Asante sana kwa hii.Jipatie Incubator za kisasa za sola na umeme za mayai 32-120
Full automatic, inageuza yenye mayai na pia ina ultrasonic Humidifier kwa ajili ya kuongeza unyevu, zinatumia solar, betri na pia umeme wa kawaida.
Bei zetu kwa sasa ni kama ifuatavyo:
incubator ya mayai 32A ni 240,000
incubator ya mayai 48 ni 350,000
incubator ya mayai 56 ni 420,000
incubator ya mayai 96 ni 490,000
incubator ya mayai 112 ni 530,000
incubator ya mayai 120 ni 550,000
zote ni full automatic na zinatumia umeme+solar/betri
View attachment 997426View attachment 997427View attachment 997428View attachment 997429
Piga/whatsapp/sms 0755571604 au 0718106434 na 0783095169 .
Tupo karibu na mwanachi relini Tabata. Popote ulipo tutakufikia.
Kuhusu matumizi ya sola inategemea unataka kuitumia kwa masaa mangapi na sola, kama ni kwa masaa 6 utahitaji solar panel 1 ya 100W na betri 1 ya 200Ah 12V na kama ni masaa 24 utahitaji solar panel 2 za 200w na betri 3 za 200Ah 12v.(incubator inatumia 160W kwa saa)Asante sana kwa hii.
Solar kuanzia watts ngapi inaweza kuendesha hiyo ya mayai 120 mkuu?
Pia, kama una incubator ya mayai 120, je ni lazima yatimie yote ndio uwashe incubator?
Asante
Nahitaji mpaka.mayai yaanguliwe.Kuhusu matumizi ya sola inategemea unataka kuitumia kwa masaa mangapi na sola, kama ni kwa masaa 6 utahitaji solar panel 1 ya 100W na betri 1 ya 200Ah 12V na kama ni masaa 24 utahitaji solar panel 2 za 200w na betri 3 za 200Ah 12v.(incubator inatumia 160W kwa saa)
Sio lazima ujaze mayai yote 120 ndio uiwashe hata ukiiwasha bila mayai hakiaribiki kitu zaidi ya umeme kupotea basi.
Naomba sifa za hii mashine mkuuView attachment 966351 sasa ipo dukani. Incubator mpya ya kisasa kabisa kwa sh 550,000. Full automatic. Vifaranga kufia kwenye mayai sasa ni basi.
Kulingana na utafiti uliofanywa, matatizo ya uzalishaji wa kuku ambayo wafugaji wa kuku wanakabilina nayo kwa kutumia mashine za kutotolesha vifaranga na huchangiwa na mambo yafuatayo:
1. Wafugaji hawafuati maelekezo ya kutumia incubator (mashine ya kutotolesha vifaranga).
2. Wafugaji hawajaribu (test)kwanza utendaji wa Incubator tupu, ili kupata uzoefu wa kurekebisha joto na unyevu, vitu/hali ambavyo ni muhimu sana kwa ufanyaji kazi sahihi wa Incubator.Kabla ya kuweka mayai yako katika Incubator, unapaswa kuiwasha kwa angalau wiki moja ili kuweza kuelewa jinsi inavyofanya kazi.
3. Wafugaji husahau kujaza maji kweye beseni (basin) la incubator hivyo husababisha mayai kukauka na kutokutotolewa.
4. Wafugaji hushindwa kuchagua mayai bora na yaliyorutubishwa ya kuweka kwenye incubator kwa kuyaangalia (scanning) kwa kutumia tochi ama egg candle.
5. Wafugaji kusahau kugeuzageuza mayai mara kwa mara ikiwa incubator zao hazina mfumo wa automatic wa kugeuza mayai; hii husababisha mayai kukaangwa (frying).Matokeo ya haya husababisha wafugaji hupata hasara, kuvunjika moyo, kukata tamaa na kuishia kulalamika kuhusu ubora wa incubator.
Kimsingi incubator yeyote mfugaji atakayochagua, mafanikio ya kutotolewa mayai yote, kwanza kunategemea juu ya ubora na urutubishwaji (fertility) wa mayai yanayokwenda kutotoleshwa, na pili, juu ya uangalifu na usimamizi wa Incubator. Jinsi utakavyoindesha vizuri ndivyo utakavyopata mafanikio zaidi. Umewekeza au unapanga kuwekeza fedha zako, basi unapaswa kuwa mweledi (professional) vinginevyo utapoteza fedha zako pamoja na mayai. Ufanisi wa matumizi bora ya Incubator ndogo unapatikana pale ambapo 80% hadi 90% ya mayai yanapofanikiwa kutotoleshwa vizuri.
Hizi ni baadhi ya dondoo tutakazo kuwa tunapeana juu namna ya kupata matokeo bora kwa incubator yako.
Pia tunauza incubator bora na za uhakika kwa bei nafuu. Incubator zetu ni mpya, (full automatic)zinatumia kompyuta ndogo kudhibiti kiasi cha joto na unyevu, zinageuza-geuza mayai zenyewe, zina feni 2 za kusambaza kiasi sawa cha joto na unyevu kwenye mayai. Mashine zetu zinatumia kiasi kidogo cha umeme, pia zinaweza kuhifadhi joto na unyevu kwa hadi ya masaa 5 mara baada ya kukatika umeme hivyo kukupa nafasi ya kuunganisha generator bila mayai yako kuathirika kwa kukatika umeme.Tuwasiliane kwenye 0783 095 169 au 0755 571604 ikiwa utahitaji incubators zetu.
Nawatakia mafanikio kwenye miradi yenu ya ufugaji
Kuhusu suala la matumizi ya umeme niliwahi kuliandikia kwenye post za mwanzoni… shida ni namna ya kutafsiri vipimo vya umeme kuja kwenye uhalisia.Go direct to the point kuwa unauza incubator badala ya kuweka mwishoni kabisa.
Alafu kuna kitu muhimu kabisa hujasema au kwa sababu wewe ni muuzaji.
Kuna watu wanajiita mafundi wa kutengeneza incubator lakini wamevamia fani.
Niliwahi kununua incubator ya mayai 700++ nilikoma ndani ya mwezi mmoja nilijikuta nalipa umeme laki 2 na nusu.
Nikaja kugundua baadaye tatizo lipo kwenye aina ya incubators hizi tunazotengenezewa watengenezaji wengine wa incubators ni feki balaa.
Kuhusu suala la matumizi ya umeme niliwahi kuliandikia kwenye post za mwanzoni… shida ni namna ya kutafsiri vipimo vya umeme kuja kwenye uhalisia.
Kwa mfano mashine ya mayai 1056 inayotumia umeme wa 220-240V na Power consumption ya 200W.(zipo pia zinazotumia 300W, 400W na zaidi)
Kwa maana hiyo kwa masaa 24 inatumia unit 4.8 i.e. (200x24/1000= 4.8kWh) za umeme na kwa siku 21 za utotoleshwaji wa mayai itatumia umeme wa units: 4.8x21=100.8 ambazo ukizizidisha na bei ya unit moja say 310Tshs.(weka bei ya sasa kama kwa tarrif uliyopo)
Hivyo kwa mwezi utatumia umeme wa 31,250Tshs.
Kwa hiyo mwenye mashine ya 1056 ila ya 400W atajikuta anatumia umeme mara mbili ya mtu mwenye mashine ya mayai 1056 ya 200W.
So pole sana kwa yaliyokukuta mkuu.
Kiwango cha joto na unyevu kwa hasa siku ya 18 hadi 21 ni muhimu sana ili vifaranga waweze kuanguliwa vizuri. Aidha kiwango cha joto kinapozidi nyuzi 37.5C na kiasi cha unyevu kuwa chini ya 68% husababisha pia kiasi cha majimaji yaliyopo ndani ya yai kupotea na hivyo hufanya kifaranga kukauka na kujishika kwenye ganda la yai hivyo kushindwa kutoka.Habari, nini kinachosababisha vifaranga wafie katika mayai?. Yaani siku zinakuwa zimefika wengine wanatotoreka wengine wanafia mayayini
Hili Jambo limenitokea mpk nikakata tamaa Ila baada ya kusoma hii comment, nimepata nguvu zaidiFanya 'egg candling' (kumulika mayai na tochi) angalau mara tatu ili kufuatilia mchakato wa utotoleshwaji wa mayai.
Hii huwezesha kujua mayai yaliyorutubishwa na yasiyorutubishwa, mayai ambayo mbegu ilikufa ndani ya wiki 1 baada ya kuwekwa kwenye mashine na mayai halisi unayotegemea kupata vifaranga.
Ikiwa pia mayai hayakutoa vifaranga usiyatupe bila kuchunguza tatizo lilikuwa wapi. Mfano virafanga wanaweza kufika kwenye mayai kabla ya kuanguliwa kutokana na aidha kiwango kidogo sana cha unyevu au kiwango kikubwa cha joto. Hivyo itakusaidia kujua nini cha kuboreshwa wakati ujao.
Kwenye ujasiriamali kuna kijifunza wakati wote, usikate tamaa kwa kushindwa mara moja tu. Jua chanzo cha tatizo liko wapi na rekebisha usonge mbele.
Nakutakia mafanikio tele kwenye ujasiriamali wako.View attachment 1223643