India: Wakulima waandamana kudai mageuzi ya kilimo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Maelfu ya wakulima wamekuwa wakiandamana kudai mageuzi katika sekta ya kilimo wamepigana na kulazimisha kuvuka kizuizi cha polisi na gesi za kutoa machozi kuingia katika eneo la kihistoria la Delhi -Red Fort

Walikua wakiandamana kwa miguu na wengine wakiwa ndani ya matrekta wakiwa ni sehemu ya maandamano makubwa yaliyopangwa katika siku ya Jamuhuri ya India.

Waandamanaji wengi walikwepa njia zilizokuwa zimeafikiwa na makabiliano yakatokea baina yao na polis, mmoja wa waandamanaji alikufa.

Huduma za inaneti na simu zimezimwa katika baadhi ya maeneo ya Delhi huku vikosi vya usalama viking’ang’ana kurejesha hali ya utulivu.

Serikali bado haijatoa kauli yoyte juu ya ghasia, lakini ripoti zinasema wazziri wa mambo ya ndaniMinister Amit Shah alifanya mkutano na polisi wa Delhi kuhusu ghasia hizo.

Serikali inasema mageuzi yaliyoibua maandamano yatashugulikiwa na sekta ya kilimo, lakini wakulima wanasema watapoteza mapato.

Maelfu kwa maelfu ya wakulima wamekuwa katika mgomo tangu mwezi Novemba mwaka jana, wakidai sheria za kilimo zifanyiwe mabadiliko. Walikataa pendekezo la serikali la kuweka sheria wiki iliyopita.

1611667571688.png
 
Hata Tz twahitaji mabadiliko ya sera za kilimo nahisi tuko mbioni kuandamana🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom