Wangari Maathai
JF-Expert Member
- Aug 13, 2018
- 34,962
- 70,472
Utawaudhi watu wewe motivesheni spika...kuna kadada kamemaliza sua kenyewe kanatengeneza karanga za kusagwa na mtindi....mtindi kanauza had lita 50 per day... ukimuuliza habar za kuajiriwa wala hana habari..huko.maofisini daily anapitisha ss ukimwambia mtu anakuambia alichosomea na anachofanya anajidhalilisha...na bado kanakaa kitaa mishe zinaenda! Kukosa kazi nchi yako ni uzembeHalafu ukiwaambia kitu na mifano wanakuita motivational speaker. Wakati najenga kibanda changu alipita kijana akaniambia bro naomba kazi ya madirisha, nikamuuliza mjumbe wa eneo lile unamjua huyu na anaweza kazi? Akaniambia namjua anaweza nikamwambia nitakuita. Hapo ndio anaanza anza, kweli ikafika siku nikamuita akaweka madirisha yote ya aluminium. Baada ya mwaka kama na nusu nakutana nae ana Vitz akaniambia bro mambo si mabaya sasa nashukuru watu wananiamini.
Baadae tena nikamuona na kirikuu akaniambia nimeuza ile Vitz nimenunua hii kwa ajili ya kazi yangu na sasa hivi nimeshaanza ujenzi karibu namalizia.
Huyu kijana ametoka Mbeya kaingia mjini kakodi fremu anatengeneza madirisha ya aluminium sasa hivi anaitwa hadi Mtwara kuwekea watu madirisha ofisi ishakuwa kubwa maisha yanaendelea. Sasa nyie hapa mjini na degree zenu subirini serikali iwaajiri.