India: Watu 10 wafariki baada ya jengo la ghorofa tatu kuporomoka

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Bhiwandi.jpg
Takriban watu 10 wamepoteza maisha baada ya jengo la makazi ya watu lenye ghorofa tatu kuporomoka mapema leo asubuhi katika eneo la Bhiwandi lililopo katika viunga vya jiji la Mumbai, India.​
Zaidi ya watu 25 wanahofiwa kukwama chini ya vifusi vya jengo hilo, kwa mujibu wa Kitengo cha Taifa cha Dharura, ikiongeza kuwa wafanyakazi wa uokoaji wanaendelea na juhudi za kuwaokoa watu katika eneo hilo.​
Zaidi ya wafanyakazi 40 wa misaada ya dharura wapo atika eneo hilo wakiendelea na juhudi za uokoaji, huku watu wawili wakipatikana wakiwa hai kutoka chini ya vifusi vya jengo hilo.​

Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi ameonesha kusikitishwa na tukio hilo, akichapisha taarifa katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter, akisema kuwa msaada wote unaohitajika utatolewa kwa wale walioathirika, huku akiwaombea majeruhi kupona haraka.​

Jengo hilo lililoporomoka lilikwisha wekwa katika orodha ya majengo hatari na notisi ya wakazi kuondolewa kutoka katika jengo hilo ilikwisha kutolewa, kwa mujibu wa gazeti la Times of India, likimnukuu Pankaj Ashiya, Kamishna wa Manispaa ya Mji wa Bhiwandi-Nizampurya.​
Kuporomoka kwa majengo si jambo geni nchini India. Mwezi mmoja uliopita, takriban watu 13 walipoteza maisha wakati jengo la ghorofa tano lilipoporomoka katika eneo la Mahad, takriban maili 100 kusini mwa Mumbai. Mwaka 2017, takwimu za Taasisi ya Taifa ya Uhalifu nchini humo zilionesha kuwa zaidi ya watu 1,200 walipoteza maisha kutokana na matukio ya kuporomoka kwa majengo nchini humo.​
Chanzo: Al Jazeera.
 
Back
Top Bottom