Uchaguzi 2020 Inawezekana kuwa asilimia 50 ya wabunge wa mkoa wa Mara watatoka upinzani

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
1,554
2,000
Jinsi kampeni zinavyoendelea mpaka sasa ninaamini kuwa asilimia 50 ya Wabunge wote wanaotoka Mkoa wa Mara watatoka upinzani. Nianze na Tarime Mjini, Rorya, Bunda Mjini na Tarime vijijini hali siyo shwari kwa CCM. Tujiulize hapa ni nani wa kulaumiwa?. Mimi ninatoa lawama kwa uongozi wa Wilaya na Mkoa kwa mapendekezo usio na tija jinsi walivyotoa alama kwa watia nia.

Mfano Bunda Mjini chaguo la wananchi alikuwa ni Mwanza Huduma lakini wakamleta mtu tofauti na Mwanza Huduma. Tarime Mjini chaguo la wananchi ni Kangoye lakini cha kushangaza wakamleta mtu tofauti na Kangoye. Rorya chaguo la wananchi alikuwa ni Olwero lakini cha kushangaza wakamleta mtu tofauti mbali ni chaguo la wananchi. Katika Jimbo la Serengeti Dr. Kebwe ndiye alikuwa wa kwanza lakini cha kushangaza wakamuacha.

Kama matokeo yatakuwa kama hapo juu basi Wenyeviti wa Wilaya zilizotajwa na Mwenyekiti wa Mkoa namba tatu wawajibishwe bila kuwaonea huruma kwa ushauri wao mbaya na usio na tija.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom