Inawezekana vipi mtu akajiajiri ambapo hajawahi kuuza hata karanga? Serikali acheni porojo, toeni ajira kwa wahitimu

Halafu ukiwaambia kitu na mifano wanakuita motivational speaker. Wakati najenga kibanda changu alipita kijana akaniambia bro naomba kazi ya madirisha, nikamuuliza mjumbe wa eneo lile unamjua huyu na anaweza kazi? Akaniambia namjua anaweza nikamwambia nitakuita. Hapo ndio anaanza anza, kweli ikafika siku nikamuita akaweka madirisha yote ya aluminium. Baada ya mwaka kama na nusu nakutana nae ana Vitz akaniambia bro mambo si mabaya sasa nashukuru watu wananiamini.
Baadae tena nikamuona na kirikuu akaniambia nimeuza ile Vitz nimenunua hii kwa ajili ya kazi yangu na sasa hivi nimeshaanza ujenzi karibu namalizia.
Huyu kijana ametoka Mbeya kaingia mjini kakodi fremu anatengeneza madirisha ya aluminium sasa hivi anaitwa hadi Mtwara kuwekea watu madirisha ofisi ishakuwa kubwa maisha yanaendelea. Sasa nyie hapa mjini na degree zenu subirini serikali iwaajiri.
Utawaudhi watu wewe motivesheni spika...kuna kadada kamemaliza sua kenyewe kanatengeneza karanga za kusagwa na mtindi....mtindi kanauza had lita 50 per day... ukimuuliza habar za kuajiriwa wala hana habari..huko.maofisini daily anapitisha ss ukimwambia mtu anakuambia alichosomea na anachofanya anajidhalilisha...na bado kanakaa kitaa mishe zinaenda! Kukosa kazi nchi yako ni uzembe
 
Yani huna ajira bado unaona aibu kuuza maji.. Aiseeee!!
Hii elimu yetu inahitaji marekebisho sana

Yes kama mzazi nitampa kijana wangu mtaji auze maji tatizo lipo wapi, huenda huko kwenye maji akapata fursa nyingine zaidi na kuonekana.

Watu huanza kuthamini kujituma kuliko blah blah za nimegraduate..
Kwani nimebisha basi,we muweke tu
 
Mtaa nauelewa mzee baba sema huwezi jua kila kitu but through experiences! Nafanya engagement mdo mdo ili kupata more experiences...
mzee kariakoo kuna mawinga siku hizi mpaka graduate
mtu anampanga mteja kwenye mzigo anakula mpaka 100000
kupitia wale wateja wanatengeneza majina wanatumia mpaka wateja nje ya nchi

maisha yakikupiga vizuri utanyanyuka aibu inaondoka na unafanya chochote kujinusuru
ila mwaka wa kwanza au wa pili toka chuoni mtu anashinda kwenye ajira portals
 
Wewe hukwenda kujiajiri kwa kukosa option, you went there because you chosen that path! Wanaolalamika hapa ni hawa ambao waliambiwa soma mwanangu upate kazi nzuri akili imejengwa hivyo toka ground “0” halafu ghafla unaambiwa kazi amna jiajiri!
You have the point bro.
 
Halafu ukiwaambia kitu na mifano wanakuita motivational speaker. Wakati najenga kibanda changu alipita kijana akaniambia bro naomba kazi ya madirisha, nikamuuliza mjumbe wa eneo lile unamjua huyu na anaweza kazi? Akaniambia namjua anaweza nikamwambia nitakuita. Hapo ndio anaanza anza, kweli ikafika siku nikamuita akaweka madirisha yote ya aluminium. Baada ya mwaka kama na nusu nakutana nae ana Vitz akaniambia bro mambo si mabaya sasa nashukuru watu wananiamini.
Baadae tena nikamuona na kirikuu akaniambia nimeuza ile Vitz nimenunua hii kwa ajili ya kazi yangu na sasa hivi nimeshaanza ujenzi karibu namalizia.
Huyu kijana ametoka Mbeya kaingia mjini kakodi fremu anatengeneza madirisha ya aluminium sasa hivi anaitwa hadi Mtwara kuwekea watu madirisha ofisi ishakuwa kubwa maisha yanaendelea. Sasa nyie hapa mjini na degree zenu subirini serikali iwaajiri.
Sikatai hii kitu
Lakini ukumbuke Kila mtu ana angle yake ya kutoboa
Na haiwezekani watu wote wakatoboa kwa biashara na ishu Kama hizo
Ndo maana Kuna ajira
 
Wakuu tusiweke nguvu kulaumu serikali, hebu tuwekeze nguvu kwenye kujifunza skills ambazo hatujasomea shuleni. Njooni tujiajiri kwenye affiliate na content marketing online wakuu, baadhi ya mapato yangu ya miaka minne ni haya (hizo figures ni kwa Pounds):

Capture.PNG
 
Utawaudhi watu wewe motivesheni spika...kuna kadada kamemaliza sua kenyewe kanatengeneza karanga za kusagwa na mtindi....mtindi kanauza had lita 50 per day... ukimuuliza habar za kuajiriwa wala hana habari..huko.maofisini daily anapitisha ss ukimwambia mtu anakuambia alichosomea na anachofanya anajidhalilisha...na bado kanakaa kitaa mishe zinaenda! Kukosa kazi nchi yako ni uzembe
Hana habari ila akija kuajiriwa hawezi kuikataa hiyo nafasi.

Mimi mwenyewe sijakaa nyumbani tu, napambana nikiwa sina kipaumbele cha Ajira.

Suala la kutoa na kuhakikisha Ajira zipo ni jukumu la serikali kwa asilimia 100.

Serikali kuwaambia vijana wajiajiri ni upumbavu usio na mfano.

Ni sawa na kibarua wako, umempa kazi na umemlipa pesa ya kufanya kazi hiyo lakini anabaki tu kukwambia boss usiwe mvivu jitahidi kufanya kazi usinitegemee sana mimi na wakati huo huo pesa za kazi anachukua.

Kama serikali imeshindwa jukumu hili la ajira, iondoke waje wanaoweza. Kwani lazima wawe wao????

Ni niwathibitishie hili, leo serikali imewashindwa kabisa machinga, imebaki kuhonga vyeo na pesa kwa bongo movie na bongo fleva, baada miaka 10 wanaenda kuwashindwa tena graduates.

Wakati huo vyuo vitakuwa vimetema kikamilifu.

Ndani ya miaka 10 ijayo hakika hii nchi, probably ikawaka moto. Maana haina mwelekeo.

Machinga haina pension, kuuza maji wala kuosha kucha hakuna pension.

Hizi kazi ni juhudi tu za KUBAKI HAI.

Kazi hivi huwezi kufanya ukalea na kusomesha EXTENDED FAMILIES.

Mimi nimefanya umachinga wa mabanda Kariakoo. Nilikuwa naamka saa 10 usiku, napanda gari nafika kariakoo saa 12 nafungua GOLI. Unauza mbele ya duka la mhindi huku ukiporomoshewa matusi. Unasimama masaa 12 kwasababu Kariakoo ni Crowded hakuna sehemu ya kukaa na huwezi kusimama mbele ya duka la mhindi kumzibia biashara yake.

Saa 12 jioni unafunga, unaanza kutafuta daladala mpaka unarudi gheto saa 4 usiku, unapitia kuku broiler gengeni unaenda kupika. Mpaka unamaliza kula ni saa 5 au saa 6 usiku. Kesho yake unaamka saa 10 alfajiri tena.

Kazi hizi hazina likizo, mwili ukikataa tu unapumzika mwenyewe.

Usidhani watu Dar wanaishi BACHELOR kwa bahati mbaya.

Pesa yote inaishia kwenye nauli, kodi ya nyumba, na chakula. Hata mama utashindwa kumtumia hata 100.

Tusubiri hao waosha kucha, waoshe mpaka 2030 na wakati huo Tanzania itakuwa inaendelea kuwa na watu zaidi MILIONI 70.

Mimi nimezaliwa kijijini, nimekuwa kijijini, hustles nazijua na ninaishi jijini.

Maisha ya wabongo bado hali ni mbayaaaaa.

Usione mtu ana kigari anapita ukafikiri ana maisha mazuri. Wengi hali ni mbaya, vigari wamenunua kwa kuunga unga sana wengine mikopo. Bodaboda akimkwaruza tu rangi la gari lake ndio utajua. Mfukoni hana hata MIA MBOVU.
 
Hana habari ila akija kuajiriwa hawezi kuikataa hiyo nafasi.

Suala la kutoa na kuhakikisha Ajira zipo ni jukumu ka serikali kwa asilimia 100.

Serikali kuwaambia vijana wajiajiri ni upumbavu uzio na mfano.

Ni sawa na kibarua wako, umempa kazi na umemlipa pesa ya kufanya kazi hiyo lakini anabaki tu kukwambia boss usiwe mvivu jitahidi kufanya kazi usinitegemee sana mimi na wakati huo pesa anachukua.

Kama serikali imeshindwa jukumu hili la ajira, iondoke waje wanaoweza. Kwani lazima ????

Ni niwathibitishie hili, leo serikali imewashindwa kabisa machinga, imebaki kuhonga vyeo na pesa kwa bongo movie na bongo fleva, baada miaka 10 wanaenda kuwashindwa tena graduates.

Ndani ya miaka hakika hii nchi, probably ikawaka moto. Maana haina mwelekeo.

Machinga haina pension, kuuza maji wala kuosha kucha hakuna pension.

Hizi kazi ni juhudi tu za KUBAKI HAI.

Tusubiri hao waosha kucha, waoshe mpaka 2030 wakati huo Tanzania itakuwa inaendelea kuwa na watu zaidi MILIONI 70.

Ni nchi gani huko wasomi wote wameajiriwa mkuu. Mie nadhan serikali iweke mazingira mazuri ya watu wazawa kufungua viwanda ajira zipatikane...means iwataftie masoko...kifupi tunajidanganya sana..hata chadema akiingia madarakani tusijifikirie MTELEMKO HUO..NEVER ON EARTH..serikali iko kusbsides tu mambo...!
 
Kichwa cha habari kinajieleza vizuri.

Hizi story za kujiajiri ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya viongozi wa serikali ambao wao ni waajiriwa zinaumiza sana.

Haiwezekani nipo shuleni kuanzia Nina umri wa miaka 6 Mpaka leo Nina miaka 25/26 then uje uniambie nijiajiri.

Najiajiri Nini Sasa?

Inaudhi sana.
Serikali haiwezi kuajiri kila mtu anayehitaji ajira
 
Ni nchi gani huko wasomi wote wameajiriwa mkuu. Mie nadhan serikali iweke mazingira mazuri ya watu wazawa kufungua viwanda ajira zipatikane...means iwataftie masoko...kifupi tunajidanganya sana..hata chadema akiingia madarakani tusijifikirie MTELEMKO HUO..NEVER ON EARTH..serikali iko kusbsides tu mambo...!
Hakuna nchi ambayo wameajiri wasomi wote. Hata kama wakitaka hawataweza kwasababu siyo kila mtu anataka ajira ya serikali.

Na mimi nikuulize swali ni nchi gani ambayo ina uhaba wa watumishi wa taaluma fulani na vijana wenye taaluma hiyo wapo mtaani lakini hawapewi kazi ????

Nikupe mifano miwili:

Sasa hivi kuna upungufu wa watumishi wangapi wa kada ya Afya ????

Ni zaidi ya ELFU TISINI.

Juzi wametoa nafasi za Ajira 3,300!!!!!

Wameomba watu 31,000 maana yake hata wataalamu wa Afya walioko mtaani wakiajiriwa wote bado upingufu wa watumishi hautaisha.

Sasa nambie ni nchi ipi ina upungufu wa Ajira wa aina hii ???

Tanzania kuna upungufu wa walimu wangapi ???

Leo kibali kinatoka cha kuajiri walimu 6,900 na waombaji ni 81,000???

Walimu wapo ila kuna upungufu mkubwa kiasi kwamba huko mashuleni mwalimu mmoja anafundisha darasa lenye watoto 120!!!

Ni nchi gani ina tatizo la Ajira la aina hii ???

Kama serikali inaamini kwenye kujiajiri, ni nini kinawafanya wachukue watu waliojiajiri kwa mafanikio na kuwapa teuzi za kisiasa?

Tanzania ina watu karibu MILIONI 60 lakini Serikali imeajiri Watu LAKI 5 tu kati ya hao 60M na inawalipa vimishahara vya wastani wa Tsh LAKI 5 tu. Na mpaka leo imeshindwa kuwahudumia.

Sasa hii ni serikali ya aina gani ?

Ni kipi kinawafanya watu kama BATILDA walikuwa mabalozi, kina Kafulila wamekuwa wabunge kuendelea kuajiriwa upya, badala ya serikali kuwaambia wajiajiri ili na wao waajiiri watu wengine?

Suala la kujiajiri ni personal issue. Mtu mwenyewe akiona kama kuna greener pastures kwenye kujiajiri anafanya na siyo serikali kuhubiri hili. Huku kukwepa wajibu wake.
 
Serikali haina pesa mkuu...mashirika yenyewe yanajiendesha kwa hasara...hili ni donda ndugu
Nafikiri sentensi sahihi inatakiwa, serikali haina pesa za kufanya mambo ya wananchi.

Kwa lugha rahisi inawadharau wananchi na wala siyo kipaumbele chao.

Wewe ulishawahi kusikia vyama vya siasa vimekosa ruzuku ?

Umewahi kusikia wabunge karibu 400 wameshindwa kulipwa mafao, tena huwa hawachangii. Ni pesa za kuchota tu hazina.

Kuna wazungu walikamata ndege huko Canada, walikuwa wanadai karibu milioni 300 na pesa za kuwalipa zilipatikana.

Kigwangallah alikusanya Bongo movie na bongo fleva akawapeleka kupanda mlima, Clouds wakala Milioni 600, Wasafi wakala 140M na TBC wakala 300. Kuna matokeo yoyote chanya kwenye utalii baada ya hilo tukio ?

Wazee wa Bodi ya TASAC walikaa vikao 12 kwa mwaka wakatafuna milioni 600. Maana yake kila mwezi ni 50M.

Funga kazi ni pesa za kuwalipa kina Halima Mdee, wabunge haramu kikatiba 19 zipo, ila za kuajiri vijana wa LAKI 5 hakuna.

Hakuna kingine zaidi ya dharau tu.

Hayo mashirika yanajiendesha kwa hasara kwasababu, wakurugenzi wake wanateuliwa WATAFUNE kwa wakati wao na siyo kuleta ufanisi wa shirika.

Kama mtu alimsaidia mtawala fulani wakati wa uchaguzi, baada ya uchaguzi akapewa shirika, unadhani kapewa ili shirika lipate mafanikio au kapewa sehemu ya ulaji tu kama shukhrani.

Mtu ANATAFUNA tu maana kwanini aumize kichwa kukuza shirika wakati anajua, akija mtawala mwingine na yeye ataweka watu wake.
 
Umelenga mule mule huu ujinga wakusema vijana mjiajiri wakati wenyewe wamekumbatia hizo ajira nikutuona wajinga.
 
Wazee wetu hawa wanatamaa, hawataki kuondoka maofisini.

Mfano mwaka jana yule mama mtakwimu mkuu wa serikali alimaliza muda wake akastaafu mpaka akaagwa. Wiki mbili zilizopita kwenye uzinduzi wa kitabu cha sensa, walipoita mtakwimu mkuu nashangaa anasimama yeye, nilibaki nastaajabu inamaana alirudishwa kimya kimya.

Hivyo hivyo ndio wanapeana kazi kwenye vitengo nyeti kwa kujuana.
Yule mama sijui ndio naibu spika eti anasema wakufunzi waongezewe muda wa kufundisha hata miaka 70 yaani ujinga ujinga.
 
Sasa hivi Ajira zinatolewa kwa WASTAAFU, WENYE AJIRA, WANASIASA, WALIOJIAJIRI na WANAOJIUZULU.
 
Vijana hata sisi tulioajiriwa na serekali tufukunzwe kazi wote au tustaff kwa maslahi ya umma

Then mkaajiriwa nyinyi,lazima kuna ambao watabakia uraiani sababu nafasi zitakuwa zimejaa

So na mkisubiri mpaka tusitaff mtangoja sana ndio kwanza ninae miaka 38 bado miaka 22 ya kufanya kazi

So anzia hapo hapo ulipo utatoboa tu
 
Back
Top Bottom