India: Askari Polisi washambuliana kwa risasi wenyewe kwa wenyewe

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,480
9,241
ASKARI Polisi saba wamefariki dunia huku 50 wakijeruhiwa nchini India, katika mashambuliano ya risasi ya wenyewe kwa wenyewe , yaliyoibuka Jumatatu, tarehe 26 Julai 2021, kwenye Mji wa Vairengte nchini humo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Tukio hilo lisilo la kawaida limetokea baada ya Polisi katika majimbo ya Assam na Mizoram, yaliyoko Kaskazini Mashariki mwa India, kurushiana risasi, hatua iliyotokana na mgogoro wa muda mrefu wa mipaka ya majimbo hayo.

Mgogoro huo ulishika kasi mwezi mmoja uliopita, baada ya Polisi wa Jimbo la Mizoram, kudai kwamba Polisi wa Jimbo la Assam, wamejiongezea eneo la mpaka.

Waziri Mkuu wa Jimbo la Assam, Himanta Biswa Sarma, ameshutumu mapigano hayo akisema Polisi wa Mizoram hawakupaswa kutumia nguvu, katika kukabiliana na mgogoro huo.

MwanahalisiOnline
 
India ndio maana wana katiba kubwa kuliko zote duniani. Wana mchanganyiko wa hali ya juu sana na ubaya jamii zao zina PhD ya ubaguzi.
Hayo majimbo yao yanajiendesha yenyewe (yaani hadi kumiliki taasisi za ulinzi) kama Ethiopia?
 
India ni kama nchi iliyokusanywa kama Ethiopia hizo jamii hazikuwa na mahusiano ila wanafanana tu. Sasa ukiunganisha jamii za hivo alafu kukawa na ujinga, umaskini na ubaguzi mwingi lazima itokee kutokubaliana kama hivi ndio maana hawawezi acha kumiliki polisi wake kila jimbo. Ila wana jeshi moja la ulinzi
 
ASKARI Polisi saba wamefariki dunia huku 50 wakijeruhiwa nchini India, katika mashambuliano ya risasi ya wenyewe kwa wenyewe , yaliyoibuka Jumatatu, tarehe 26 Julai 2021, kwenye Mji wa Vairengte nchini humo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Tukio hilo lisilo la kawaida limetokea baada ya Polisi katika majimbo ya Assam na Mizoram, yaliyoko Kaskazini Mashariki mwa India, kurushiana risasi, hatua iliyotokana na mgogoro wa muda mrefu wa mipaka ya majimbo hayo.

Mgogoro huo ulishika kasi mwezi mmoja uliopita, baada ya Polisi wa Jimbo la Mizoram, kudai kwamba Polisi wa Jimbo la Assam, wamejiongezea eneo la mpaka.

Waziri Mkuu wa Jimbo la Assam, Himanta Biswa Sarma, ameshutumu mapigano hayo akisema Polisi wa Mizoram hawakupaswa kutumia nguvu, katika kukabiliana na mgogoro huo.

MwanahalisiOnline
ndio mambo ya majimbo hayo ambayo cdm wanayataka, ati jimbo fulani mtu anamiliki hadi polisi wake wa jimbo, na kuna mipaka ya kijimbo ambayo watu wanagombania kwenye nchi moja. jifunzeni basi cdm.
 
Hao jamaa migogoro yao ni sababu ya ubaguzi wa kijamii, kitabaka na kiasili miongoni mwao na sio serikali ya majimbo.

Toleeni mfano na nchi zingine kama Marekani, Urusi, Canada, China maana hata hao wana utawala wa majimbo, msiangalie upande mmoja tu kwa nchi zenye migogoro.
 
Huku kwetu hawana madhara hua anajiua mwenyewe tena kwa wivu wa mapenzi tuu
 
Wahindi hawajawahi kua serious hata siku moja hapa duniani.

Jamii ya kindezi sana yenye maamuzi ya kipuuzi.
Rejea ile ishu ya jeshi la India kutungua ndege yake yanyewe.
 
ndio mambo ya majimbo hayo ambayo cdm wanayataka, ati jimbo fulani mtu anamiliki hadi polisi wake wa jimbo, na kuna mipaka ya kijimbo ambayo watu wanagombania kwenye nchi moja. jifunzeni basi cdm.
Mbona Marekani wana majimbo mkuu na hakuna shida. Japo siungi mkono serikali ya majimbo ila kuna nchi zina serikali ya majimbo na zinaenda fresh tu
 
Wahindi hawajawahi kua serious hata siku moja hapa duniani.

Jamii ya kindezi sana yenye maamuzi ya kipuuzi.
Rejea ile ishu ya jeshi la India kutungua ndege yake yanyewe.
Lini hiyo mkuu walipotungua ndege yao wenyewe?
 
Hao jamaa migogoro yao ni sababu ya ubaguzi wa kijamii, kitabaka na kiasili miongoni mwao na sio serikali ya majimbo.

Toleeni mfano na nchi zingine kama Marekani, Urusi, Canada, China maana hata hao wana utawala wa majimbo, msiangalie upande mmoja tu kwa nchi zenye migogoro.

Mataga hawanaga akili ya kujua hayo mzee.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom