Tulipokuwa tunadai uhuru hatukudai uhuru ili tujengewe reli, kama ni reli wajerumani walijenga, hatukudai uhuru ili tujengewe shule kama ni shule wakoloni na wamishonari walijenga, hatukudai uhuru ili tujengewe viwanja vya ndege, hatukudai wakoloni waondoke ili tujenge hospitali.
Tulichokuwa tunadai ni Uhuru wa kujiamulia mambo yetu wenyewe bila kuingilia na mkoloni, uhuru wa kukusanyika, uhuru wa kujieleza bila kupangiwa cha kusema, tulidai uhuru wa kiuchumi kila mtu awe huru kufanya biashara, kulima, kuuza na kununua, uhuru wa kupanga na kuchagua viongozi wetu wenyewe.
Serikali imeshindwa kusimamia uhuru kamili (total independence) tuliokuwa tunadai, uhuru tulioupata tarehe 9 December 1961 umeporwa na dola, serikali imekuwa kama ndiyo mkoloni mpya, inawapangia watu cha kusema, imeua uhuru wa vyombo vya habari, imezuia vyama vya siasa kukutana, inaingilia biashara za wananchi wake, inawapangia wakulima bei na kuwalazimsha wauze wapi, haki za binadamu zinakiukwa na vyombo yenyewe vya dola.
Haya yanayofanywa na dola dhidi ya raia wake yanaharibu kabisa maana halisi ya Uhuru tuliodai na kuupata tarehe 9 December 1961. Kuna wengine wanafikia hatua wanasema 'Heri ya mkoloni mweupe kuliko mkoloni mweusi'.
Nawatakia sikukuu njema tunapoadhimisha Uhuru wa bendera.