India yafungia kwa muda akaunti za Twitter za wanaharakati wa mageuzi ya kilimo

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Mtandao wa kijamii wa Twitter umezifungia kwa muda akaunti za baadhi ya watu waliojihusisha na maandamano ya kutaka mabadiliko katika sekta ya kilimo, ikiwamo akaunti ya gazeti maarufu la Caravan linaloandika kuwatetea wakulima, mwanaharakati Hansraj Meena na mwigizaji Sushant Singh.



Hatua hiyo ya mtandao wa Twitter ya kuzifungia takriban akaunti 250 inatokana na ombi la kisheria lililopelekwa na Serikali kwa kigezo cha kuwa machapisho katika akaunti hizo yanahatarisha usalama na utangamano wa India, Waziri wa Habari na Teknolojia wa India aliuambia mtandao wa AFP.

Maelfu ya wakulima wamekuwa wakiandamana nchini India tangu mwezi Novemba, wakikusanyika katika mahema nje ya Mji Mkuu wa New Delhi wakitaka serikali ifanye mageuzi katika sekta ya kilimo. Maandamano hayo yaligeuka kuwa ya vurugu baada ya polisi kuingilia na kuwakamata baadhi ya waandamanaji akiwamo mwandishi wa gazeti la Caravan.

Kufuatia kufungiwa kwa akaunti hizo, watumiaji wa mtandao wa Twitter wameonesha kukasirishwa na hatua ya mtandao huo kuwafungia wanaharakati wanaopaza sauti kudai mageuzi, huku 'hashtag' #TwitterCensorship ikiongoza kwa siku ya Jumatatu. Mtandao huo ulifungia akaunti zaidi ya 100 na machapisho mengine 150 kwa kutumia 'hashtag' yenye utata, kwa mujibu wa mtandao wa Indian Express.

Mtandao huo wa kijamii umejitetea kuwa umechukua hatua hiyo kutokana na kupokea agizo lenye muhuri wa mahakama.

"Nchi nyingi zina sheria ambazo hutumika katika machapisho au akaunti za Twitter. Katika kuendelea kuboresha huduma zetu kwa watumiaji kila mahali, ikiwa tutapokea ombi rasmi kutoka kwa Mamlaka, tunalazimika kuzuia baadhi ya maudhui," taarifa ya mtandao huo ilieleza, ikiongeza kuwa inaheshimu uwazi katika kuhakikisha kunakuwa na uhuru wa kutoa maoni.

"Uwazi ni muhimu katika kulinda uhuru wa kutoa maoni, hivyo tuna sera ya kutoa taarifa kwa maudhui yaliyofungiwa. Baada ya kupokea ombi la kufungia maudhui, tutawajulisha wamiliki wa akaunti zilizofungiwa (labda ikiwa tutazuiwa kufanya hivyo kutokana na amri ya mahakama), ilisomeka taarifa hiyo.

Akaunti hizo zilirejeshwa saa kadhaa baadaye. Hii si mara ya kwanza kwa India kufungia mtandao wa Intaneti kwa watu wanaopinga serikali. Mwaka 2019, serikali ilizuia mtandao wa Intanet kwa miezi kadhaa katika jimbo la linalozozaniwa la Kashmir baada ya kutokea mgogoro wa kujitoa.

India inashikilia nafasi ya 142 kati ya nchi 180 katika orodha ya nchi zinazoheshimu uhuru wa kutoa maoni duniani.
 
Sasa hivi kimbilio la kwanza la serikali ni kuzima harakati mtandaoni
 
Back
Top Bottom