Inawezekana serikali ikawatumia watanzania waishio ughaibuni kama mabalozi wa kutangaza utalii

Mouse3

JF-Expert Member
Oct 29, 2013
1,436
1,275
Ndugu zangu! bila shaka mtakuwa wazima wa afya njema! nimejaribu kutafakari kwa kina kuhusu uwezekano wa serikali hii ya awamu ya tano ikawatumia watanzania waishio ughaibuni kuisadia serikali kuitangaza Tanzania katika nyanja mbalimbali ikiwemo utalii kwa kuwapatia tu!!! angalau vitendea kazi kama Bendera ya Tanzania,Vipeperushi na zana ndogondogo tu ambazo gharama yake haiwezi kuwa kubwa na yakutisha! nasema hivyo kwasababu ni wazi kabisa watanzania hawa ndio wenye nafasi ya kukutana na halaiki ya raia wakigeni huko wanakoishi na hukutana na maswali mengi kupindukia ila majibu wanayotoa mara nyingi hayana nguvu sana kama wangekuwa hata wanavipeperushi na vitu kama hivyo! mfano wanafunzi wanaosoma ughaibuni,mmoja tu akipatiwa vifaa hivyo hakika sii chini ya watu mia tano kwenda juu watakuwa na ufahamu nini kizuri kinapatikana tanzania na kushawishi wageni kututembelea! Serikali au basi hata wizara ya maliasili na utalii ingieni mikataba na raia hao kwamba mtu akifanikisha kuleta hata wageni mia kwa mwaka atapata angalau basi % ngapi na mtengeneze mtandao utakao kuwa unapokea wageni hao kupitia wizara na ikibi kama wizara mfufue hata zile kampuni zenu za safari wageni hao wapitie huko!!
Ninaamini kwa kufanya hivyo ndani ya miaka mitatu sidhani kama mtakuwa na gharama za kutangaza utalii amabazo bado matunda yake ni kidogo mmno ukilinganisha na vivutio vilivyoko Tanzania.
Jamani ni kwania njema tu sio kwamba nawabania msisafiri kutangaza utalii kwa pesa ya serikali la hasha ni mtazamo tu!
 
Back
Top Bottom