India: Kijana alivyopoteza maisha kwa ajali wakati akifanyia majaribio helikopta aliyokuwa akiiunda

May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
6,162
8,820
Nakumbuka hata hapa nchini kuna taarifa kadhaa zinazoelezea juu ya uundwaji wa chombo hichi, na hata kumewahi kutoka lawama ni kwa nini hwapewi kibali cha kujaribu Vifaa vyao hivi.

Ingawa wanasema huwezi kujua ufanishi bila kujaribu lakini nadhani kuna mashine na mashine.

Hii imetokea India, kijana mmoja aliyekatisha masomo na kuamua kujikita kwenye kutekeleza ndoto yake ya siku nyingi ya kuunda Helikopta, amepoteza

 
Hata hizi Helikopta na Ndege zinazotumika sasa,kuna watu walikufa mpaka kufanikiwa leo hii kua na vyombo hivyo vya usafiri,

Ajali kazini ni jambo la kawaida,inaweza kua kuna makosa ya kiufundi yalifanyika ila dogo kajitahidi,

Rest In Peace Hero.
Hatumlaumu Marehemu na bado anabaki kwenye orodha ya wenye uthubutu.

Lakini kwa kuwa alichokuwa anakiunda tayari kilishawahi kuundwa tena na teknolojia imeshapiga sana hatua basi hakukuwa na tatizo kama angeshirikisha Mtaalamu mmoja wa eneo hilo.

Haswa kuhakiki hayo mapanga na huenda hata wangeng'amua mapema uwezekano wa kupata ajali.
 
Hatumlaumu Marehemu na bado anabaki kwenye orodha ya wenye uthubutu.

Lakini kwa kuwa alichokuwa anakiunda tayari kilishawahi kuundwa tena na teknolojia imehsapiga sana hatua basi hakukuwa na tatizo kama angeshirikisha Mtaalamu mmoja wa eneo hilo.

Haswa kuhakiki hayo mapanga na huenda wangeng'amua haraka uwezekano wa kupata ajali.
Mkuu,kwa habari ilivyoletwa,hakuna ushahidi wowote kua Kijana hakushirikisha wataalamu,

Pia unaweza kushirikisha wataalamu ila sometimes ajali haziepukiki,

Ukiangalia hiyo clip,utaona kabisa kua Lile panga kubwa limepiga zile panga ndogo za nyuma,

Na kwa mujibu wa hiyo clip,test ilisha fanyika kabla ya ajali hiyo,

It's better to die while doing something than living for nothing.
 
Ajengewe sanamu akiwa ndani ya chopa yake. India imeendelea kiteknolojia. Mqmlaka husika zilipaswa kumsaidia na kupima mitambo yake kabla hajafanya majaribio ya kuipeleka angani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom