Inawezekanaje wanafunzi 5,000 waliofaulu wasijue kusoma, kuandika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inawezekanaje wanafunzi 5,000 waliofaulu wasijue kusoma, kuandika?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MziziMkavu, Apr 17, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  TUMEGUSWA mno na habari zilizotoka katika vyombo vingi vya habari juzi kwamba, hatimaye Serikali imekiri kuwa, udanganyifu unaofanywa na wanafunzi katika mitihani ya kitaifa ni mkubwa na kusema ni janga la taifa linalohitaji hatua za haraka kuudhibiti hasa katika shule za Serikali.

  Katika kuonyesha ukubwa wa tatizo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillipo Mulugo aliliambia Bunge juzi kwamba wizara yake imegundua kwamba shule za Serikali ndizo zilizoongoza katika uchakachuaji wa mitihani ya kumaliza elimu ya msingi iliyofanyika mwaka jana na kusema kuwa, wakati shule za binafsi zilizogundulika kufanya udanganyifu zilikuwa 32, shule za Serikali zilizofanya hivyo zilikuwa 300.

  Akijibu swali la Mbunge wa Mufindi Kusini, Mendrad Kigola aliyedai Serikali haikuwatendea haki wanafunzi 9,736 waliofutiwa mitihani yao na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), 361 kati yao wakiwa katika Wilaya ya Mufindi ambapo sasa watatakiwa kurudia mitihani hiyo Septemba mwaka huu, Mulugo alisema msimamo wa Serikali hauwezi kubadilika na kwamba adhabu iliyotolewa ni kwa mujibu wa sheria za nchi.

  Msimamo huo wa Serikali unakuja wakati zipo taarifa za kushtusha kwamba wanafunzi 5,200 waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu hawajui kusoma wala kuandika na kwamba Serikali inapanga siyo tu kuwaachisha masomo, bali pia inaangalia uwezekano wa kuwachukulia hatua za kisheria wanafunzi hao na wakuu wa shule wanazotoka. Idadi hiyo ya wanafunzi ni ya mikoa yote ya Tanzania Bara, isipokuwa Kigoma ambao taarifa zake hazijawasilishwa wizarani. Kwa maana hiyo, ni wazi kwamba takwimu za mkoa huo zikiwasilishwa wizarani idadi ya walioingia sekondari bila kuwa na sifa bila shaka itaongezeka.

  Idadi hii ya wanafunzi wasiojua kusoma wala kuandika, licha ya ‘kufaulu' mtihani wa darasa la saba mwaka jana na kuchaguliwa kuingia kidato cha tano mwaka huu ni kubwa mno kwa kigezo chochote kile. Hiki ni kitendawili kinachopaswa kuteguliwa haraka iwezekanavyo na tunayo kila sababu ya kuelekeza lawama kwa vyombo vya usalama kwa kushindwa kugundua mtandao huo wa kuchakachua mitihani hadi kuachwa ukaenea nchi nzima bila kugundulika. Ndiyo maana tunakubaliana na Waziri Mulugo anaposema kwamba uchakachuaji huu sasa ni janga la taifa.

  Ni janga la taifa kwa sababu uchakachuaji wa mitihani sasa unaonekana kujipa mfumo wa kitaasisi. Kwamba mwanafunzi anaweza kumaliza elimu ya msingi bila kujua kuhesabu, kusoma wala kuandika na akaingia sekondari hadi kidato cha nne hakika haiingii akilini. Ni kwa bahati nasibu tu kwamba wanafunzi hao 5,200 wamegundulika kutojua kusoma na kuandika baada ya kupewa majaribio ya kupima uwezo wao baada ya kuripoti shuleni kama ilivyoagizwa na Waziri Mulugo mwenyewe.

  Itakumbukwa kwamba alipotangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba Desemba mwaka jana, Mulugo aliagiza kwamba wanafunzi wote ambao wangeingia kidato cha kwanza mwaka huu, kwanza wapimwe uwezo wao wa kusoma na kuandika. Agizo hilo lilitokana na udanganyifu uliojitokeza katika mtihani huo, ambao kama tulivyosema hapo juu, wanafunzi 9,736 walifutiwa matokeo kati ya wanafunzi 9,83,545 waliofanya mtihani huo.

  Hilo hakika ndilo janga la kitaifa. Tunapojenga mifumo ya kitapeli ya kuzalisha wataalamu ‘vihiyo' matokeo yake ni makandarasi wanaojenga madaraja, majengo na barabara mbovu zilizo chini ya viwango; madaktari wanaopasua wagonjwa vichwa badala ya kufanya operesheni za miguu; au matapeli na vihiyo wengine waliomo katika ajira nyeti katika sekta za kilimo, elimu, viwanda, usafirishaji, nishati, maji, uchumi na nyinginezo.

  Janga hilo ndilo limetufikisha hapa tulipo, miaka 50 ya Uhuru bado tunaogelea katika umaskini wa kutisha licha ya rasilimali lukuki zinazotuzunguka. Katika hili, haitoshi kwa Waziri Mulugo kugundua tatizo na kukubali tu kwamba ni janga la taifa. Kinachohitajiwa sasa siyo maneno, bali ni dawa ya kukomesha janga hilo la udanganyifu katika mitihani.

  Chanzo:
  Inawezekanaje wanafunzi 5,000 waliofaulu wasijue kusoma, kuandika?
   
 2. m

  mhondo JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Ni ajabu la nane la dunia. Tanzania imewezekana.
   
 3. Chuck j

  Chuck j JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2012
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 1,991
  Likes Received: 417
  Trophy Points: 180
  Hiyo ni sera ya ccm,ili wawe na takwimu nzuri,
   
 4. The_Emperor

  The_Emperor JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 884
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  wakijua kuhesabu pesa inatosha!
   
 5. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Wamepelekwa shule lili ionekane kuwa sera ya taifa ya kuhakikisha kuwa wanafunzi wengi wanajiunga na kidato cha kwanza inatimia
  Kwanza tatizo ni la kuanzia walimu wao huko walikotoka, pili wasahihgishaji ambao waliwasahihishia mitihani yao wakijua kuwa hao wanafunzi hawajaandika lolote wakawapa point za kufaulu, tatu waliowachagua na ambao walijua kabisa wanafunnzi khao hawana kitu kichwani na wakapewa shule
  Hivi huu ni uzembe au ni nini tuseme
   
 6. m

  meekuokanyi Member

  #6
  May 21, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwanafunzi anafaulu darasa la saba kuingia sekondari lakini hajui kusoma wala kuandika. Wizara ya elimu inalichukuliaje hili suala? Tuendelee kuwaamini wasahihishaji mitihani? Baraza la mitihani linahusika hapa pia.
   
 7. Gedeli

  Gedeli JF Gold Member

  #7
  May 21, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 452
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  inawezekana maswali yalikuwa ni yakuchagua kwa hiyo asiye jua kusoma hawezi kushindwa kuandika A au B au C na kubahatisha . lakini serikali imeka kimya bila kutoa tamko lolote hi inatisha sana
   
 8. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Hayo ndo baadhi ya mambo ambayo yanawezekana Tz tu,huwezi ona kwingineko
   
 9. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280

  hii ni kansa katika elimu ya tanzania.

  nina mifano halisi. mwanafunzi hajuwi alphabet, hajuwi hajuwi kitu. aibu sana.
   
 10. Alonick Antony

  Alonick Antony Member

  #10
  May 21, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mitihani ya majibu ya kuchagua ingefutwa...maana nasikia hata hesabu zilikuwa na majibu ya kuchagua!
   
 11. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #11
  May 21, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  mbona kuna form 3 hawajui kusoma wala kuandika wapo hapa tunawafundisha bora liende. Timed bomu.
   
 12. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hii issue msichukulie kisiasa. Ulaya hata Form four kuna mitihani ya kuchagua. Mitihani ya Darasa la saba Globaly ni ya kuchagua. Tatafueteni kiini cha tatizo
   
 13. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #13
  May 21, 2012
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Huwa hawasahishi, mara nyingi huchagua kwa kusema ana ana ana do.
   
 14. k

  kiliochangu JF-Expert Member

  #14
  May 22, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 1,122
  Likes Received: 774
  Trophy Points: 280
  wanaofikiri mtihani ya kuchagua ndio chanzo cha tatizo hawajui utaini ni nini. Chance ya mtahiniwa kupata jibu sahihi kwa ku-guess ni ndogo sana. Haiwezekani mtoto aka guess akapata zaidi ya 100/250 haiingii akilini. Jaribu kufanya mtihani/Test yoyote ufanye guessing uone utapata ngapi.
  Tafuteni chanzo cha Tatizo. ili ni bomo la Taifa.
  Tusiposhikamana kwa kila mtu katika eneo lake kukabiliana na ili hakuna hatakayepona kwani mzimu huu utakula watanzania kila mahali. wakipenya hawa wakienda nje ya nchi, wakigundulika kila mtanzania ataonekana ni bure tu.
  Tuwe makini
   
 15. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2012
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hawa wanawaonea kwa sababu hawakufeli wala kufaulu - ni kwamba hawakufanya mtihani
  Ili wawe wamefeli ilibidi wajue wamweulizwa nini, sasa kama hawajui kusoma unasemaje wamefeli.. mambo ni mazito zaidi ya kufeli.. siku zijazo tutalazimika tuwafanyie wengine óral interview' you never know huenda maskini wanajua majibu basi tu wameshindwa kusoma kugundua wanaulizwa nini

  Nchi hii sijui tunaipeleka wapi, hawa nao wana waalimu toka darasa la kwanza na waalimu hao hawajagoma
   
 16. A

  Aswel Senior Member

  #16
  May 22, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 114
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hapana Baraza la mitihani halihusiki kabisa, kwani mambo hayo yanafanyika mashuleni kwa mwanafunzi ambaye hajui kusoma anafanyiwa mitihani na wenzie au walimu wenyewe, si kweli kwamba baraza linachakachua, mtindo wanaoutumia wanafunzi wa shule za msingi wanauita SHIKWAMBI yaani shinda kwa mbinu. Solution ya suala hili labda walimu wa kusimamia mtihani wa darasa la 7 wawe walimu wa sekondari kidogo hawa walimu wapo strictly kwenye usimamizi wao.
   
 17. Michese

  Michese JF-Expert Member

  #17
  May 22, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  haya mambo mbona yapo siku nyiiingi usishangae ndio bongo hiyo.watu wanaingia hadi chuo kikuu kwa kubaisha babaisha na wanamaliza kwa kudesa tu gpa kuubwa tu.
   
 18. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #18
  May 22, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,984
  Likes Received: 1,906
  Trophy Points: 280
  Mtoa mada umegusa kitu nyeti sana katika taifa hili. Ila ukweli ni kwamba si kwamba mitihani ya taifa haina kiwango la hasha. Tena katika vitu ambavyo huwa vinaandaliwa kwa umakin mkubwa ni mitihani hasa ya taifa. Tatizo kubwa ambalo limefanyiwa tafiti japo siyo maalum ni kwamba wazazi wanahusika kwa upande mmoja na mwalim na mwanafunzi kwa upande mwingine.

  mzazi anahusika vipi? hapa nitabainisha mabo ambayo mzazi anyafanya kwakujua ama kwa kutokujua kuwa anadumaza elimu ya mwanae. Ni jambo la kawaida kabisa kwa wazazi kutokufuatilia maendeleo ya watoto wao kielimu.Katika kujisahau huku kunapelekea mtot kukosa motisha na hatimaye kuishi ajuavyo. Sasa basi mzazi anapokumbuka hili mwishoni wakati wa mitihani huanza kutafuta njia mbadala ikiwemo kutoa hela mwanae aonyeshwe majibu ya mtihani au hata kununua jina la mwanafunzi mwingine.

  waalimu nao kwa upande wao, wamejisahau, hawana moyo wa uwajibikaji, wanaona ni kama kupoteza muda kumfuatilia mwanafunzi kielim na kimaadili. sasa kwa kukosa uwajibikaji huu, mwanafunzi anakosa mtu wa kumwelekeza na hatimaye atashindwa tu kupata elim iliyo kusudiwa. Pia waalim hasa wa shule za msingi hujishughulisha na kuwaonyesha wanafunzi mitihani au hata kuwafanyia.

  mwanafunzi kwa upande wake wamekuwa ni mtoto asiye na maadili toka nyumbani, ajapo shule unakuta hajajitambua na hakuna mtu anayemwongoza ili ajitambue.

  ukiunganisha yote haya utagundua mwanafunzi asiyejua kusoma na kuandika na kafaulu yuko sekondari basi ni matokeo ya mazazi na mwalimu wake. msahihishaji wa mtihani(baraza) ni ngumu kujua mwandiko wa mwanafunzi husika, au pia kujua mtihani huu mwanafunzi kakopy au la. so turudi nyuma tujitahtmin sisi wazazi na waalim kabla ya kutupia lawama serikali.
   
 19. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #19
  May 22, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Sio kila kitu kuilaumu Srikali! Hivi we Mzazi mwanao Miaka saba anenda shule hujawahi hata siku moja hata kukusomea sentesi moja iliyoandikwa mzazi nae atakuwa ni Chizi mwandamizi!
   
 20. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #20
  May 22, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  hesabu za kuchagua jibu unategemea nini?aliyefeli shule ndie anaenda kusomea ualimu hiyo ni viscous circle!
   
Loading...