Inawezekana mwanamke ukawapenda wanaume wawili kwa pamoja?

Royal Warrior

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
1,166
2,117
Habari zenu,

Naomba kuwauliza wadada hili swali mnipe uzoefu wenu.

Baada ya kuachana na mpenzi wangu wiki iliyopita, nikaamua kumtafuta ex wangu ambae tulipendana sana kipindi tupo chuo. (Tulikuja tengana baada ya kumaliza chuo, yeye akarudi mwanza, mimi nilibaki dar, slow slow mapenzi yakakata flani hivi, kila mmoja aka move on, hatukuachana kwa ugomvi au uhasama).

So tukawa kama marafiki fulani hivi, yeye alipata mpenzi mwingine, na mimi pia nikapata mpenzi mwingine, maisha yakawa yanaendelea. Tulikua tunawasiliana japo sio mara kwa mara.

Sasa jana nikaamua kumwambia kuwa mimi na mpenzi wangu tumeachana, nkamwambia ex wangu kuwa nakuhitaji turudiane, bado nina feelings na wewe.

Akaniambia kuwa yeye alinipenda na bado ananipenda lakini huyo mpenzi wake aliye kuwa nae huko mwanza nae anampenda pia. Nikamuuliza mimi na huyo mpenzi wake wa mwanza nani anampenda zaidi? Akasema kuwa anatupenda sote sawasawa.

Sasa tangia jana akili inawaza tu, hivi hichi kitu kinawezekana kweli?
 
Kwa kutumia usemi hakuna linaloshindikana chini ya jua...Naona wanaweza Tena Hawa wasasa walivyo mwendokasi namuachia malaika izraili amalizane nao!
 
Haa😀😁😂
Atajipa Jaka Moyo Bure Huyu Jamaa
Yaani Mmeachana Halafu Unajirudisha
Hujitakii Mema!!! Tunangoja Mrejesho Wako
 
unaweza ukapendwa kama brother au rafiki

Relax unapendwa bob
 
Laiti tungekuwa tunaiona kesho
Yaani dunia yote hii unarudi kwa ex ambae ana mtu wake tayari
Ama kweli hatujua kifo kinakujaje


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
😂😂😂😂😂😂😂
Wanawake we piga tu, kupenda kupendana yatakujaga tu.
 
Back
Top Bottom