Saint H.Jr
Member
- Aug 22, 2013
- 47
- 40
Wadau,
Nimeisoma kwa umakini mkubwa sana thread ya mdau mmoja aliyekata shauri na kuamua kwenda kupima HIV!
Kiukweli kabisa toka katika uvungu wa moyo wangu nampongeza sana na Mwenyezi Mungu amuokoe huyu ndugu. Lakini kati ya wachangiaji waliosimama kidedea kuchangia thread hii, mchangiaji mmoja nimemnukuu akisema, "hukujua kuwa kupata UKIMWI ni kazi ngumu sana.."
Na kwa bahati mbaya alipoombwa kutoa elimu na uzoefu wake na baadhi ya wadau, hakuonekana tena! Usemi huu umeibua tafakari na tafakuri nyingi katika halmashauri yangu ya kichwa, nikirejea na siku za mgongoni nikiwa darasani mwalimu pia aliwahi kusema maneno sawia na ya mchangiaji wa leo na toka ya hapo, swali hili limetoka katika tawala za kichwa changu kwamba, "Je, inawezekana mtu akalala (siyo kulala huku kwa kawaida, tafsida imezingatiwa) na mtu mwenye UKIMWI tena bila condom na asipate UKIMWI?".
Nisaidieni wadau.
Nawasilisha.
======

Virus vinaishi kwenye damu. Watu wamejaribu kupambanua njia tofauti tofauti za maambukzi. Ila njia ni moja tu. Kukiwa na muingiliano wa damu kati ya muathirika na asiye athirika.
Kwa wanawake ni rahisi sana kuambukizwa kutokana na jinsi maumbile yao yalivyo. Katika uke wa mwanamke kuna chembe chembe nyeupe za damu nyingi hususni wa kati wa tendo husika. Na tunajua HIV huwa vinaishi ndani ya WBC.
Ishu za manii ama orgasm fluids zinapotoka huwa hazina uhalisia wa moja kwa moja wa kuwa na VVU