisi kutokana na kuongezeka kwa shughuli za kivolkano katika mlima huo, huku likitahadharisha kuhusu hatari ya mlipuko wa lava ama gesi ya moto ambayo huweza kusafiri hadi umbali wa kilometa 5 kutoka katika mlima huo.

Mlima Merapi umeanza kuonesha mlipuko wa volcano tangu mwaka 1548, na mlipuko wa mwisho ulitokea mwaka 2010 ambapo zaidi ya watu 300 walifariki dunia.

Chanzo: Bloomberg
 
Back
Top Bottom