Individual citizens wa Zanzibar, wamenufaikaje na muungano mpaka sasa?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Individual citizens wa Zanzibar, wamenufaikaje na muungano mpaka sasa??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by analysti, Nov 14, 2011.

 1. analysti

  analysti JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 704
  Likes Received: 354
  Trophy Points: 80
  Hi thinkers!!
  Nimekuwa nikitafakari hili nsuala kwa muda mrefu sana, nikizingatia uzoefu wangu wa TZ Bara na Visiwani. Hakika maisha ya wazanzibar ni duni kupita kiasi, hali halisi ni kwamba, si tu wapo nyuma kiuchumi bali hata katika nyanja mbalimbali za kijamii. Ninajiuliza, hivi ni kweli kama kusingekuwa na muungano hali zao zingekuwa duni zaidi ya hapo walipo?? Huwa nakataa kuamini hivyo hata kidogo. Na sioni ni kwa sababu gani Zanzibar imekuwa so marginalised. Na siku zote nitawaunga mkono pale wanapotaka muungano uvunjwe, hii ni kwa sababu, they have benefited very little if not at all. Na kwakuwa kwa kipindi chote cha muungano hakijaonyesha msaada wowote kwa wa znzbr, basi ngoja wajaribu kutokuwa kwenye muungano kwa angalau miaka 40 hivi na halafu tuone kama kweli watashindwa kusurvive!!.

  Ndugu wana JF tuwe fair kwa hili, kwa mtu yeyote aliyefika zanzibar atakuwa ni shahidi wa jinsi wa zanzibar wanavyoishi maisha magumu, Ni kweli hata bara kuna maisha magumu, ila ile proportion ya watu walio kwenye umasikini uliokithiri ni kubwa mno znzbr, na hata ambao kwa kule wanaonekana wako better of, na pengine na wao wapo comfortable, ukiwalinganisha na huku, ni watu duni bado. Ni nini maana ya hii hali??? Na ni kwa nini iwe hivi kwa tanzania iliyo moja??

  Natambua uwepo wa mikoa kwa tz bara ambayo iko marginalised as well, hata hii ingekuwa na option ya kujitenga ingefanya hivyo, but kwa kuwa hakuna hiyo option wanaendelea na michakato mingine ya kujikwamua. likini kwa zanzibar, nchi ambayo ilikuwa independent kwa nini iendelee kuwa kwenye muungano ulioprove kutokuwa na faida kwao???
   
Loading...