Inawezekanaje bajeti ya Kenya ikawa kubwa mara mbili zaidi ya Tanzania?

666 chata

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
1,688
3,816
Hakuna neno lingine zaidi ya haya ni maajabu?

Kenya ina watu milion 53 huku Tanzania ikiwa na watu takribani milion 60.

Ukubwa wa Tanzania ni kilomita za mraba laki 9++ huku kenya wakiwa na eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba laki 5++.

Nchi ya Tanzania iko mbele mara elf moja dhidi ya kenya ktk mambo yote yenye kuleta faida kubwa kiuchumi kwa kuanzia maliasili, malighafi, madini, utalii, rasilimali watu, jografia nzuri na siasa safi.

Umoja uliopo Tanzania ni mkubwa mara elfu dhidi ya ule wa Kenya ambao wako kimakundi makundi tokana na ukabila.

Sasa inawezekanaje nchi kama Kenya ikawa na bajeti ya Tshs Trillion 66 huku Tanzania ikiwa ni Tshs Trillion 38?

Mambo haya yanawezekanaje jamani? Kwa bajeti hio ya kenya ni wazi kwamba wenzetu hawa kila kitu wako mbele yetu mara mbili zaidi!

ni nchi ya ajabu hii jamani daah.
 
Swali gani hilo ? Uchumi wa Kenya ni mkubwa kuliko Tanzania kwa tofauti kubwa tu au hilo nalo haulijui ? Isitoshe Kenya hakuna Makambas, hivyo wana umeme 24/7/365!
 
Soma hoja hizo vizuri, swala hapa sio wanatuzidi uchumi, swala ni nani ni tajiri dhidi ya mwenzake? uchumi wa export na import of goods haujustify kua kenya ni mkubwa kwetu.
 
Kenya ni tajiri zaidi ya Tanzania na tofauti ni kubwa sana tu, na ni tajiri kwa sababu Kenya ina uchumi mkubwa kuliko Tanzania, got it ?
 
Korea Kusini ni ndogo kuliko Kenya na ina watu wachache kuliko Kenya ila bajeti yake mara 15 ya Tanzania na uchumi wake kwa ujumla ni mkubwa mara 40 ya wa Tanzania
Hakuna neno lingine zaidi ya haya ni maajabu?

Kenya ina watu milion 53 huku Tanzania ikiwa na watu takribani milion 60.

Ukubwa wa Tanzania ni kilomita za mraba laki 9++ huku kenya wakiwa na eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba laki 5++.

Nchi ya Tanzania iko mbele mara elf moja dhidi ya kenya ktk mambo yote yenye kuleta faida kubwa kiuchumi kwa kuanzia maliasili, malighafi, madini, utalii, rasilimali watu, jografia nzuri na siasa safi.

Umoja uliopo Tanzania ni mkubwa mara elfu dhidi ya ule wa Kenya ambao wako kimakundi makundi tokana na ukabila.

Sasa inawezekanaje nchi kama Kenya ikawa na bajeti ya Tshs Trillion 66 huku Tanzania ikiwa ni Tshs Trillion 38?

Mambo haya yanawezekanaje jamani? Kwa bajeti hio ya kenya ni wazi kwamba wenzetu hawa kila kitu wako mbele yetu mara mbili zaidi!

ni nchi ya ajabu hii jamani daah.
 
Nchi zote duniani hazikosi watu wenye njaa, viwango ndio vinatofautiana.
Kweli bajeti ya Kenya ni kubwa lakini hawa jirani sijui fedha zinaenda wapi maana wananchi Wana njaa balaa.
 
Back
Top Bottom