Incompatible "analogue" party in the "digital" citizens | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Incompatible "analogue" party in the "digital" citizens

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by soldado, Sep 9, 2010.

 1. soldado

  soldado Member

  #1
  Sep 9, 2010
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna mdau alitoa maoni haya katika website ya gazeti la Mwananchi jana 08/09/2010...


  "Watanzania walio wengi ni maskini kiasi kwamba ukiwa angani kwa ndege vijumba vyao vinaonekana kama vichuguu! Ni vigumu kutofautisha kichuguu na nyumba. Tangu Mungu aumbe dunia hii, hawajapata mabadiliko yoyote!

  Maisha yamekuwa magumu kiasi kwamba ni nafuu hata wakati wa ukoloni walipokuwa manamba katika mashamba ya wazungu. Hata hivyo, nchi yenyewe, imebarikiwa na utajiri wa ajabu wa maliasili. Lakini cha ajabu, tangu ukoloni hadi leo wanaendelea kuishi na kuzaliana katika vijumba vya matope mithili ya panya katika shimo.

  Wanakufa na kilimo cha jembe la mkono, na wala mazao yao hayana soko. Kilimo chenyewe hadi Mungu mwenyewe awahurumie, alete mvua! Wamebaki kujihangaikia wenyewe usiku kucha, mchana kutwa, mithili ya wakimbizi wasiokuwa na serikali. Sera za maendeleo ni maneno matupu. Maendeleo yenyewe ni yale ya ufukunyuku! Watanzania wamekwishachoka na kukata tamaa. .

  Wakijaribu kufukua maliasili waliyo nayo, CCM inawaambia ni wachimbaji haramu. Wakiamua kuishia baharini na ziwani kuvua samaki, na hapo napo CCM na serikali yake inaambia ni wavuvi haramu. Wakiishia maporini kuwinda na kutafuta kitoweo, na huko nako CCM wapo. Wanawanyooshea kidole, wanaambiwa wao ni majangiri na wawindaji haramu. Mbuga za wanyama zinauzwa kwa wazungu, ambao wanapewa kibali cha kuua watanzania maskini, majangiri! Dhahabu zimekwapuliwa na makaburu. Hadi ardhi nayo inapigiwa tena mahesabu, tena mazito! Sasa vijana wote wameishia Dar es salaam. Msongamano wa watu na magari unatia kichefuchefu. Na huko nako CCM inawaambia ni vibaka na wazururaji. Hivi wamemkosea Mungu nini hawa?

  Hao ndio watanzania ambao bila aibu wala msongo wa dhamira, CCM bado inawarubuni kwa kauli mbiu za kitapeli za maisha bora, ambayo hawajayaona mpaka leo, mpaka kesho! Ni utapeli mtupu! Wanabaki tu kudanganywa na vitisheti vya kijani na vikofia vya njano, huku dhahabu na almasi zao zinakwapuliwa. Wanachekelea na kushangilia mithili ya watoto walio na mtindio wa ubongo, ambao wakiona hata nzi anaruka, wanacheka na kurukaruka!

  Ndivyo CCM inavyowafanya watanzania. Sasa wanaume wazima na akili zao hata hawajiulizi hizo ahadi walizoahidiwa mwaka 2005 ziko wapi! Wamekwishasahau ! Maisha yako palepale. Bado wanaendelea kuishi katika vichuguu. Hakuna maisha bora wala ndugu yake maisha nafuu. Sasa wanadanganywa tena na vyandarua..

  Kana kwamba rushwa ya vikofia na vyandarua haitoshi, wakaona ni afadhali wawanyemelee na viongozi wa dini kwa rushwa ya futali. Wakaambiwa siku hiyo wavae dadhifu,. Mungu bariki viongozi wa dini wakashituka. Ni wasomi hawa! Ni masikini, lakini mang'amuzi wanayo! Wakakataa futali ya Kikwete! Wakasema wazi kuwa hiyo ni rushwa.. Maaskofu wamefungua watanzania macho. Hongereni sana viongozi wetu wa dini.

  Wanaume wenzangu wengine walioelemewa na kimeta cha CCM wajifunze kutoka kwa maaskofu!Wanaum e wengine wanatisha! Utakuta mwanamme wa familia ya watoto saba hana hata baiskeli! Chakula chake cha siku hadi atambikie! Uwezo wa kuwalipia watoto ada, ni songombingo! Wakati huo, kwa pembeni kuna mwanamke mmoja mrembo, eti first lady anatembea na msafara wa magari 20 na posho kibao. Bili hiyo inalipwa na maskini wanaolala katika vinyumba mithili ya vichuguu.

  Na kwa bahati mbaya, mwanaume huyo wanasimama kuushangilia msafara wa first lady. Kisa na mkasa? Pengine ni kwa sababu ya kuosha macho. Au hawajawahi kuona msafara mkubwa namna hiyo! Anasema ni sawa! Hata mke wa rais wa America anatumia msafara wa magari ishirini. Ama kweli! Hiki nacho ni kimeta kingine kilichodumaza fikra na mang'amuzi ya watanzania. Tangu lini limbukeni wa Bagamoyo akalinganishwa na mke wa rais wa America? Hii ni kufuru!

  Watanzania wameelemewa sana na utando wa buibui na tongotongo za kitapeli za ccm. Wanahitaji maji ya kunawa watoe tongotongo machoni, tena maji yenyewe, yawe na dawa inayowasha kidogo ili kuwazindua kwa vile akili za watanzania walio wengi zimedumaa. Wamekwishapachi kwa kasumba ya kudhani kwamba unyonge na umaskini ni jadi yao, na kwamba kuondokana na hali hiyo si rahisi.

  Hadi inashangaza! Katika karne ya leo, vijijini watanzania wanaishi maisha ya ujima. Tena kwa kuloa samaki na kuwinda? Wengine ukiwatazama, wana dalili za utapiamlo. Lakini bila aibu hao ndio CCM inawarubuni kwa rushwa za vikofia na kuwatumia tu katika kampeni. Baada ya ushindi hawakumbukwi tena na baadala yake wanaendelea kunyonywa.

  Chadema inawapigia tarumbeta! amkeni, kumepambazuka! Mmedanganywa vya kutosha! Hizo tongotongo hadi lini? Msitazame tena mambo ya vyama. Tazameni watu wenye uzalendo wa kweli watakaowaonyesh a dira ya kimaendeleo. Wakati ndio huu, na saa ya ukombozi ni sasa.

  Ninyi mlioelemewa na kimeta cha CCM, msiendelee tena kuzubaa katika dimbwi la umaskini. Jinasueni! Msitapetape tena na CCM kama vifaranga vya kuku vinavyopigwa na mvua kali wakati mama yao akiwa analiwa na kimbulu! Endeleeni tu kuikumbatia CCM wakati maliasili kama dhahabu inaliwa na vimbulu wachache.

  Simameni, mseme Imetosha! Kwa nini kuendelea tu kushangaa na kukodoa tu macho mithili ya mijusi waliobanwa na mlango msijue namna ya kujinasua? Amkeni mjinasue, kabla mafisadi hawajawabana na mlango sawasawa!

  Tuma ujumbe huu kwa haraka kwa ndugu, jamaa na marafiki, babu na bibi yako kule kijijini ambao bado wamesinzia wakidhani kuwa bado Nyerere ndiye rais wa nchi hii. Uwaambie Nyerere ameisha kufa. Nchi imetekwa nyara na tayari wamekwisha wekwa rehani!

  Fanya haraka kutuma ujumbe huu kwa njia ya simu kama unayo, au kwa njia ya barua posta, mradi tu vibaka wasiikwapue njiani wakidhani ni hela, maana njaa ni kali kweli kweli!. Uwaambie waamke! Wakati ni huu! Mwenye Masikio ya kusikia na asikie!

  Mwenye maoni awasiliane nami kwa e-mail hii: mak.ralph[​IMG]yahoo.com"
   
 2. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  nimeipenda sana hii mkuu
   
 3. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,326
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kweli ni ujembe muhimu kwetu sote, ni muhimu usambae hadi kwenye mizizi na mashina ya jamii zetu sote.
   
Loading...