Inawezekanaje wanafunzi 5,000 waliofaulu wasijue kusoma, kuandika?

Hiyo yote ni mbinu ya chama cha mafisadi kuwanyang'ang'anya wanainchi maskini fedha kwa sababu ya matumbo yao.

Ila mwisho wao hakika yaja!
Wapende wasipende!
 
Wadau kuna wanafunzi 22 wasiojua kusoma na kuandika darasa la tatu na la nne shule ya msingi Ngira. Kuna wanafunzi 102 jumla wanaosoma class 3 na 4.ANAEPASWA KULAUMIWA NI NANI? JE NI MWALIMU?JE NI MWANAFUNZI MWENYEWE?"Wakaguzi wamewaletea noma walimu". Hao wanafunzi wengine mbona wanajua?
 
Mi nashindwa kuelewa kwa nini inapenda kuwakandamiza walimu? Hivi yenyewe imeshajiuliza imetimiza wajibu wake walimu na shule zake kwa ujumla. Unambiwa siku hizi haipeleki hata ruzuku hata ikipeleka ni kidogo sana tena kwa kuchelewa. Hivi inawadharau kiasi hicho hii ni sawa na bosi anaemdharau house girl/boy ni rahisi sana kuwekewa kinyesi kwenye chakula.
 
Kwanza huu uzi hapa nilipo uweka ndiyo pake au nimekosea?Maana naona jukwaa la Lugha upo,Elimu upo na hata jukwaa la siasa upo.Kila siku nasikia waliofaulu kujiunga na elimu ya kidato cha kwanza hawajui kusoma wala kuandika,Hivi ni waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza au walioteuliwa kujiunga na kidato cha kwanza? na kama wamefaulu au wameteuliwa kujinga na elimu ya sekondari ni vigezo gani vilivyo tumika? na hao ambao hawakufaulu/kuteuliwa wako katika hali gani?JF naomba tulijadili ili tujue elimu yetu ya bongo.
 
ninavyoona hata wewe hujuwi kusoma kwa sababu unauliza swali ambalo unaweza kusoma na kupata jibu lake
NANUKUU
''Kwanza huu uzi hapa nilipo
uweka ndiyo pake au
nimekosea?Maana naona
jukwaa la Lugha upo,Elimu upo
na hata jukwaa la siasa upo''
Ushauri
kajifunze kusoma
 
Hiyo issue mkuu mbona ni ya cku nyingi sana? Watu wameshaijadili vyakutosha.enough is enough.
 
Asiyejua kusoma wala kuandika hawezi kuwa amefeli wala kufaulu kwani kafanya mtihani? utasemaje kafeli wakati hakujua umeuliza nini? Labda oral ingemsaidia huenda anajua majibu kashindwa kusoma swali
 
Kwanza huu uzi hapa nilipo uweka ndiyo pake au nimekosea?Maana naona jukwaa la Lugha upo,Elimu upo na hata jukwaa la siasa upo.Kila siku nasikia waliofaulu kujiunga na elimu ya kidato cha kwanza hawajui kusoma wala kuandika,Hivi ni waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza au walioteuliwa kujiunga na kidato cha kwanza? na kama wamefaulu au wameteuliwa kujinga na elimu ya sekondari ni vigezo gani vilivyo tumika? na hao ambao hawakufaulu/kuteuliwa wako katika hali gani?JF naomba tulijadili ili tujue elimu yetu ya bongo.

•Shule ya msingi janja janja imefaulisha wanafunzi wote.
•kwa kua hyo sredi ipo sehemu zote tatu basi tuwashauri mods waanzishe jukwaa "MTAMBUKA"
 
kuna watu wa kule fb wakija hapa wana toa pumba tuu,Tunazungumzia mustakabadhi wa elimu yetu wao wanachangia pumba,kama hamna cha kuchangia si mkae kimya au mrudi fb.Kikubwa hapa nini kifanyike ktk kukuza elimu ya Tz maana wahusika wanapita huku kunamichango mizuri huwa wanaichukua na si kila kitu pumba.Hapa tunaangalia ni kwanini kama wahusika wapo makini ni kwanini amalize darasa lasaba na asijue kusoma wala kuandika? au mtu anamaliza kidato cha nne ajui kuzungumza kingereza? tatizo ni mwanafunzi,mwalimu au serekali yetu?
 
Hivi karibuni tumekuwa tukiona matangazo na misisitizo kuhusu kuzipigia kura Mbuga ya Serengeti na Mlima Kilimanjaro kuingia katika MAAJABU YA DUNIA. Mfano, kigezo cha Serengeti, ni kuwa Makundi makubwa ya wanyama yanayohama kutoka sehemu kwenda nyingine na kurudi katika eneo hilo hilo. Kuna taarifa ambazo ni rasmi katika nchi yetu ya Tanzania, kuwa kuna Wanafunzi wanamaliza DARASA LA SABA NA KUFAULU VIZURI NA KUCHAGULIWA KUINGIA KIDATO CHA KWANZA lakini GHAFLA wanagundulika HAWAJUI KUSOMA wala KUANDIKA.Ndugu zangu hili JAMBO ni la AJABU SANA. Likipata wadau wakulipigia debe, hili nalo laweza kuwa AJABU LA DUNIA.Yaaaaaaaaaaaaaaaaaaaani, kwa watu waelewa hii ni Ajaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaabu saaaaaaaaaaaaaaaaaaana.
 
siku hiz uwa awafaulu,wanachaguliwa tu sababu ya shule nyingi za kata,mtihan upo tu kama kanuni lakin kuchaguliwa awaangalii matokeo,wote wanachaguliwa tu kujiunga kidato cha kwanza
 
Back
Top Bottom