Inawezekana Spika wa Bunge hajui sheria? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inawezekana Spika wa Bunge hajui sheria?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Dec 24, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Inauma kichwa kidogo. Inawezekana kweli mtu awe bosi wa mhimili lakini akawa hajui haki, wajibu na ukomo wake? Inaingia vipi akilini, eti, Spika wa Bunge, Anne Makinda, apitishe posho kwa wabunge wakati hilo lipo nje ya mamlaka ya bunge!

  Maslahi yote ya wabunge, kisheria huidhinishwa na rais. Inakuwaje wabunge waanze kufaidi posho za vikao shilingi 200,000 wakati mwenye mamlaka ya kupitisha hilo hajaamua. Inaonekana fedha zipo ndiyo maana zinatumika hata bila kufuata utaratibu.

  Spika wa Bunge anajua kwamba posho zote hulipwa baada ya rais kuidhinisha. Posho anazobebea bango, hazikuidhinishwa. Ugumu wa Rais Jakaya Kikwete kupitisha malipo hayo ni sawa na uthibitsho wa kuidhinisha masharti mapya ya kazi kwa wabunge.

  Hii ina maana kuwa suala la nyongeza ya posho linaingia moja kwa moja kwenye mashati ya kazi kwa wabunge. Masharti hayo hupitishwa na Ofisi ya Rais. Hivyo kitendo cha kuanza kulipa posho mpya bila masharti mapya ya kazi za wabunge ni kukiuka Sheria ya Utawala wa Bunge, kifungu cha 19.

  Tume ya Bunge inapaswa kuwajibika kwa kutumia vibaya mamlaka yake. Posho mpya ziidhinishwe leo na Rais Jakaya Kikwete au zikataliwe moja kwa moja, ni lazima zile zilizolipwa zirejeshwe mara moja kwani zimelipwa kinyume cha sheria ambazo ni wabunge wenyewe walitunga.

  Spika Makinda anapaswa kuheshimu sheria ambazo bunge limepitisha. Haiwezekani kiongozi mkubwa kama yeye, afanye makosa ya wazi namna hiyo. Mosi, hoja yake ya kuwajaza ‘manoti' wabunge haikubaliki, pili, ametekeleza kinyume cha sheria za nchi.

  Hata hivyo, JK naye anapaswa kulaumiwa kwenye suala hili. Tangu sakata la posho za wabunge lianze, hajawahi kutoa kauli inayoonesha mtazamo wake. Amekuwa akigusia tu bila kutoa ufafanuzi. Mathalan, aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Facebook:

  "Maslahi yote ya wabunge huidhinishwa na rais." Baada ya hapo, akaeleza kwamba yeye hajapitisha malipo ya posho. Wiki iliyopita, aliandika: "Hatuwezi kuvumilia kuona taasisi za umma zikitumia mamilioni ya fedha kwa ajili tu ya posho kwa watumishi wake.

  " Taasisi hizi kwa mfano Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) ambazo ni mali ya umma zinapaswa kutumia fedha hizi kwa ajili ya kukuza na kujiboresha zenyewe na sekta husika zaidi na zaidi na si vingineyo."

  Ukitazama maelezo ya JK, ni rahisi kutambua analenga wapi. Tatizo anasema hawezi kuvumilia taasisi za umma zikitumia mamilioni kwa ajili ya posho kwa watumishi wake, akatolea mfano Tanapa na kuacha kuzungumzia bunge ambako ndiko kwenye kipima joto.
  Ni vizuri wabunge wote wakatambua kuwa suala la posho halina mapokeo chanya kwa wananchi. Wengine wanafananisha hali ya wao

  kujilimbikizia maposho kuwa sawa na ujambazi wa mchana kweupe (daylight robbery).
  Baadhi ya wabunge ambao wametoa hoja ya kuongezewa posho, wamejenga hoja dhaifu. Huwezi kujadili kumuongezea fedha mtu

  mwenye uhakika wa kutengeneza zaidi ya shilingi milioni 10 kwa mwezi kwamba eti ana maisha magumu. Vipi watumishi wengine ambao wanafanya kazi kubwa lakini wanaminywa maslahi?

  Wengine wanadai posho eti kwa sababu wabunge huwa wanatoa michango ya harusi. Kwamba huwa wanaombwa kuchangia fedha nyingi kutokana na uheshimiwa wao. Eti, wanadai ubunge ni mzigo, kwani wananchi huwa wanadhani wana fedha nyingi.
  Swali wanalopaswa kuulizwa wabunge wanaolalamikia posho ni hili: "Kama uwakilishi ni mzigo, wamelazimishwa na nani? Na kama wakati

  anagombea ubunge hakufahamu kuwa kutumikia umma ni jukumu linalohitaji kujitoa muhanga, kwa nini basi asitue mzigo huo leo?
  Haihitaji kozi, inahitaji busara ya kawaida kutambua kuwa kama umepata nafasi ya uongozi lakini baadaye unagundua nafasi hiyo ni

  mzigo, kinachopaswa kufanywa siyo kudai au kulalamika posho hazitoshi, badala yake ni kuachia ngazi, kuwaachia wenye wito wafanye kazi wanayoipenda.

  Enyi nyote mnaolilia posho, si mnaona mamilioni hayo hayatoshi? Isiwe deni, achieni ngazi, muwapishe wenye wito wa kuwatumia wananchi.  Chanzo. Inawezekana Spika wa Bunge hajui sheria?
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,506
  Trophy Points: 280
  Mzizi Mkavu, madam speaker japo kitaaluma sii mwanasheria kama mtangulizi wake, ila sheria, taratibu na kanuni, anazijua fika, tatizo lake ni dogo tuu, "assumption" kuwa kwa vile huo uspika aliupata kwa kigezo cha jinsia yake, na unaofahamu udhaifu wa anayetakiwa kuidhinisha linapokuja suala la jinsia, then madam speaker baada ya kupeleka ombi mezani na kwa kuzingatia mazoea ya hakuna ombi toka bunge limewahi kujataliwa, then aka proceed ili kusave time akijua kibali kitatolewa!.

  Infact kilikuwa kitolewe kama wabunge wangejinyamazia na kujilia kwa ulani!

  Kitendo cha kupayuka, kimepelekea mkuu kusita kupitisha sio kwa sababu anawahurumia wafanyakazi wengine ambao mishahara yao haifiki hata hiyo 150,000 kwa mwezi!. Amesita kupitisha simply sababu siri imevuja!.

  Picha nzuri inayofuatia ni wabunge kuirejesha hiyo posho kwa kukatwa kidogo kidogo, then everything back to normal as if nothing happened!.

  Katika awamu ya nne, muwajibikaji ni Lowassa tuu!.
   
 3. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  ...labda bosi alisaini bila kujua alichosaini kama kawaida yake. Hana muda wa kusoma yaliondikwa kwenye 'document'.

  ...au ilikuwa danganya toto ili mswada wa katiba upitishwe kuwa sheria.

  ...labda....
   
 4. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Anajua sema alifanya kazi kama kauli ile "Kama ilivyo kawaida unaombwa kuchangia sh mil 50 kwenye account hiyo" ni kawaida tu
   
 5. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2011
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  With my few reservations abt EL...nakubaliana na Pasco km Lowassa angekuwa Rais asingekaa kimya hadi sasa ktk hili suala la posho
   
 6. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  sababu nchi inaendeshwa ndivyo sivyo kila mtu na lake.....huyu anasema vile mara yule vile na siku zinaenda mkuu haoni hilo
   
 7. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #7
  Dec 24, 2011
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Nyie tulieni tu mpaka kufikia October 2015 tutakuwa tumeona na kusikia mengi ila wasi wasi wangu ni huyu bi mkubwa kama atamaliza hizi mbio maana naona kama anahema sana na nijuavyo mimi 2014 to mid 2015 waasi ndani ya magamba wataongezeka iliwajitengenezee mazingira ya kurudi mjengoni maana wajanja wameshasoma nyakati kuwa siku hizi watu wanadeal na sifa za mtu binafsi na sio kama ilivyokuwa enzi za chama kimeshika hatamu ambapo kuna baadhi walidiriki kusema kuwa magamba hata yakisimamisha jiwe ilimradi likachorwa jembe na nyundo basi litashinda
   
 8. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #8
  Dec 24, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  uspika wa kupewa ndo faida zake hizo, anajiamulia kile anachoona kinafaa tu, na kwake kuwaongezea wabunge mishahara ni ili ajenge sifa kwao wamchague tena 2015, shubutuuuu! kwenye hii gutter politics asahau kuchaguliwa tena kuwa spika.
   
 9. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #9
  Dec 24, 2011
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kuna dots zina miss, lakini with time zitajulikana!
   
 10. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #10
  Dec 24, 2011
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,473
  Likes Received: 4,751
  Trophy Points: 280
  kitaaluma ni MWANASHERIA!!!!!!!!!????
   
 11. CHEMPO

  CHEMPO JF-Expert Member

  #11
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa serekali ya magamba hakuna la kushangaa hapo...jiulizeni ni lini walishakuwa sahihi? Huyu bi chau hana analojua zaidi ya mipasho,,,,,kweli hata mimi naweza kuwa rais saa yoyote ngoja nijiandae
   
 12. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #12
  Dec 24, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Alisomea wapi vile!
   
 13. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #13
  Dec 24, 2011
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Online!

   
 14. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #14
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  spika wa bunge la JMT ni kilaza!
   
 15. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #15
  Dec 24, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hii habari ya posho imetusaidia kuufahamu udhaifu wa huyu mama kama ni kweli.Haiwezekani spika mzima ulipe posho isiyoidhinishwa eti kwa matarajio mkuu angesaini tu!Spika hajui kwamba suala la pesa za umma ni sensitive sana?Kwa nini ajifanyie mambo kiholela kiasi hicho?Kweli ULEVI wa madaraka ni mbaya kuliko wa pombe!
   
 16. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #16
  Dec 24, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hata baba ndani ya nyumba ukimtokea house girl wako basi heshima ndani hamna, hakuna mwenye sauti ya mwisho, baba nae ugwaya kutoa uamuzi.
   
 17. k

  komredi ngosha JF-Expert Member

  #17
  Dec 24, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 381
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  du! Mifano mingine balaa
   
Loading...