Kuna magonjwa mengi yanayosababisha upungufu wa Kinga mwilini ikiwemo maambukizi ya VVU.
Kumekuwa na mijadala mingi pamoja na tetesi zinazohitaji majibu ya kina kuhusu uwezekano wa kupata VVU/UKIMWI kutoka kwa mtu aliye athirika hasa ikihusisha ushiriki wa tendo la ndoa pasipo kutumia kinga hata kama ni mara moja tu.
Ukweli upoje na majibu ya kisayansi yanatoa picha gani? Baadhi hudai hauwezi kupata VVU/UKIMWI kwa kufanya tendo moja tu la ngono na muathirika pasipo kutumia kinga kwa kuwa maambukizi hayaji kirahisi hivyo kama tunavyodhani.
Kumekuwa na mijadala mingi pamoja na tetesi zinazohitaji majibu ya kina kuhusu uwezekano wa kupata VVU/UKIMWI kutoka kwa mtu aliye athirika hasa ikihusisha ushiriki wa tendo la ndoa pasipo kutumia kinga hata kama ni mara moja tu.
Ukweli upoje na majibu ya kisayansi yanatoa picha gani? Baadhi hudai hauwezi kupata VVU/UKIMWI kwa kufanya tendo moja tu la ngono na muathirika pasipo kutumia kinga kwa kuwa maambukizi hayaji kirahisi hivyo kama tunavyodhani.
- Tunachokijua
- HIV ama Human Immunodeficiency Virus ni kirusi kinachoshambulia mfumo wa kinga mwili, ambacho baada kuishi mwilini kwa kipindi fulani kinaweza kusababisha upungufu wa kinga mwilini (UKIMWI).
Virusi hawa wenye sifa ya RNA, hubeba aina 15 za protini pia huzungukwa na kuta mbili za mafuta. Hushambulia seli hai zenye vipokeo vya CD4 pekee, hubadilika mara kwa mara pamoja na kupoteza sifa ya kuishi kikiwa kwenye mazingira yasiyo rafiki.
Ili virusi viweze kuingia mwilini na kusababisha madhara huhitaji mambo matatu ya msingi-
- Damu au Majimaji ya mwili
- Kitendo hatarishi
- Upatikanaji wa moja kwa moja wa mishipa ya damu
Kwa kutumia rejea ya CDC, huu ndiyo wastani wa watu wanaopata maambukizi ya VVU/UKIMWI katika kila kundi la watu 10,000 wanaokuwa kwenye mazingira hatarishi kwa mara ya kwanza.
- Watu 9250 kwa kupokea damu
- Watu 63 kwa kushirikiana vitu vyenye ncha kali
- Watu 138 kwa kushiriki tendo la ndoa kinyume cha maumbile
- Watu 8 kwa kushiriki tendo la ndoa kwa njia ya kawaida
Uwepo wa maambukizi ya magonjwa ya zinaa, hatua ya maambukizi ya VVU/UKIMWI, idadi ya nakala za virusi (Viral load) pamoja na udhaifu wa kinga ya mwili ya mhusika huongeza uwezekano wa kupata maambukizi ya VVU/UKIMWI.
Kondomu kama kinga
Kwa mujibu wa USAID, Matumizi ya kondomu husaidia kupunguza maambukizi ya VVU kwa zaidi ya 90%. Ni muhimu kutumia njia hii ili kujilinda dhidi ya gonjwa hili hatari ambalo kwa mwaka 2021 pekee liliondoa uhai wa takriban watu 650,000 duniani.
Kwa kuwa ni ngumu kujua hali ya afya ya mtu kwa kumtazama hasa kwa kuzingatia idadi ya nakala za VVU pamoja na hatua ya ugonjwa kwa wahusika, pia ili kufuta kabisa nafasi ya kuugua ugonjwa huu, ni muhimu kujilinda kikamilifu pamoja na kuepuka mazingira yote hatarishi yanayoweza kufanya uambukizwe.
Aidha, ili kupunguza nafasi ya kuambukiza wengine, waathirika wa VVU wanapaswa kutumia dawa za kufubaza makali ya maambukizi ili kudhibiti utengenezwaji wa nakala mpya za virusi, pamoja na kuongezeka kwa ukubwa wa maambukizi. Wanaofikia kiwango cha chini kabisa cha nakala za VVU hukosa sifa ya kuambukiza wengine.
Usijaribu kushiriki ngono zembe kwa imani kuwa nafasi ya kuambukizwa VVU/UKIMWI ni ndogo. Tendo la mara moja linaweza kukufanya ukanasa kwenye mtego huo.