India: Mlipuko mpya wa Covid-19, UK. USA, zatangaza zuio la safari za India; Hapa kwetu wasafiri wahindi kama kawa

Taso

JF-Expert Member
Jun 12, 2010
2,197
2,000
V7O4DVDE2BMQ5EWZBIENM62IN4.jpg

NSG7JORLIZOVVNKWQKCIZYAYG4.jpg

UINGEREZA imeiweka India katika orodha nyekundu, red list, ya vikwazo vya safari. Rais wa Uingereza peke yao ndio watakaoruhusiwa kuingia kutoka India. Zuio hilo linaanza kesho Ijumaa. April 23, 2021.

Hii ni baada ya mfumuko mpya wa maambukizi na vifo vya COVID-19 nchini India unaoifanya nchi hiyo kuwa kiunga hatari cha ugonjwa huo duniani, new hotspot. Covid-19 ya India kwa sasa inasambazwa na kimelea kipya cha kutisha zaidi chenye mabadiliko mapya mawili vya vinasaba, double mutant.

Marekani nayo imewaasa raia wake kutokwenda India maana hali ni hatari hata kama wamepata chanjo.

Hapa kwetu Tanzania safari za popote ikiwemo India zinaendelea kama kawaida. Tunachofanya ni kupima jotoridi la wasafiri mara wafikapo, kitu ambacho kimeonekana hakiaminiki sehemu nyingi duniani hususan kwa wasafiri wa India. Nchi za Canada, Hong Kong, na nyinginezo zimelalamika kwamba asilimia kubwa ya wasafiri wanaofika kwenye airport zao hukutwa na maambukizi ya Covid-19 wanatokea India, na wanakuwa wamebeba nyaraka kutoka kwao zinazoonyesha hawana maambukizi hayo. Mashirika ya ndege ya India pia yameshutumiwa kwa kusafirisha watu walioathirika na Covid-19

Chanzo:
UK India Travel Advice
India Daily
Center for Disease Control
 
The Icebreaker

JF-Expert Member
Feb 11, 2018
7,581
2,000
Wahindi walikua na zile sikukuu zao hivi karibuni,

Unakuta umati unaingia kwenye mto kuoga na kufanya ibada,Serikali iliwataka kusitisha hizo ibada ila hawakusikia,

Sasa hivi maambukizi yameongezeka halafu hao hao raia wanarudi kuilaumu Serikali!
 
Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,578
2,000
Wahindi walikua na zile sikukuu zao hivi karibuni,

Unakuta umati unaingia kwenye mto kuoga na kufanya ibada,Serikali iliwataka kusitisha hizo ibada ila hawakusikia,

Sasa hivi maambukizi yameongezeka halafu hao hao raia wanarudi kuilaumu Serikali!
Serikali inalaumiwa?? Binadamu kazi SANA, watakuwa walikuwa na wao wanasema, tumtegemee Mungu, huku wanaoga!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
UHURU JR

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
11,488
2,000
Sisi tusiopima hatujui kiwango cha maambukizi kikoje hatujui mlipuko mpya wala wa zamani ukoje, sasa hapo tunaanzaje kuzuia hao wahindi kwa kigezo cha huo mlipuko mpya?
 
joseph1989

JF-Expert Member
May 4, 2014
7,296
2,000
India wana double mutation na triple mutation variants.Zote zinasambaa kwa speed na zina madhara makubwa,hiyo double inaathiri sana watoto na hiyo triple Inaweza kukuendesha hata kama umepata chanjo.

Huu ugonjwa kama series na hii double mutation wanadai ishafika UK.
 
mjombakim

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
976
1,000
India wana double mutation na triple mutation variants.Zote zinasambaa kwa speed na zina madhara makubwa,hiyo double inaathiri sana watoto na hiyo triple Inaweza kukuendesha hata kama umepata chanjo.

Huu ugonjwa kama series na hii double mutation wanadai ishafika UK.
duh apa kwetu hatuwezi kuwa na triple kweli
 
ielewemitaa

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
5,188
2,000
V7O4DVDE2BMQ5EWZBIENM62IN4.jpg

NSG7JORLIZOVVNKWQKCIZYAYG4.jpg

UINGEREZA imeiweka India katika orodha nyekundu, red list, ya vikwazo vya safari. Rais wa Uingereza peke yao ndio watakaoruhusiwa kuingia kutoka India. Zuio hilo linaanza kesho Ijumaa. April 23, 2021.

Hii ni baada ya mfumuko mpya wa maambukizi na vifo vya COVID-19 nchini India unaoifanya nchi hiyo kuwa kiunga hatari cha ugonjwa huo duniani, new hotspot. Covid-19 ya India kwa sasa inasambazwa na kimelea kipya cha kutisha zaidi chenye mabadiliko mapya mawili vya vinasaba, double mutant.

Marekani nayo imewaasa raia wake kutokwenda India maana hali ni hatari hata kama wamepata chanjo.

Hapa kwetu Tanzania safari za popote ikiwemo India zinaendelea kama kawaida. Tunachofanya ni kupima jotoridi la wasafiri mara wafikapo, kitu ambacho kimeonekana hakiaminiki sehemu nyingi duniani hususan kwa wasafiri wa India. Nchi za Canada, Hong Kong, na nyinginezo zimelalamika kwamba asilimia kubwa ya wasafiri wanaofika kwenye airport zao hukutwa na maambukizi ya Covid-19 wanatokea India, na wanakuwa wamebeba nyaraka kutoka kwao zinazoonyesha hawana maambukizi hayo. Mashirika ya ndege ya India pia yameshutumiwa kwa kusafirisha watu walioathirika na Covid-19

Chanzo:
UK India Travel Advice
India Daily
Center for Disease Control
Ije ije sisi tutaishi nayo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom