Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 8,933
- 25,268
Hali ya taharuki imetokea katika mji wa Meerut baada ya kundi la nyani kumvamia mfanyakazi wa maabara aliyekuwa amebeba sampuli za damu za wagonjwa wa COVID-19.
Nyani hao walikimbia baada ya kuiba sampuli tatu na kuzitafuna wakiwa juu ya mti. Tukio hili lilirekodiwa na camera ikimuonyesha nyani huyo akitafuna sampuli hizo na baadhi ya sehemu ya sampuli hizo zikiwa zimezagaa chini ya mti. Wakazi wa mji huo wamesemekana kuwa na wasi wasi kwamba tukio hilo linaweza kueneza ugonjwa huo zaidi katika mji huo.
Inasemekana mfanyakazi huyo ameambiwa ajieleze kwa maandishi kwa nini alirekodi video hiyo baadala ya kuomba msaada.