Inawezekana vipi mtu aliyekuja Dar es Salaam mwaka 1992 kukosa kiwanja?

Habari wakuu

Hapa nilikuwa naweka ligi ya mabishano, hivi inawezekana kweli watu walioingia mjini hapa 1992 mpaka leo 2021 Hana hata kiwanja cha kuzugia kweli, enzi hizo maeneo ya Tegeta, Goba, Kawe, Bunju ilikuwa mapori matupu unafika unafyeka nyasi na kujipa eneo mwenyewe.

Mbaya zaidi ulikuwa ukitaka hata kiwanja cha jero pale Ubungo unapata, Sasa mtu ananiambia kaja DSM 1992 lakini tunaganga njaa hapa, imenibidi nitafakari kidogo.

Nimesikitika sanaa.

Uzi tayari ...!
Acha uongo wewe,,, ndo mnavyojidanganya hivyo nyie mliotoka mikoani juzi,, eti kawe mwaka 1992 kawe,Goba, unajikatia tu ovyoooo!
Wadanganye hao hao wa mikoani wenzio
 
Sends ya 2022 itaonesha wenye nyumba na wapangaji. Haitaonesha wenye viwanja kwani hatulali viwanjani
 
•√√ Hili suala ambao hatuna viwanja miaka hii pengne masera wapya wa mwaka 2050 watakuja na hoja pia kama hii, kuwa tulikwama wapi, basi labda tujiandae kukwepa pia fedheha hii.

USHAURI
•√√ Nimewahi kukaa mkoa wa Lindi aice kuna sehemu inaitwa ng'apa viwanja hawauzi kabisa, bali unapewa pori hekari unazotaka Ila uzihudumie ili eneo liwe lako jumla, usipolihudumia kwa mda utakaopewa basi eneo anapewa MTU mwingine, kupata eneo we nenda kwenye uongozi wa serikali ya kijiji au kwa mtendaji wa kijiji au kata, pia mapori yapo mengi tu huku mikoani na bei bado ni nafuu we nunua tu miaka ijayo ndo miji mingine hiyo.
 
Miaka ya 1990's ukisema umetoka Bunju ulikuwa unachekwa na kila mtu. Ulikuwa unaitwa ni MSHAMBA wa kutupwa. Sasa unasemaje?
kiongozi umenikumbusha kitu ,miaka ya 92 mzee alihama toka magomeni kuja boko(mangengeni) miaka ya 99 nilikuwa nasoma sec magomeni mapima ,basi nilikuwa nachekwa sana na wanafunzi wenzangu nikiwaambia natoka bunju ,na pia enzi hizo bunju Itv haishiki (kipindi cha analojia cha antena ) basi wanahadithiana michezo ya max na zembele nahisi kwenye 2000 na kitu kama sio 2002 au 2001 basi kwavile Itv haishiki japo mnatv sana sana mlikuwa mnapata Tvz (zbc kwa sasa) basi wanakucheka wanakuona wabushi unapitwa na kila kitu ,ILA LEO BUNJU HASHIKIKI ,
Tumekaa boko magengeni njia panda ya mbweni ,Mtu akikwambia kule ubungo (mbweni) akupe kiwanja bure hutakai ,Mbweni na ununio kulikuwa na baskeli zinakodishwa 300 za kwenda huko ila leo ununio pakishua mbweni pakishua
 
Habari wakuu

Hapa nilikuwa naweka ligi ya mabishano, hivi inawezekana kweli watu walioingia mjini hapa 1992 mpaka leo 2021 Hana hata kiwanja cha kuzugia kweli, enzi hizo maeneo ya Tegeta, Goba, Kawe, Bunju ilikuwa mapori matupu unafika unafyeka nyasi na kujipa eneo mwenyewe.

Mbaya zaidi ulikuwa ukitaka hata kiwanja cha jero pale Ubungo unapata, Sasa mtu ananiambia kaja DSM 1992 lakini tunaganga njaa hapa, imenibidi nitafakari kidogo.

Nimesikitika sanaa.

Uzi tayari ...!
Mkuu kuna watu wamezaliwa mjini na bado hawana hata kiwanja cha kufuga kuku.

Maisha ni yale yale ,,tofauti ni namba za miaka tu.
Kujenga ni Mungu akuzinduwe sio pesa.

Wapo watu walishindwa kununuwa hata nyumba za national housing ambazo zilizikuwa zinauzwa 10000 shillings.
Tena zilizikuwa zinakopeshwa.
 
Hiyo jero ilikuwa ngumu kuipata pia na hayo mapori unayoyataja hata sasa yapo mfano Bagamoyo, Msata, Chalinze
Watu wanazungumzia jero kama vile wanvyoweza kununulia chupa ya hill water kwa sasa. Enzi hizo watu wanatumia tsh.1-10 hivi ndio hela za kawaida. Hio 500 ulikuwa mshahara wa mtu huo!

Miatano ya zama hizo uki valuate kwa sasa inaweza kuwa sawa na laki 5 ya leo! Niliongea na mzee akaniambia yeye alinunua eneo kwa TZS 25,000 mwaka themanini huko wakati huo mbezi beach eneo ni TZS 600,000. Mambo yalikuwa tight vile vile msione kinyonge. Hizo hela zilikuwa ndefu sana.
 
Huwa wananichekesha wanavyojisifia,eti ooh me nimekuja mjini kabla baba yako hajafikiria hata kukuzaa wewe,kwa hiyo me mtoto wa mjini,ukimuuliza so what unamiliki nini hapa Town?anaanza kukuambia we dogo una dharau sana.
 
Naona huu uzi watu wanachukulia masihara. Kiukweli aisee tuache kubweteka. Miaka 20 ijayo watu watakua wanatushangaa pia kwa kutokuwa na viwanja pamoja na kuishi Dar muda mrefu. Tununueni viwanja. Sehemu kama Kigamboni kuna viwanja vingi. Usiseme kule ni pori. Nipigie kupata viwanja Kigamboni gezaulole, Kigamboni Kisarawe II, Kigamboni mji mwema, Kigamboni Dege Nk. 0762815104
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom