Incubator ni nini? Inatumikaje ? na ni kwa kiasi gani itaniongezea uzalishaji wa kuku wa mayai?

Aug 24, 2021
27
16
Nini maana ya Incubator ya mayai? Eggs incubator?
Ni jinsi gani ya kuitumia Incubator kuyapa joto mayai?
Ni kitu gani nifanye kabla ya kuweka mayai ndani ya incubator?
Nini kitatokea nisipogeuza mayai ndai ya incubator mara kwa mara?
Je kuna incubator ambazo zinageuza mayai zenyewe?
Nitajuaje kifaranga kimekufa ndani ya yai?

Ni kwa mda gani mayai yanaweza kukaa ndani ya incubator bila kuwa na umeme?

Nini maana ya Incubator ya mayai? Eggs incubator.​

Ni kifaa chenye feni na heater. Ambayo inaendelea kuyapa mayai joto linalo stahili kwa kipindi chote cha siku 21. kama ni mayai ya kuku. Au kwa maneno mengine ni kifaa ambacho. Kinayapa mayai ya ndege joto linalohitajika hadi kipindi yanapoanguliwa. Kifaa hiki kina dhibiti joto na unyevu na kuweka joto katika hali kamili inayofaa

Ni jinsi gani ya kuitumia Incubator kuyapa joto mayai?​

Kitendo cha kuitumia incubator kinapita kwenye hatua kuu nne.

1. Ku seti incubator yako.​

· Kiwango cha joto.​

  • Hii inahusisha kuseti joto la incubator lisizidi au kupungua 99.5 degree. Na kwa kuongeza degree ata moja au kupunguza itasababisha kuharibika kwa kiinitete cha yai.

· Unyevu​

Asilimia 40 hadi 50 ya unyevu ndani ya incubator yako inatakiwa kuzingatiwa. kwa kipindi cha siku 18 za kwanza. Na asilimia 65 adi 75 ya unyevu inahitajika. kwa siku za mwisho kabla ya kuanguliwa kwa mayai. Nikimaanisha kama ni mayai ya kuku ni siku 21-18=3 za mwishoni.

· Uingizaji wa hewa.​

Makaka ya yai huwa yana hitaji kuingiza kiasi flani cha hewa ili. Kifaranga anavoanza kutengenezwa apate hewa safi. Kwahio incubator inatakiwa kuweza kufanya mzunguko mzuri wa hewa. Kwa kuingiza hewa ya oxygen na kutoa hewa ya Cabondioxide.

2. Kutafuta mayai yenye rutuba.​

Kama una mitetea ya kutosha wenye majogoo wazuri. Mayai utakayoyapata yatakua moja kwa moja ni mayai yenye rutuba. Mayai yenye asimia kubwa ya kuanguliwa. Yanahitajika kushikwa kwa umakini na usafi wa mikono. Bila hivo utajikuta unaaribu kiinitete cha yai.
  • 3. Incubate​

    Kitendo cha ku incubate ndio cha kuyaweka mayai kwenye incubator. Na hatua ya kwanza kabla haujayaweka ndani ya incubator. Ni kuchora “X” kwenye upande mmoja wa yai na “O”.kwenye upande mwingine wa yai. Ili kujua ni mayai gani yameshageuzwa yakiwa ndani ya incubator.

    Pia hakikisha mayai yako hayata kaa ndani ya siku nzima bila kuyageuza mara 3 kwa siku. Ukiwa na mfululizo mzuri wa kugeuza mayai yako pia ni vizuri. Na ukiweza kuongeza mda wa kuyageuza mayai ata hadi mara 7 kwa siku.

    Ili mayai yasikae yakiangalia upande mmoja kwa mda mrefu. Itakua ni vizuri pia. Maana dhumuni ni kubadilisha mwelekeo wa kiinitete. Mara nyingi iwezekanavyo. Endelea kuyageuza mayai angalau kwa siku 18. Lakini uyaache yenyewe kwa siku chache zilizobaki.
  • 4. Mayai kutotolewa​

    • Kwa siku za mwisho. Utaanza kuona mayai yakijigusa gusa. Kutokana na kijusi cha kuku. Kuanza kuwa hai. Kifaranga kitatoboa kitobo kidogo kwenye ukuta wa yai. Ili kianze kupata hewa.
    • Kwa kawaida inatakiwa kifaranga apumzike kwa masaa 6 hadi masaa 12. Kwa mda wote ambao mapafu yake yanaendelea kukuwa. Epuka kutaka kujaribu kumsaidia kifaranga kutoka nje ya yai. Maana ni rahisi sana kumsababishia majeraha.
    • Na wakati kifaranga yupo huru kutoka ndani ya yai. Muachie kwa mda flani akauke kwa joto. lililopo kwanza ndani ya incubator. Kabla haujampeleka sehem nyingine na kuanza kumfuga.
    • Ni kitu gani nifanye kabla ya kuweka mayai ndani ya incubator?
    • Weka mayai yako katika joto la kawaida la chumba(room temperature). Kwa mda usiopungua masaa kumi na mbili. Kabla ya kuanza kuyaweka mayai yako ndani ya incubator.
    • Anzisha incubator yako bila kua na mayai yoyote. Kwa masaa 24 hai 48. Ili kufatilia hali nzima ya unyevu na joto lililopo ndani ya incubator.

Nini kitatokea nisipogeuza mayai ndai ya incubator mara kwa mara?​

Kiini tete cha njano. Kitagusana na kuta za yai na kitaganda hapo. Kitendo ambacho kitasababisha kifo. Kumbuka kugeuza mayai kama ilivoelekezwa. Yakiwa ndani ya incubator.

Itakusaidia kuepusha kitendo hichi. Na itaongeza ukuaji mzuri wa kiinitete chako.

Je kuna incubator ambazo zinageuza mayai zenyewe?​

Ndio. Zipo na zinakitu kinaitwa (automatic turner). Kifaa hichi kipo kugeuza mayai kila baada ya masaa manne. Nikimaanisha kinazunguka taratibu. Na kufanya robo mzunguko wa kwanza. Ndani ya lisaa limoja. Nusu mzunguko ndani ya masaa mawili. Na kumalizia kabisa mzunguko mzima ndani ya masaa 4.

Nitajuaje kifaranga kimekufa ndani ya yai?​

Kwa kutumia mshumaa. Muulika ndai yay ai ukiona kuna vimishipa vidogo vya damu. Jua kuwa ukuaji unaendelea. Na njia zingine zipo lakini hii ndio nzuri pale unapotumia incubator.

Ni kwa mda gani mayai yanaweza kukaa ndani ya incubator bila kuwa na umeme?​

Kukatika kwa umeme kutasababisha kupungua kuanguliwa. Kwa mayai kwa asilimia 40 hadi 50. Na kwa kipindi tu umeme ukikatika kuwa makini sana kuangalia. Mayai yako ndani ya siku 6 kama yanaendelea na ukuaji. Na kama baada ya siku sita haujaona mabadiliko. Sitisha mara moja kitendo cha incubation.

Je nahitaji kuyaosha mayai kabla sijayaingiza kwenye incubator?​

Hapana. Kwanza epuka kushika mayai ukuwa na mikono yenye maji mengi. Na hairuhusiwi kuosha mayai kabla ya kuyaweka kwenye incubator.Kumbuka kua maji maji yanaongeza uzalishaji wa bacteria. Ndani ya kuta za yai. Na ni vizuri kuku wako wanao taga kuwaandalia mahali pasafi. Pa kutagia ili usipate maswali kama haya.

Je ni incubator gani nzuri nitakayoweza kununua?​

Kutokana na mahitaji yako. Nikimaanisha kama unataaka uzalishaji wa kuku wengi. Inahitaji kuchagua. Incubator yenye uwezo wa kuweka mayai mengi. Na pia kama utataka incubator ndogo lakini. Yenye uwezo wa kufanya kila kitu yenyewe. Pia zipo na zina bei zake.

Kumbuka kuwa makini sana kwenye kuchagua incubator yenye ubora. Na katika kuchagua incubator yenye ubora unahitaji kuzisoma kwanza. Au kushauriwa ili upate matokeo mazuri.
 
naomba kujua,unaposema joto lisizidi au kupungua 99.5 degree,ni katika unit gani?,celcius,au faehneit?,
 
Mimi Niliseti siku 18 za kwanza joto 37.8 na unyevu 63 na siku ya 18_21 nimeweka joto 36.5 na unyevu 73 je niko sawa? Naombeni ushauli wenu
 
Back
Top Bottom