Je, inawezekana mtu akalala na mwenye UKIMWI tena peku na asipate UKIMWI?

jaman msaada please imepita miezi sita toka niachane kimapenz na mdada mmoja ambaye alikua mtu wang sabab aliniomba tuachane ili apate wa kumuoa kweli nilifanya hivo Mung si athuman yule bint akapata mchumba baada ya mwez tu kuachana na alikua ananiambia hawajawah sex na mtu wake mpaka ndoa mara kwa mara tulipoachana alikuwa anaenda kupima peke yake analeta majibu . negative cha ajabu mwez huu wameenda kupima na mmewe mtarajiwa kajikuta ni positve mme wake negative na bado hawajasex aliponiambia nilistuka nikambana akasema mara ya 'm wisho kusex amesex na mimi / mwaka ja na October ilibid nikapime haraka mda huo nikakutwa negative nikamletea vipimo vyang NIMESHINDWA NIMSAIDIAJE ila mchumba wake anaimani nae sana wadau nipen hatua za kumsaidia inauma sana
Your case is very very interesting..

I wait for it to be continued
 
Wewe utakuwa umeoteshwa kulizungumzia tunda hili humu.Haya ndiyo mambo ambayo ninayaongelea mara nyingi kwamba elimu ambayo tunapewa nyumbani na mashuleni ni irrelevant,yaani haikidhi haja/mazingira tunayoishi,yaani haina maana.
Ukifuatilia kwa undani kwa nini tuliambiwa hivyo lazima utagundua kwamba kulikuwa na mkono wa mtu hapo.Wazazi wetu wamepigwa changa la macho kwa faida ya watu wachache.Sasa kwa nini nasema umeoteshwa;

Jibu;
Limao halikaushi damu,bali limao lina faida lukuki mwilini ambapo kama mtu,na hasa watoto,watatumia vizuri tunda hili basi kwa mtu/mtoto huyo kuumwa kwake ni hadithi.Hata leo ukianza kulitumia tunda hili ninakuhakikishia utarudi hapa kutoa ushuhuda.Unaweza ku google mwenyewe uone faida zake;

1.Huimarisha kinga ya mwili-vitamin C
2.Husafisha utumbo mpana,huzuia constipation-Dietary Fiber
3.Hutibu malaria,kipindupindu-Antibacteria
4.Huweka sawa pH ya damu-Limao hufanya damu iwe alkaline.
5.Husaidia mmeng'enyo wa chakula-Husaidia/huchochea kuzalishwa kwa nyongo
6.Huzuia magonjwa ya moyo na presha ya juu ya damu-pH balance,calcium,magnesium na potassium
7.Hutuliza homa na mafua
8.Huondoa sumu mwilini-alkaline blood/pH balance
9.Hutibu arthritis na Rheumatism-Husafisha damu na huondoa uric acid
10.Huondoa mikunjo kwenye ngozi
11.Huondoa maumivu ya kuumwa na nyuki,sunburn
12.Huboresha afya ya macho
13.Huzuia kuvuja kwa damu ndani ya mwili au puani
14.Huondoa makovu kwenye ngozi

Na mengine mengi madogomadogo.

-Kisukari(Type 1 diabetes) kwa heri(angalia;4,8)
-Cancer ya utumbo mpana kwa heri(angalia; 2)
-Cancer yoyote kwa heri kama utakuwa na tabia ya kunywa maji ya limao(angalia;2,4,8)
-Kipindupindu kwa heri kama una tabia ya kunywa maji ya lima kila asubuhi(angalia;1,3)
-Soko la dawa za malaria litashuka kama watu watakuwa wanatumia maji ya limao(angalia;1,3)
-Kwa watu wenye maumivu ya magoti huweza kupata nafuu kwa kunywa maji ya limao tu na kusahau dawa za hospitalini(angalia;9)
-Kwa kina dada warembo;kwa kutumia limao tu wataepukana na vipodozi vyenye sumu ili kungarisha ngozi zao(angalia;10,14)

Yaani usiende mbali sana,chukulia cancer,kisukari na malaria pekee.Kama watu watapenda kutumia maji ya limao mara kwa mara kwenye maisha yao ina maana soko la dawa za cancer,kisukari na malaria kwisha habari yake.Limao ni tunda tulilolizoea sana lakini hatujui faida zake,tumelidharau kwa sababu ya mazoea.
Na hivi ndivyo baadhi ya vitu ambavyo viko kwenye mlolongo wa mambo ninayotaka wana JF wenzangu wajue.Ni muhimu sana hili tunda,dharau tu na mazoea ndivyo vinatuathiri.

Kwa mfano;Mtu kama anaumwa ugonjwa wa joints(magoti yanauma/yamevimba nk),ukimpa maji ya limao kila asubuhi ni tiba tosha.Ukitaka kukata mzizi wa fitina unaweza kujumlisha tiba.Limao+mafuta ya nazi/olive oil+tumeric(bizari)+tangawizi+celery,hapo utakuwa umemaliza kabisa.Lakini watu wanahangaika kwa kukosa uelewa.
Malaria,cancer,kisukari na mengineyo vivyohivyo.Hapo ndipo utakapoona kwamba vitu vingi tunavyovijua sasa tumebebeshwa/irrelevant.Waliotudanganya wasingependa tujue ukweli huu kwa kuwa hakutakuwa na soko tena.Kibaya zaidi tiba kama hizi hawawezi kuzi patent.
Incredible
Austonishing
Flabbergasting
Outstanding.
....juice ya limao kwanzia ni rafiki yangu badala ya pombe.
 
mi ninavyofaham ni kwamba virus wanaishi kwenye blood plasma/umajimaji wa damu, so kushiriki ngono na muathirika kuna probability kubwa ya kuweza kuambukizwa, kwenye hii michezo michubuko inaweza kuwepo au hata katikamate kamaunayekiss naye ana mchubuko basi wajomba watapitia huko huko
 
mi ninavyofaham ni kwamba virus wanaishi kwenye blood plasma/umajimaji wa damu, so kushiriki ngono na muathirika kuna probability kubwa ya kuweza kuambukizwa, kwenye hii michezo michubuko inaweza kuwepo au hata katikamate kamaunayekiss naye ana mchubuko basi wajomba watapitia huko huko
Nakuomba ndugu yangu inafaa zaidi ungeanza kuusoma huu uzi tokea mwanzo.
 
Hii kitu inaitwa HIV mimi hua naona kama ni laana na si ugonjwa,unachanganya sana huu,kuna watu mke na mume m1 anao mwingine hana,kuna watu wengine wamepima wakakutwa nao lakini mpaka hapa wana miaka zaidi ya 20 wanaishi na wanakufa wenye malalia,huu ni ugonjwa kweli huu!!!!???
 
Kinachoniacha hoi, yaani dawa zake zinaenda kumteketeza mdudu ndani ya seli, hapo unaponaje..mdudu mwenyewe hajulikani kiini macho...na upimaji wake uko tofauti na ugonjwa wowote....cha msingi ni kuwa na mazoea ya kunywa maji ya kutosha, mazoezi na kupumzisha mwili wako....utosikia ilo lidubwana lakufoji....
 
Kinachoniacha hoi, yaani dawa zake zinaenda kumteketeza mdudu ndani ya seli, hapo unaponaje..mdudu mwenyewe hajulikani kiini macho...na upimaji wake uko tofauti na ugonjwa wowote....cha msingi ni kuwa na mazoea ya kunywa maji ya kutosha, mazoezi na kupumzisha mwili wako....utosikia ilo lidubwana lakufoji....
ARV haziui virusi (cidal) bali huzuia kuongezeka kwao (static)

Kinga yako ya mwili ndio huviua
 
Mkuu,vipi kuhusu mbadilishano wa manii,maana si wote mtafika kileleni kwa maana ya wote kutoa semen
Mkuu nadhani sina uelewa wa kukujibu hapo, nadhani wachangiaji wengine wataweza kujibu.
Manii haziusiani na ukimwi kwa sababu mwanaume huwa anatoa hvyo virusi vya ukimwi haviwezi kupita kwenye bomba la mkojo(urethira)
Pia virusi vya ukimwi haviishi kwenye manii
 
Baadhi ya Madhara ya Dawa za ARV.png


Picha hii inaonyesha mabadiliko katika kucha yanayoambatana na matumizi ya dawa za kupunguza makali ya Ukimwi.
 
kuna uhusiano kati ya blood transfusion na kuambukizana HIV, yaani anayeweza kukuambukiza ni yule ambaye anaweza kukuongezea damu.
mfano: universal recipient ndio anaweza kuambukizwa hiv na kila mtu
 
MADHARA YATOKANAYO NA ARVS NCHINI YATAFUTIWE UFUMBUZI WA HARAKA


MADHARA yatokanayo na dawa za ARVs kwa baadhi ya watumiaji hapa nchini yanahitaji ufumbuzi wa haraka ili kuweza kuondokana na tatizo hilo.


Hivi karibuni, vyombo vya habari vimeripoti tukio la kusikitisha lilitokea mkoa wa Mtwara kwamba kuna mwanaume anayeishi na virusi vya UKIMWI amebadilika maumbile yake na kuota matiti kama mwanamke katika kifua chake baada ya kuanza kutumia dawa za kupunguza makali ya UKIMWI (ARV).


Alipotoa taarifa kwa daktari aliambiwa hali hiyo ni ya kawaida kwa watu ambao wanatumia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo kwa muda mrefu.


Sikika imeguswa na matukio yanayotokana na utumiaji wa dawa hizo na kufuatilia suala hilo kwa ukaribu zaidi. Pamoja na baadhi ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI (WAVIU), kutoa taarifa ya kuwa dawa wanazotumia zinawaletea madhara makubwa, bado baadhi wa watoa huduma husika wamekuwa hawachukui hatua yoyote juu ya ubadilishaji wa dawa hizo kwa WAVIU.


Kutokana na taarifa kutoka kwa baadhi ya watumiaji wa dawa hizo wamepatwa na madhara mengi ambayo ni uzito kupungua, mwili kuchoka, miguu na mikono kufa ganzi, mapele, kucha kubadilika rangi kuwa nyeusi na pia baadhi yao kubadilika kimaumbile pindi tu wanapoanza kutumia dawa hizo.


Utaratibu uliopo ni kwamba mtumia dawa hizo anapoona athari zinaanza kutokea anapaswa kutoa taarifa kwa muuguzi wake ili aweze kubadilishiwa dawa nyingine lakini imegundulika kuwa mgonjwa anapotoa taarifa juu ya madhara hayo humchukua zaidi ya miezi sita kabla ya kubadilishiwa dawa na wakati mwingine huambiwa kuwa hali hiyo ni ya kawaida na itaisha.


Sikika pia imegundua kuwa baadhi ya vituo vya kutolea huduma hizo havina mashine za CD4. Kifaa hiki ni muhimu kwa ajili ya kujua maendeleo ya mgonjwa na kutoa ushauri katika kinga za mwili na pia kuendelea na aina ya dawa wanazotumia. Tatizo hili limeendelea kuwa sugu hasa katika maeneno ya vijijini ambapo WAVIU wanalazimika kwenda mwendo mrefu sana kwa ajili ya vipimo vya hivyo. Suala hili limeonekana wazi katika wilaya za Kondoa na Mpwapwa ambapo baadhi ya vituo vya afya havina mashine za CD4.


Vituo hivyo ni Kisese, Hamai, Songolo, Busi na Kwa Mtoro vinavyopatikana wilayani Kondoa na vituo vya afya vya Kibakwe, Rudi, Mima na Pwaga vilivyopo wilaya ya Mpwapwa.Ukosekanaji wa kifaa hiki kwa kiasi kikubwa unachangia mgonjwa kuendelea kutumia aina ya dawa moja ambayo huenda haimfai tena kulingana na CD4 zake kutojua kama zimepanda au zimeshuka.


Sikika inapendekeza kuwa hatua kali zichukuliwe kwa watoa huduma ambao hawafuati utaratibu wa maadili ya kazi zao. Wizara husika pia iwajibike katika kuwasaidia wale ambao wameathirika kutokana na madhara ya utumiaji wa dawa hizo. Mfumo wa sasa wa kusikiliza matatizo ya watumia huduma uimarishwe ili kupunguza athari kubwa zinazotokana na madhara ya kutumia madawa hayo kutokana na wahudumu wengi kutumia lugha chafu.


Pia serikali inapaswa kuweka mashine za CD4 kwenye vituo ambavyo havina na kuzifanyia matengenezo haraka pale zinapoharibika ili zitumike kuwapima wagonjwa maendeleo ya kinga zao za mwili kabla hawajaanza matumizi ya dawa hizo ili kuondokana na tatizo hilo kubwa. chanzo.MICHUZI BLOG: Madhara yatokanayo na ARVs nchini yatafutiwe ufumbuzi wa haraka


 
Back
Top Bottom