India: Mwanafunzi aliyekuwa wa kwanza katika mtihani apelekwa jela

STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
13,075
17,237
Mwanafunzi mmoja ambaye alikuwa ameshika nafasi ya kwanza katika mtihani wake nchini India amehukumiwa kifungo jela baada ya kuruudia mtihani huohuo kwa mara ya pili na kushindwa kufaulu.

Mwanafunz huyo mwenye umri wa miaka 17 ambaye alikuwa wa kwanza katika mtihani huo katika jimbo la Bihar, alisema katika mahojiano kwamba somo alipendelo la sayansi ya siasa linahusu mapishi. Baada ya kanda hiyo kusambaa ,bi Rai alilazimika kukalia tena mtihani na alikamatwa aliposhindwa huku matokeo yake ya mtihani yakifutiliwa mbali.

Aliwasilishwa mahakamani siku ya Jumapili ambapo hakimu alimuhukumu kifungo jela hadi tarehe 8 mwezi Julai.

Uamuzi wa kumpeleka jela umekosolewa kwa kuwa ni mtoto na kwamba badala yake angepelekwa katika jela ya watoto.

Gazeti la Hindu lilimnukuu afisa mkuu wa polisi Manu Maharaj akisema kuwa bi Rai atalazimika kubaini kwamba yeye ni mtoto. Wakati huohuo agizo la kukamtwa limetolewa kwa wanafunzi wengine ambao walifanya vyema katika mtihani akiwemo Sauragh Shrestha ambaye alikuwa wa kwanza katika somo la sayansi lakini ambaye baadaye
alishindwa kusema kwamba H2O ni maji.

Chanzo: BBC
 
Hiyo ingekuja nchini kwetu hakiyanani watu wengi wangeumbuka maana jinsi walivyofaulu inatia mashaka.
 
Attachments

  • VID-20150508-WA0010.mp4
    2.5 MB · Views: 46
Saadam Hussein alikuwa Rais wa Kuwait nadhani Mh alikuwa sahihi kabisa.Ukisema alikosea sheria ya mtandao itachukua mkondo wake inabidi twende hvyo hivyo mpaka tutaelewana.
 
Hivi aliyesema Tanzania ni Muungano wa nchi mbili ambazo nai Tanganyika na Zimbabwe karudi tena Bungeni?
 
Yupo kama kawa,si unajua tena mtaji wa CCM kushinda ni Wananchi Mbumbumbu. Wewe fikiria huyo aliesema Tanzania ni Muungano wa Tanganyika na Zimbabwe alikuwa ni Waziri tena wa Elimu sasa hao waliompigia kura wana hali gani kielimu.
 
Back
Top Bottom