India: Kijana apoteza maisha akijaribu helikopta aliyounda

Msudu

JF-Expert Member
Aug 19, 2021
428
1,000
Kijana mmoja aitwae Sheikh_Ismail_Ibrahim, 24, amepoteza maisha wakati wa majaribio ya kurusha Helikopta yake aliyounda nyumbani.

Video iliyonasa Chopa hiyo inaonesha panga ndogo mkiani ling'oka na kugongana na panga kubwa juu na kwenda kugonga kichwa chake.

Kijana huyo alikimbiziwa hospitalini na marafiki zake waliokuwa wanashuhudia tukio lakini alifariki dunia muda mfupi baadae wakati zikifanyika juhudi za kuokoa maisha yake.

Sheikh Ismail Ibrahim aliypewa jina la utani la 'Yavatmal Rancho' kwa ubunifu wa kazi zake za chuma, alikuwa na matumaini ya kwenda kurusha helikopta hiyo siku ya Uhuru wa India mnamo 15 Agosti.

Kijana Sheikh alikuwa ametumia miaka miwili kutengeneza helikopta hiyo huko Yavatmal, katikati mwa India, akifanya majaribio ya chini nyumbani kwake kabla ya majaribio ya kupaa yaliyogharimu uhai wake.

'Munna Helicopter' ndiyo jina ambalo kijana huyo alikuwa na ndoto ya kuwa kampuni ya wazawa inayounda Helikopta nyepesi za bei nafuu nchini India.
View attachment 1898873
Kafa kishujaa aisee
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom