Inawezekana tabia ya wahariri wa vyombo vya habari kutokujiongeza ndio kunachangia sana wanasia kuongea upotoshaji majukwaani

Siku hizi hata hamu ya kufuatilia media zetu zinatipoti nini inazidi kuniishia siku hadi siku.
Binafsi nilishaacha nategemea zaid habari za humu kwasababu vyombo vingi vya habari vinaandika kwa lengo la kumfurahisha jiwe na serkali yake
 
Tasnia ya vyombo vya habari nayo katika taifa hili iko shaghalabagala kwa sasa,viko hoi.
Unajua kuna jambo moja ambalo huenda watanzania wengi hawalielewi na jambo hilo ndio moja ya chanzo kikubwa cha wanasiasa wa nchi hii kuja na utetezi wa kusema "nimenukuliwa vibaya" wakati si kweli.

Ni hivi,wanasiasa wa nchi yetu, hasa wa kutoka chama tawala,wana tabia ya kuongelea mambo "kiujumlajumla" huku kwa makusudi wakiwepa kutoa details kwasababu wanajua wahariri wetu nao watawanukuu kiujumla hivyo hivyo bila kutafuta clarification ya kaulu zao na tena kwa kuzifanya kauli hizo kuwa ndio habari kuu katika media zao.

Mifano ipo mingi na hapa nitaongelea mifano mitatu ambayo miwili imetokea leo hii na mmoja ni wa siku za nyuma.

Mfano wa kwanza ni kauli ya leo ya Spika kuhusu Bunge kugharamia matibabu ya Lissu.

Ukimsikiliza kwa makini,utagundua Spika aliamua kuongea kwa ujumla kuwa Bunge limekuwa likimplipa Lissu fedha kinyume na madai ya Lissu kuwa tangu apigwe risasi Bunge limekata kumghramia matibabu yake.

Spika alikwepa kuweka wazi ni aina gani ya malipo kwasababu aliju kwa kutamka vile,kesho baadhi ya magazeti na pengine yote yangekuja na heading kuwa Bunge limelipa gharama za matibabu ya Lissu na hivyo kumfanya Lissu aonekane muongo.

Hata hivyo,huenda reaction ya mitandao kuhusu matamshi yake na tishio la CHADEMA kutakua kuonyesha uongo wa kauli hiyo,ndio kumemfanya aseme amenukuliwa vibaya vinginevyo asingetoa ufafanuzi alioutoa.

Mfano wa pili unahusu kauli ya Spika juu ya utata wa ni wapi zilipo fedha za umma kiasi cha shilingi trilioni 1.5 kama anavyohiji mhe.Zitto.

Ukimsikiliza Spika,utagundua kuwa anataka kumanisha kuwa Zitto ametamka kuwa serikali imeiba hizo fedha wakati Zitto anataka ufafanuzi wa wapi ziliko fedha hizo na kupitia ufafanuzi huo au uchunguzi utakaofanyika,ndio itafahamika ni wapi hasa fedha hizo zilipo au zilitumikaje.

Kama nilivyosema hapo awali, inawezekana kabisa Spika katoa ufafanuzi ule ambao binafsi nauona uko kisiasa zaidi akiamini kwa nafasi yake kama Spika, media zitamnukuu hivyo hivyo na kumfanya Zitto aonekane ni muongo na mzushi.

Mfano wa tatu ni kitendo cha Raisi kumuuliza CAG mbele ya vyombo vya habari kama kuna hela kiasi cha shilingi trilioni 1 5 zimeibiwa/zimepotea kama inavyoripotiwa.

Ukweli ni kwamba, Magufuli alijua CAG asingeweza kusema kuwa kiasi hicho cha fedha kimepotea kwani uchunguzi ni lazima ufanyike unless alitaka kumtega CAG ajichanganye kisha achukuliwe hatua.

Ninaamini Magufuli alitarajia jibu la hapana kutoka kwa CAG na pia alitarajia wahariri wangeichukua kauli hiyo ya CAG kama ilivyo na hivyo kumfanya Zitto aonekane Muongo kama ambavyo hata Spika leo hii ametumia kauli hiyo kutaka kuwafanya watu wamuone Zitto ni muong na mzushi.

Kwahiyo, kwa mifano hii michache, utagundua tabia ya baadhi ya wahariri kupokea habari kama zilivyo na kuziripoti bila kujiongeza kwa kutaka ufafanuzi wa ziada kwa mfano kutoka kwa CAG mwenyewe au Zitto, ndio kunapelekea wanasiasa kuongea mambo kiujumla jumla huku wakikwepa kutoa details kwani wanaamini baadhi ya wahariri watazitoa kama zilivyo na hivyo malengo yao ya kisiasa yatatimia.

Na katika wamu hii, bwana mkubwa anautumia na kufaidika sana na udhaifu huu wa media zetu kugeuka kuwa ni media za kuripoti tu kila akisemacho bila kujiongeza na kumsaidia mwananchi kuelewa ukweli hasa ni upi.

Tushukuru sana uwepo wa mitandao ya kijamii ambayo kwa sasa inatumika kuweka mambo sawa na hivyo ku-play nafasi ya wahariri panapokesana weledi miongoni mwa baadhi ya waandishi wetu ingawa ni ukweli pia mitandao nayo hutumika kupotosha ila uzuri ni kwamba siku zote ukweli ndio huibuka mshindi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom