Inawezekana serikali ikakopa dola 600M bila kushirikisha Baraza la Mawaziri mwenyekiti akiwa Rais?

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Huu ni mkopo mkubwa sana kwa nchi, je Baraza la mawaziri ambalo mwenyekiti wake ni Rais hawakujua yaliyomo ndani ya mkataba ikiwamo kulipwa kwa kampuni ya EGMA ya Kitilya?

Na kama walijua na kukubaliana na yaliyomo katika mkataba,shida inatokea wapi?

Ninavyojua wizara ya fedha inatakiwa kuandaa paper na kuipitisha ngazi kadhaa ikiwamo Baraza la mawaziri ili lipitishe na baada ya kupitisha ndipo mkopo hutolewa. Sasa wanaoshitakiwa kosa lao nini?

Kipindi hicho wajumbe wa Baraza la mawaziri chini ya Kikwete walikuwa akina nani na wanatuambiaje?
 
Mawaziri waliokuwa kwenye serikali ya jk wanatuambiaje?
 
Serkali ya CCM hakuna kitu hakiwezekani.Hata ikibidi kuvunja sheria watavunja tu.Wanatunga sheria leo kesho wanageuza,hiyo ndio TANZANIA ya leo tulipofikishwa.
 
Haukuwahi kusikia kuwa Mikataba mingine katika nchi hii ilikuwa inasainiwa guest huko ulaya! Kwahiyo, usione ajabu kuwa Mkataba huu ulipigwa juu kwa juu bila ya Baraza la Mawaziri na Rais kujua kinachoendelea!
 
Mawaziri waliokuwa kwenye serikali ya jk wanatuambiaje?
Ukikamatwa na trafic polisi kwa sababu ya mwendo kasi hata ukijitetea kuwa dereva mbele yako alkuwa pia kwenye mwendo kasi trafic atakujibu ni kweli lakini nimekukamata wewe. Hivyo hivyo hao walioshitakiwa kwa skendo hii wana nafasi ya kujitetea kwa kuwataja wahusika wengine na hakimu ataamua kuwakamata au la.
 
Watanzania tuliaminishwa kuwa fisadi ktk nchi hii ni lowassa tu.Hao mafisadi wengine wakina nani na wameletwa na nani toka wapi?
 
Ndio maana shtaka la utakatishaji wa fedha limefutwa na hayo mengine yataishia hewani
Kesi za wale wahindi wa EPA umezisikia tena?
Ni maigizo tuu
Hivi huyo Miss Tz Sinare si wa akina Sinare wale mawakili wa bei mbaya wa Tanesco,-Rex Attorneys?
Kama ni ndio jibu unalo hawawezi muachia mwanao aingie mkenge
 
Huu ni mkopo mkubwa sana kwa nchi,je Baraza la mawaziri ambalo mwenyekiti wake ni rais hawakujua yaliyomo ndani ya mkataba ikiwamo kulipwa kwa kampuni ya enigma ya kitilya? Na kama walijua na kukubaliana na yaliyomo katika mkataba,shida inatokea wapi? Ninavyojua wizara ya fedha inatakiwa kuandaa paper na kuipitisha ngazi kadhaa ikiwamo Baraza la mawaziri ili lipitishe,na baada ya kupitisha ndipo mkopo hutolewa,sasa wnaoshitakiwa kosa lao nini? Kipindi hicho wajumbe wa Baraza la mawaziri chini ya kikwete walikuwa akina nani NA wanatuambiaje?
Kwani jamaa si wamepelekwa mahakamani na serikali?
Maana hao wamedanganya serikali au wameingia mkataba kinyume cha sheria!
Subiri kesi isomwe utapata majibu, usiwe na haraka sana!
 
Watanzania tuliaminishwa kuwa fisadi ktk nchi hii ni lowassa tu.Hao mafisadi wengine wakina nani na wameletwa na nani toka wapi?

CHADEMA waje na hili waliweke wazi maana ufisadi wa lowasa ndo waliueneza watupe vitu tena am waiting
 
Kwa hiyo kama ni mkwe?! Alimtuma? Wewe hutumwa na wakwezo kuiba? Jiongeze, acha papara hapa jf siyo fb kwa kuuzia ulimbukeni wako.
Mtu wa 'kawaida' ataoaje kwa Lowasa, kwa mfano!?
Akimtafutia kazi yenye fursa ya kuiba (kama ni kweli kaiba) ni sawa na kumwambia iba.
 
Ndio maana shtaka la utakatishaji wa fedha limefutwa na hayo mengine yataishia hewani
Kesi za wale wahindi wa EPA umezisikia tena?
Ni maigizo tuu
Hivi huyo Miss Tz Sinare si wa akina Sinare wale mawakili wa bei mbaya wa Tanesco,-Rex Attorneys?
Kama ni ndio jibu unalo hawawezi muachia mwanao aingie mkenge

Mkuu kuna mtu nilishabishana nae humu ndani akabisha khs Hilo suala la Rex na mtoto wao
 
Mwanasheria Mkuu wa serikali ni mjumbe wa baraza la mawaziri,na anahusishwa katika hatua za awali za kuandaa CABINET PAPER,na pia anahudhuria katika vikao vya Baraza la mawaziri kama mshauri wa kisheria,je hakushauri serikali kwamba kinachofanyika kinakiuka sheria? Kuwalipa akina kitilya? Je kama alishauri kwamba mkataba hauna matatizo,inakuwaje sasa ofisi yake tena inaandaa mashtaka kwenye jambo ambalo yeye kama mwanasheria Mkuu alisema halina tatizo?kama alishauri akakataliwa,alichukua hatua gani? Pasco@manyerere jackton,Mzee Mwanakijiji
 
Huu ni mkopo mkubwa sana kwa nchi, je Baraza la mawaziri ambalo mwenyekiti wake ni Rais hawakujua yaliyomo ndani ya mkataba ikiwamo kulipwa kwa kampuni ya EGMA ya Kitilya?

Kipindi hicho wajumbe wa Baraza la mawaziri chini ya Kikwete walikuwa akina nani na wanatuambiaje?
Mkuu Ipara, maadam hili ni swali, then subiria hapa hapo, muda kidogo tuu, sasa hivi hao waliokuwa wajumbe wa baraza la mawaziri enzi za JK, watakusikia na watajitokeza, ili uwajue ni kina nani, kisha watakuja hapa, humu ndani ya jf, na kutuambia kilichokuwa kinafanyika ndani ya vikao vya baraza la mawaziri!.

Wee subiri tuu!.

Pasco
 
Back
Top Bottom