India: Kijana apoteza maisha akijaribu helikopta aliyounda

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,907
6,700
Kijana mmoja aitwae Sheikh_Ismail_Ibrahim, 24, amepoteza maisha wakati wa majaribio ya kurusha Helikopta yake aliyounda nyumbani.

Video iliyonasa Chopa hiyo inaonesha panga ndogo mkiani ling'oka na kugongana na panga kubwa juu na kwenda kugonga kichwa chake.

Kijana huyo alikimbiziwa hospitalini na marafiki zake waliokuwa wanashuhudia tukio lakini alifariki dunia muda mfupi baadae wakati zikifanyika juhudi za kuokoa maisha yake.

Sheikh Ismail Ibrahim aliypewa jina la utani la 'Yavatmal Rancho' kwa ubunifu wa kazi zake za chuma, alikuwa na matumaini ya kwenda kurusha helikopta hiyo siku ya Uhuru wa India mnamo 15 Agosti.

Kijana Sheikh alikuwa ametumia miaka miwili kutengeneza helikopta hiyo huko Yavatmal, katikati mwa India, akifanya majaribio ya chini nyumbani kwake kabla ya majaribio ya kupaa yaliyogharimu uhai wake.

'Munna Helicopter' ndiyo jina ambalo kijana huyo alikuwa na ndoto ya kuwa kampuni ya wazawa inayounda Helikopta nyepesi za bei nafuu nchini India.
FB_IMG_1629402650900.jpg
 
=

Kuna mwingine alikuwa na yake huko Sumbawanga. Kama kawaida yetu:

IMG_20210718_063455_991.jpg

Alipoelekezwa kuacha kuhatarisha maisha yake na watu wengine kama ilivyozoeleka walitokea wenye kuita husuda.

Haya mambo si ya maombezi wala ndoto wala kudra za Mola.

Ama kweli "he learnt it the very hard way!"

Apumzike kwa amani mja huyu wa Mola.
 
Kijana mmoja aitwae Sheikh_Ismail_Ibrahim, 24, amepoteza maisha wakati wa majaribio ya kurusha Helikopta yake aliyounda nyumbani.

Video iliyonasa Chopa hiyo inaonesha panga ndogo mkiani ling'oka na kugongana na panga kubwa juu na kwenda kugonga kichwa chake.

Kijana huyo alikimbiziwa hospitalini na marafiki zake waliokuwa wanashuhudia tukio lakini alifariki dunia muda mfupi baadae wakati zikifanyika juhudi za kuokoa maisha yake.

Sheikh Ismail Ibrahim aliypewa jina la utani la 'Yavatmal Rancho' kwa ubunifu wa kazi zake za chuma, alikuwa na matumaini ya kwenda kurusha helikopta hiyo siku ya Uhuru wa India mnamo 15 Agosti.

Kijana Sheikh alikuwa ametumia miaka miwili kutengeneza helikopta hiyo huko Yavatmal, katikati mwa India, akifanya majaribio ya chini nyumbani kwake kabla ya majaribio ya kupaa yaliyogharimu uhai wake.

'Munna Helicopter' ndiyo jina ambalo kijana huyo alikuwa na ndoto ya kuwa kampuni ya wazawa inayounda Helikopta nyepesi za bei nafuu nchini India.
View attachment 1898873
Good for him amefia anachokiamini. Why should someone waste time to invent the wheel?
 
Back
Top Bottom