India : Taharuki baada ya Nyani kuiba sampuli za damu za waonjwa wa COVID19 kuzitafuna na kukimbia

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,906
25,180
Screenshot from 2020-05-29 18-35-15.png

Hali ya taharuki imetokea katika mji wa Meerut baada ya kundi la nyani kumvamia mfanyakazi wa maabara aliyekuwa amebeba sampuli za damu za wagonjwa wa COVID-19.

Nyani hao walikimbia baada ya kuiba sampuli tatu na kuzitafuna wakiwa juu ya mti. Tukio hili lilirekodiwa na camera ikimuonyesha nyani huyo akitafuna sampuli hizo na baadhi ya sehemu ya sampuli hizo zikiwa zimezagaa chini ya mti. Wakazi wa mji huo wamesemekana kuwa na wasi wasi kwamba tukio hilo linaweza kueneza ugonjwa huo zaidi katika mji huo.

Inasemekana mfanyakazi huyo ameambiwa ajieleze kwa maandishi kwa nini alirekodi video hiyo baadala ya kuomba msaada.

Shida ya India ni hii kwamba ngedere wanezagaa mno hadi mijini na hawawachukulii hatua yeyote.
 
Sisi huku tulipima sambuli za Mbuzi na sasa ni zamu ya India kupima Sambuli za Nyani.
 
View attachment 1462764

Hali ya taharuki imetokea katika mji wa Meerut baada ya kundi la nyani kumvamia mfanyakazi wa maabara aliyekuwa amebeba sampuli za damu za wagonjwa wa COVID-19.

Nyani hao walikimbia baada ya kuiba sampuli tatu na kuzitafuna wakiwa juu ya mti. Tukio hili lilirekodiwa na camera ikimuonyesha nyani huyo akitafuna sampuli hizo na baadhi ya sehemu ya sampuli hizo zikiwa zimezagaa chini ya mti. Wakazi wa mji huo wamesemekana kuwa na wasi wasi kwamba tukio hilo linaweza kueneza ugonjwa huo zaidi katika mji huo.

Inasemekana mfanyakazi huyo ameambiwa ajieleze kwa maandishi kwa nini alirekodi video hiyo baadala ya kuomba msaada.

View attachment 1462767
Hao nyani watakuwa wametumwa na upinzani
 
Wanaabudu nyani sasa wamuuwe mungu wao
Kuna siku walikula futari ambayo watu walikuwa wanamalizia kusali msikitini ili wapige msosi. Yaani Nyani waliwa-time waislam. Walichokifanya hawakuwapiga wala kuwafukuza, walienda kwenye temple ambayo mungu wao ni nyani kuwapa taarifa. Waumini wa mungu nyani walifurahi sana kuona mungu wao wanakula. Walilipa gharama ya msosi wote.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom