#COVID19 Indonesia kuipa Tanzania dawa za Uviko-19 za milioni 345

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Serikali za Tanzania na Indonesia zimekubaliana kushirikiana katika kuboresha huduma za afya kwa faida ya pande zote mbili.

Hayo yamebainika Machi 8, 2022 ambapo Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alikutana na Tri Yogo Jatmiko, Balozi wa Jamhuri ya Indonesia nchini Tanzania katika ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Katika mazungumzo hayo, Balozi huyo amemwambia Waziri Ummy kuwa Serikali ya Indonesia imeweka kipaumbele cha kushirikiana na Tanzania katika kuboresha huduma za tiba mtandao (telemedicine), kuimarisha uhusiano katika masuala ya dawa makampuni ya Indonesia yanayozalisha dawa pamoja na kuipatia Serikali msaada wa dawa za UVIKO-19 zenye thamani ya shilingi milioni 345.

Waziri Ummy aliiomba Serikali ya Indonesia kuleta wawekezaji watakaojenga viwanda vya dawa nchini pamoja kuangalia uwezekano wa Bohari ya Dawa (MSD) kuingia mikataba na viwanda vinavyozalisha Dawa nchini Indonesia.

Kwa upande wa kubadilishana uzoefu wa utaalamu na utaalamu bobezi wa tiba, Balozi huyo amesema Serikali yake iko tayari kuleta wataalamu nchini ili waweze kuwajengea uwezo wataalam hapa nchini kupitia mafunzo kwa vitendo katika Hospitali zinazotoa huduma za kibingwa katika magonjwa ya moyo na saratani na huduma za upandikizaji viungo.

Nae Waziri Ummy kwa niaba ya Serikali amemshukuru Balozi Jatmiko kwa kumtembelea pamoja na kuonesha nia ya kuanzisha ushirikiano katika Sekta ya afya na akamwambia kuwa Serikali iko tayari kutoa ushirikiano katika maeneo ambayo wamekusudia kuwekeza.

Waziri Ummy amemueleza Serikali ya Awamu ya sita iko katika utekelezaji wa mpango mkakati wa tano wa masuala ya afya ambapo lengo likiwa ni kuboresha na kusogeza huduma karibu na wananchi ikiwemo huduma za mama na mtoto, vipimo, masuala ya lishe, huduma za kibingwa, bima ya afya kwa wote n.k.

Chanzo: Wizara ya Afya

Ummy.jpg
 
View attachment 2144337
Hivi zile dawa za madagascar mlimaliza kuzifanyia majaribio?
 
Can't we Exchange that with Paracetamol ?

Indonesia ?, I would be more happier with Palm Oil from them and not COVID / Pharmaceutical Products
 
Nchi hii bado ina viongozi wapuuzi sana ugonjwa umeshajifia wao wanakazana kutulisha nidawa ya majaribio
 
Na hizo kinga zikifika kila Mtanzania anatakiwa kudungwa mara 50 ili ziishe safi sana.

... anaupiga mwingi 😁!.
 
Unaomba chanjo ya uviko huku pua ikiwa haina barakoa...😊😊
 
Back
Top Bottom