Inawezekana mfumuko wa bei Tanzania ni wa kutisha, idara ya Takwimu wametupiga chenga ya mwili kwa takwimu za Januari, ila nimewagundua

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
4,064
2,000
Kuna mabadiliko makubwa sana ya kitakwimu nimeyagundua kwenye report ya mfumuko wa bei ya mwezi January, ambayo inasema kwamba mfumuko wa bei kwa miezi 12 iliyopita mpaka mwisho wa mwezi January 2021 ni asilimia 3.5 tu!.

Niliangalia hii report ilivotoka wiki iliyopita, lakini sikuelewa inakuwaje mfumuko wa bei umekuwa kwa kiasi kidogo sana (kwa asilimia 0.3% kutoka data za mwezi December 2020 ambazo zinasema mfumuko ulikuwa ni 3.2%) wakati hali ilivo huku mtaani ni kwamba tumeshuhudia ongezeko kubwa sana la bidhaa muhimu hususani bidhaa za chakula ambazo kimsingi zinazochukua sehemu kubwa wakati wa ukadiriaji wa mfumuko wa bei.

Wakati najiuliza maswali ya nini kimetokea, leo nikabahatika tena kupitia takwimu ya mfumuko wa bei kwa mwezi January na kwa bahati macho yakatua kwenye ‘Basket of commodities’ ambayo wanasema imeongezeka kutoka bidhaa 278 walizokuwa wakitumia mpaka bidhaa na huduma 383 ikiwa ni ongezeko la bidhaa 105 ndani ya kipindi cha mwezi mmoja. Mbali na hiyo wameongeza pia idadi ya mikoa kutoka 25 mpaka 26 wakijumuisha na mkoa wa Songwe.

nbs.png


Jan-18
Jan-20
Feb-20
Mar-20
Apr-20
May-20
Jun-20
Jul-20
Aug-20
Sep-20
Oct-20
Nov-20
Dec-20
Jan-21
Basket of commodities (goods and services)
278
278​
278​
278​
278​
278​
278​
278​
278​
278​
278​
278​
278​
383
Number of regions covered
25
25​
25​
25​
25​
25​
25​
25​
25​
25​
25​
25​
25​
26
Inflation last 12 months in %
3.7​
3.7​
3.4​
3.3​
3.2​
3.2​
3.3​
3.3​
3.1​
3.1​
3.0​
3.2​
3.5​

Mabadiliko haya yanatuambia nini?

>> Kuongeza idadi ya bidhaa kwenye kapu kutoka 278 mpaka 383 na hapo hapo kuongeza idadi ya mikoa kutoka 25 mpaka 26, maana yake ni kwamba sampuli ya takwimu ya mfumuko wa bei imeongezeka, na impact yake ni kwamba ime haribu kabisa uhalisia wa takwimu ya mfumuko wa bei ambao umekuwepo kwa mda mrefu. Kwa sababu ukiongeza sampuli kwa lugha ya kitakwimu maana yake ni kwamba unapunguza makali ya namba nikiwa na maana ya kwamba kama wastani wako ulikuwa ni asilimia 6%, unavoongeza sampuli nyingine, inapelekea kushusha wastani wa namba kutoka 6% mpaka hata 3.5%. Lengo haswa ikiwa ni kuonesha kwamba mfumuko wa bei haupo wa kutisha ila ki uhalisia ni kwamba, kama wangetumia parameters walizotumia mwezi wa 12 mwaka jana na ambazo zimekuwepo kwa mda mrefu, lazima tungeona utofauti mkubwa sana kwenye data za mfumuko wa bei kwa mwezi January ambao naamini kabisa utakuwa upo hata kwa Zaidi ya asilimia 5% mpaka 6%, tofauti na hii asilimia 3.5% waliyoitoa. ………………………… kwa ambao bado hawajanielewa kuhusu madhara ya kuongezeka kwa bidhaa kwenye kapu na idadi ya mikoa…… jaribu kufikiria umepika mchuzi mtamu sana wa Samaki halafu ukazidisha chumvi kiasi cha mboga kushindwa kulika, so unaamua kuongeza maji ya kutosha ili upunguze makali ya chumvi, mwisho wa siku chumvi inakuwa kawaida na inaweza kulika lakini mchuzi umekuwa chururu na ubora wote umepotea….. Ndo maana ya kilichofanyika hicho.
Kuna kitu kingine pia kimebadilika ambacho kimenifanya niongeze mashaka na hizi takwimu kwamba kuna ukweli fulani ambao unafichwa kwamba yawezekana mfumuko wa bei unazidi kuwa mkali siku hadi siku. Na kikubwa kinachotia mashaka ni mabadiliko haya makubwa yaliyotokea kwenye calculation nzima ya mfumuko wa bei tena ndani ya kipindi cha mwezi mmoja tu.

>> Mbali na kuongeza sampuli ya data kwa kuongeza idadi ya bidhaa kwenye kapu na idadi ya mikoa, kumetokea pia madadiliko makubwa kwenye ‘weights’ za makundi ya bidhaa kwenye kapu. Na kitakwimu unavobadili ‘Weights’ inapelekea kuathiri pia output ya namba unazozipata.


Angalia kwa makini tofauti iliyopo kwenye weights za mwezi January 2021 na zile za kuanzia January 2018 mpaka December 2020 ambazo zipo sawa.

Weights in %
S/nItems for January 2018 and December 2020
Jan-18
Dec-20
Jan-21
Change Dec-20 to Jan-21
1​
Food and Non-Alcoholic Beverages
38.5​
38.5​
28.2​
-10.3​
2​
Alcoholic and Tobacco
3.7​
3.7​
1.9​
-1.8​
3​
Clothing and Footwear
8.3​
8.3​
10.8​
2.5​
4​
Housing, Water, Electricity, Gas, and Other Fuel
11.6​
11.6​
15.1​
3.5​
5​
Furnishing, Housing Equipment and Routine Maintenance of the House
6.3​
6.3​
7.9​
1.6​
6​
Health
2.9​
2.9​
2.5​
-0.4​
7​
Transport
12.5​
12.5​
14.1​
1.6​
8​
Information and Communication
5.6​
5.6​
5.4​
-0.2​
9​
Recreation and Culture
1.6​
1.6​
1.6​
0.0​
10​
Education
1.5​
1.5​
2.0​
0.5​
11​
Restaurants and hotels
4.2​
4.2​
6.6​
2.4​
12​
Miscellaneous goods and services
3.1​
3.1​
2.1​
-1.0​
13​
Insurance and financial services - Added for January 2021 Indexn/an/a
2.1​
2.1​
Total weight
99.8
99.8
98.2
Key weight movements

 • Reduced weight on food and Non-Alcoholic by 10.3%
 • Increase weight on Clothing and Foot wear by 2.5%
 • Increase weight on Housing, Water, Electricity, Gas, and Other Fuel by 3.5%
 • Increase weight on Transport by 1.6%
 • Increase weight on restaurant and hotels by 2.4%
 • Increase weight on furnishing, Housing Equipment by 1.6%


Tafsiri ya kubadilisha uzito kwenye kapu (Implication of weight changes)

 • Wamepunguza weight ya basket ya chakula na vinywaji (food and non-alcoholic beverages) kutoka 38.5 mpaka 28.2, madhara ya kupunguza weight kwenye kapu la chakula na vinywaji ni kwamba, inapunguza impact kwenye mahesabu ya mfumuko wa bei inapotokea bei za bidhaa za chakula kwa mfano kama ilivo mafuta ya kupika yalivopanda bei kwa sasa hivi, inakuwa ni ngumu kuona mfumuko wa bei unapanda kwa sababu weight ya bidhaa za chakula imeshushwa. Kwa kufanya hivi pekee, wameondoa uhalisia kabisa wa consumption pattern ya watanzania, kwa sababu, hata kimahesabu ya kawaida, kwa mtanzania wa kawaida, anatumia karibu Zaidi ya asilimia 40% mpaka 45% ya kipato chake kwenye kununua chakula na vinywaji. Sasa unavoshusha weight ya chakula kutoka 38.5% mpaka 28.2% maana yake ni kwamba unaona kabisa kwamba, takwimu za mfumuko wa bei zitapoteza uwezo wa kuakisi gharama za maisha ya raia waliowengi wa kipato cha chini na cha kati.
 • Wameongeza weight au uzito na umuhimu kwenye makundi ya bidhaa ambazo bei zimekua hazina mabadiliko kwa mda mrefu kwa sababu ya mwenendo mzima wa uchumi, hususani kwenye sekta ya malazi hoteli na migahawa, shule, na mavazi ambazo weight imeongezeka kwa kiasi kikubwa.
 • Maana ya kupunguza uzito kwa makundi ya bidhaa za chakula na vinywaji ambazo ndizo zinazonunuliwa kwa wingi na wananchi na ambazo pia bei zimekuwa zipo volatile sana na kuamua kuongeza weight kwenye makundi ya bidhaa ambazo bei zake zipo stagnant na hazihitajiki sana sana na raia kuliko vyakula, ni kwamba inapelekea pia kupunguza mfumuko wa bei ki takwimu. (It’s a highest professional manipulation ambayo naweza kusema imefanyika, na mbaya Zaidi hakuna ufafanuzi wowote umetolewa.)


Ombi kwa Idara ya taifa ya takwimu.

 • Watueleza na watueleweshe sababu haswa zilizopelekea mabadiliko yote waliyofanya ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kwenye mahesabu yao ya makadirio ya mfumuko wa bei kwa mwezi January ambayo yalikuwa na mabadiliko yafuatayo 1) Kuongeza kapu la bidhaa kutoka bidhaa 278 mpaka bidhaa 383, 2) Ni kwanini waongeze idadi ya mikoa sasa, kutoka 25 mpaka 26, na 3) Ni kwanini wameamua kufanya mabadiliko makubwa ya weight kwenye bidhaa za vyakula ambayo kimantiki imeharibu kabisa uhalisia wa expenditure pattern ya mtanzania wa kipato cha chini na kati.
 • Watupe taarifa sahihi ya mfumuko wa bei kwa mwezi January kwa kutumia parameters ambazo zimakuwa zikitumika hapo mwanzo.
 • Wasijaribu tena kutuficha, maana watanzania tupo makini na tunafuatilia kwa karibu nchi inavokwenda, watoke wazi na watueleze kilichotokea, kama mfumuko wa bei upo 6% watoke na watueleza ukweli. Namba huwa hazidanganyi, wakijaribu ku manipulate data kama wanavojaribu kufanya, tutaona tu impact kwenye variable nyingine za kiuchumi. Watatuficha mpaka lini?


Wasalaam,

N. Mushi

Mtetezi wa wanyonge
 

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
4,064
2,000
Nimekusoma na kukuelewa. Nasubiri waje watupe majibu ya hizo mambo ulizowaachia.
Sidhani kama watatoka kujibu.. maana yake ni kwamba kama wakitumia approach ya mara ya kwanza ina maana mfumuko wa bei wa Tanzania kwa sasa upo juu ya asilimia zaidi ya 5.5%.. ndo mana wamefanya haya mabadiliko ili kushusha mfumuko kwa kucheza na namba
 

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
4,064
2,000
Mtaalamu umeelezea kitaalamu sana kiasi kwamba sina uhakika kama sisi wananchi wa kawaida na wale wawakilishi wetu pale Idodomya tumekuelewa.
Inahitaji kufuatilia sana .. na kuchimba ndani kwenye data.. mimi mwenyewe mara ya kwanza siku notice kilichotokea kwenye hizi data... Leo ndo nimeziangalia tena nikapata wazo la kuingia kwenye basket na weight na ndo nikakuta wamefanya marination za ajabu!!
 

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
4,064
2,000
Kuna watu hamdanganyiki kirahisi...sisi wengine ni watazamaji tu.
Walitoa hizi takwimu wiki iliyopita, lakini mwenyewe nilijaa.. nikiamini hakuna chochote.. leo nimeiangalia kwa mara ya pili kwa sababu nilikuwa najiuliza hii inflation inakuwaje stable na hivi karibuni vitu vimepanda kiholela ... wanatuchezea akili
 

wa kupuliza

JF-Expert Member
Jun 15, 2012
4,514
2,000
Hapo Mwisho umemaliza vizuri, namba huwa hazidanganyi kuna siku ukweli utajulikana tu, mathalani hakuna anayekaa madarakani milele, kuna Mamlaka siku za usoni itatuweka wazi ya utawala huu, Kama ambavyo ya awamu hii ilivyoweka wazi ya awamu iliyopita

Na muda hao atakua anapigwa madongo ya usoni na cha kufanya hana,atakua nae anasemwa ukigeuka hivi deal,ukienda huku deal...
 

Granite

JF-Expert Member
Jul 6, 2016
265
1,000
Na muda hao atakua anapigwa madongo ya usoni na cha kufanya hana,atakua nae anasemwa ukigeuka hivi deal,ukienda huku deal...
Ndo ambavyo huwa inakuwa ndo maana mzee makamba aliwahi kutoa ushauri wa kuwa na akiba ya maneno, Maisha ya Mwanadamu ni mzunguko tu unaenda wee unazunguka afu unarudi ulipoanzia
 

Mzee23

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
1,227
2,000
Asante kwa darasa, nimejikuta natamani kujua kulikoni vyakula na vinywaji vimepunguzwa "weight" natamani watoke hadharani watangaze kuwa mwaka huu wana KIKOKOTOO KIPYA Cha mfumuko wa bei
 

ikindo

Senior Member
Nov 29, 2011
104
225
Na muda hao atakua anapigwa madongo ya usoni na cha kufanya hana,atakua nae anasemwa ukigeuka hivi deal,ukienda huku deal...
Kwani hivi hayo matangazo ya mfumuko wa bei yanamsaada gani kwa sisi wanyonge? Maana mimi hua nayaonaga tu mara imepanda mara imeshuka, wataalamu muliopo hapa naomba mutuelimishe na sisi wanyonge ili tuelewe mnaposema wanapika data ina madhara gani kwetu hata wakipika.
 

Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
3,510
2,000
Market Basket inabadilika kila mwaka kwenye kupima inflation ndio utamaduni huo.

Pili suppose kweli inflation ni kubwa zaidi ya serikari inavyotangaza, iwapo level za supply and demand ni zilezile maana yake kuna hela nyingi kwenye mzunguko wa fedha.

Sera unazohitaji ni more taxation kwenye bidhaa zilizopanda sana ili watu wapunguze matumizi au kuongeza interest za mabenki ili watu wapunguze kukopa, kuzalisha na kutumia.

Ata pale serikali isipoingilia maswala ya interest ili watu wasikope bado kama inflation is uncontrollable una halalisha lenders kutokupunguza interest za mikopo kwa madai ya kwamba thamani ya fedha sio stable so they have to consider Net Present Value ya miaka ijayo mkopaji anapolipa. Swala ambalo linachangia interest za mikopo zibaki 15-20% na kufanya bidhaa zinazo zalishwa Tanzania kuwa na bei kubwa sikoni kutokana na gharama za uzalishaji.

Consider poor purchasing power ya watanzania ndio maana watu wana import hayo ndio matatizo mnayolilia serikali ikichukua hatua, kama mtoto alielia mbwa mwitu, sio kila kitu kupinga tu.
 

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
4,064
2,000
Asante kwa darasa, nimejikuta natamani kujua kulikoni vyakula na vinywaji vimepunguzwa "weight" natamani watoke hadharani watangaze kuwa mwaka huu wana KIKOKOTOO KIPYA Cha mfumuko wa bei
Wameona food inflation inawaumbua.. na vile weight yake ni kubwa impact yake pia kwenye inflation ni kubwa.. kwa hiyo itakuwa wamepunguza weight yake ili kuhakikisha inflation hairuki kwenda popote
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom